• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Historia

TAARIFA FUPI YA WILAYA YA MBARALI

UTANGULIZI.

Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa Wilaya tano na Halmashauri saba zinazounda Mkoa wa Mbeya.  Wilaya hii ilianzishwa mnamo tarehe 7 Julai, 2000 kwa mujibu wa vifungu vya 8 na 9 vya Sheria ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982 na kupatiwa cheti kilichosainiwa tarehe 5 June, 2003.

MAHALI ILIPO NA MIPAKA YAKE.

Wilaya ya Mbarali ipo kati ya nyuzi 33.40 na 35.40 Longitudo kuelekea upande wa Mashariki, nyuzi 7.41 na 9.25 kusini ya Ikweta.  Upande  wa Kaskazini Mashariki, inapakana na Wilaya ya Iringa Vijijini, upande  wa Mashariki inapakana na Wilaya ya Njombe, upande wa Kusini  kabisa inapakana na wilaya ya Mbeya na Kaskazini inapakana na Wilaya ya Chunya.

1.2. ENEO NA MATUMIZI YA ARDHI.

Wilaya ina jumla ya eneo la Kilometa za mraba 16,000 na mgawanyo wa matumizi ya ardhi ni kama inavyoonyesha kwenye jedwali No. 1.

JEDWALI I:

NA

MATUMIZI YA ARDHI

KM ZA

MRABA

HEKTA

ASILIMIA

YA UWIANO

1

Ardhi kwa  ajili ya kilimo

3,215

321,500

20.09

2

Eneo la wanyama pori

5,200

520,000

32.5

3

Hifadhi ya Misitu

172

17, 200

1.1

4

Eneo la makazi

6,078

607,800

38.0

5

Uwanda wa Tambarare, vilima, maeneo oevu na ufugaji

2,590

259,000

16.2

 

JUMLA

16,000

1,600,000

108

 

 

1.3. SURA YA NCHI

Wilaya ya Mbarali ipo uwanda wa chini wa tambarare wenye nyasi na sehemu kubwa ya Wilaya imepitiwa na Bonde la Ufa na maeneo yenye miinuko kwa upande wa Magharibi, ikiwa na mito mitatu ya kudumu.  Vile vile Wilaya ina chanzo kikuu cha maji ambacho ni Mto Ruaha Mkuu ambao baadaye huungana na mto Rufiji na kumwaga maji katika Bahari ya Hindi.

Wilaya imegawanyika katika kanda tatu za KIIKOLOJIA ambazo ni Uwanda wa Msangaji, Uwanda wa kati wa Usangu na Tambarare za Kusini mwa Usangu.

JEDWALI II:

NA

KANDA

MAHALI ILIPO

ALTITUDE (M)

UDONGO WA MVUA

SHUGHULI KUU ZA KIUCHUMI

1

Uwanda wa Msangaji (kanda ya Kaskazini)
 Ruaha National Park

1200-1800

Udongo wa mawe wenye rutuba ndogo
Mvua milimita 500-900 kwa Mwaka
Unyevunyevu miezi 3-5
Eneo lipo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA)

2

Uwanda wa kati wa tambarare  ya Usangu (Ukanda mkuu wa ufugaji)
Ruiwa
Ut/Usangu
Rujewa
Mapogoro
Sehemu ya kata ya Mawindi

1000-1400

Udongo mweusi na kichanga
Mvua mm 450-650 kwa mwaka
Unyevunyevu miezi 3-4
Kilimo cha mazao ya:
Mtama
Uwele
Ufugaji
Mahindi
Mpunga

3

Tambarare za Kusini  Usangu (ukanda wa kusini – kanda ya kilimo)
Ilongo
Rujewa
Chimala
Mapogoro
Igurusi
Ubaruku

750-1000

Mvua haba mm 360-750
Kilimo cha mazao ya:
Mahindi
Karanga
Pamba
Kilimo cha umwagiliaji Mpunga
Ufugaji

 

1.4. HALI YA HEWA NA UOTO

Wilaya ya Mbarali ipo katika latitude inayoanzia mita 1,000 – 1,800 juu ya usawa wa Bahari.  Wastani wa joto ni kati ya nyuzi 25c na 30c.  Wastani wa mvua hutofautiana kati ya milimita 300-940, hata hivyo kuna misimu miwili yaani msimu wa kiangazi ambao huanzia mwezi Mei – Novemba na msimu wa mvua ambao huanza Desemba – Aprili

Kwa ujumla Wilaya yote iko ndani ya uwanda wa Tambarare katika Bonde la Usangu ambalo lina uoto wa Asili aina ya Mipogoro.

Hali ya Mvua kwa Miaka Mitano iliyopita ni kama ifuatavyo:

NA

MWAKA

WASTANI WA MVUA (MM)

1

2005/2006

300.00

2

2006/2007

800.00

3

2007/2008

450.00

4

2008/2009

400.00

5

2009/2010

412.80

6

2010/2011

428.00

7

2011/2012

473.96

8

2012/2013

216.48

9

2013/2014

770

Hali hii ya upunguaji wa Mvua, inaathiri sana uzalishaji wa mazao ya kilimo hususani mpunga ambao ndio tegemeo kuu la mapato yetu ya ndani.

 

 

1.5. MUUNDO WA UTAWALA  NA MAKABILA.

Muundo  na utawala wa Wilaya ya Mbarali ni kama inavyoonyesha kwenye jedwali.

JEDWALI III

TARAFA

MAJIMBO YA UCHAGUZI

KATA

VIJIJI

VITO NGOJI

KAYA

WAH. MADIWANI

KUCHAGU

LIWA

KUTEULIWA

JML

2

1

20

103

713

69,888




 

1.6 MAKABILA

Makabila makuu yaliyopo Wilayani Mbarali ni Wasangu, Wahehe, Wakinga, Wabena na Wanyakyusa.  Vile vile yapo makundi madogo ya makabila wakiwemo Wasukuma, Wanji, Wabarbeig na Wagogo.

Makundi mengi ya makabila haya ni wakulima na wafugaji ambao walihamia bonde la Usangu kutoka Mikoa ya Arusha, Mwanza, Shinyanga, Singida na Dodoma.

1.7. IDADI YA WATU

Kufuatia sensa ya kitaifa ya idadi ya watu ya mwaka 2012, Wilaya ya Mbarali sasa ina jumla ya watu 300,517 ambao kati yao 145,867ni wanaume na 154,650 ni wanawake ikiwa na ukuaji wa 2.8%.

1.8. IDADI YA WATUMISHI.

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ina jumla ya watumishi 2,527. Mahitaji ni watumishi 2,971 hivyo kuna upungufu wa watumishi wapatao 1,012 kama jedwali linavyoonyesha hapa chini;

JEDWALI IV

Na

IDARA/KITENGO

IKAMA ILIYOIDHINI SHWA

WATUMISHI WALIOPO

UPU NGUFU

ZIADA

1

Utawala na Utumishi

144

130

14

-

2

Fedha na Biashara

22

19

3

-

3

Mipango,Takwimu na Ufuatiliaji

6

5

1

-

4

Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika

134

83

51

-

5

Mifugo na Uvuvi

128

48

80

-

6

Elimu ya Msingi

1648

1193

455

-

7

Elimu ya Sekondari

495

434

61

-

8

Maji

13

7

6

-

9

Ujenzi

30

21

9

-

10

Afya

688

365

323

-

11

Ardhi na Maliasili

26

21

5

-

12

Maendeleo ya Jamii

27

23

4

-

 

JUMLA

2,971

2,527

1,012

-

 

 

1.9: MWENENDO WA MAPATO NDANI YA HALMASHAURI

Halmashauri imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo na ustawi wa jamii kupitia Mapato yake ya Ndani yanayotokana na vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushuru wa mazao, ushuru kutokana na huduma mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri. Mwenendo wa mapato ya ndani ya Halmashauri ni kama ifuatavyo:-

 

JEDWALI V

NA

MWAKA

MAKISIO

MAPATO

ASILIMIA (%)

1

2007/2008

319,882,060

487,449,295

152

2

2010/2011

478,894,538

666,742,372

139

3

2009/2010

       721,124,000

    639,527,000

88.7

4

2010/2011

       728,757,700

    621,890,570

85.3

5

2011/2012

773,027,000

934,388,639

121

6

2012/2013

1,348,748,000

915,496,546

67.9

7

2013/2014

1,602,798,000

1,396,807,050.55

87.1

8

2014/2015

2,672,063,706

1,921,741,556.72

72

 

 

2.0: SHUGHULI ZA KIUCHUMI.

Uchumi wa Wilaya ya Mbarali unategemea kwa kiwango kikubwa uzalishaji wa mali vijijini hasa sekta ya Kilimo, wastani wa asilimia 83  ya wakazi Wilaya ya Mbarali hujishughulisha na kilimo, shughuli zingine za kiuchumi ni pamoja na ufugaji, uvuvi na biashara ndogondogo; kwa ujumla wake pato la mkazi wa Mbarali ni shilingi 376,500/= kwa mwaka.                                       

2.1 KILIMO

Asilimia 83 ya wakazi wa Wilaya ya Mbarali hujishughulisha na kilimo na ufugaji.  Mazao muhimu ya chakula ni pamoja na Mpunga, Mahindi, Viazi vitamu, Mihogo, Maharage na Mtama.  Hata hivyo mpunga huzalishwa kama zao la chakula na biashara.  Mazao ya biashara ni Alizeti, Karanga na Mazao ya bustani.

Kutokana na hali ya hewa isiyotabirika na kupungua kwa mvua, Halmashauri imekuwa inawekeza katika Kilimo cha umwagiliaji.

Mpaka sasa, Wilaya ya Mbarali ina jumla ya skimu za umwagiliaji 80 zenye jumla ya hekta 78,953. Kati ya hizo skimu 34 zimeboreshwa zenye jumla ya eneo linalofaa kulimwa hekta 41,724 lakini zinazolimwa ni 23,519. Aidha skimu 46 hazijaboreshwa zengye jumla ya eneo linalofaa kulimwa hekta 37,229 lakini zinazolimwa ni 20,989.

 

Juhudi zinaendelea za kuboresha miundombinu ya skimu za kilimo cha umwagiliaji, kuwajengea uwezo wakulima ili waweze kuzalisha kwa tija zaidi, Ujenzi wa miundombinu ya masoko (maghala na viwanda vya usindikaji) na kuboresha barabara za vijijini  zipitike kwa urahisi.

2.2. MALIASILI

Wilaya ina utajiri wa maliasili mbalimbali ikiwa ni pamoja na misitu, wanyamapori, madini, ufugaji nyuki, samaki na sehemu ya hifadhi ya Taifa Ruaha, vilevile pori la akiba la Usangu.

3.0 HUDUMA ZA KIJAMII NA FURSA ZILIZOPO

3.1 ELIMU

Wilaya ina shule/vyuo kama ifuatavyo:

Jedwali vII

NA

AINA YA SHULE

SERIKALI

BINAFSI

TAASISI

JUMLA

1

Shule za awali

100

-

2

102

2

Shule za msingi

103

2

-

105

3

Shule za sekondari

16

1

6

23

4

Vituo vya EWW

5

-

-

5

5

Vituo vya MUKEJA

12

-

-

12

Idadi ya wanafunzi wa shule za msingi                    51,999

Idadi ya wanafunzi wa shule za sekondari               9,580

Idadi ya walimu shule za msingi                                1,193

Uwiano wa walimu na wanafunzi                              1:44

Kwa Mwaka wa masomo 2013 kiwango cha  ufaulu kwa Elimu ya Msingi ni 70.0%

Wanafunzi waliofaulu na kuchaguliwa kuingia Sekondari ni 4143.Wanafunzi hao wote walipata nafasi ya kujiunga na Kidato cha Kwanza.

Kiwango cha ufaulu Kwa Elimu ya Sekondari ni; Kidato cha pili 94.87% na Kidato cha nne 71.23% (83.23%).

 

Aidha kwa upande wa Walimu hali halisi iko kama ifuatavyo:

JEDWALI VII

Sekta

Idadi ya Walimu

Asilimia ya Upungufu

Wanaohitajika

Waliopo

Upungufu

Elimu ya Msingi

1299

1193

106

8

Elimu ya Sekondari

597

506

91

15

 

 

 

 

3.2 AFYA

Wilaya ina vituo vya kutolea huduma ya afya kama ifuatavyo:

JEDWALI VIII

NA

VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA

SERIKALI

BINAFSI

TAASISI

JUMLA

1

Hospitali

1

-

1

2

2

Kituo cha afya

5

-

1

6

3

Zahanati

34

2

4

40

Kwa upande wa Rasilimali watu katika Idara ya Afya, hali iko kama ifuatavyo:

 

Shule

Idadi ya Watumishi

Asilimia ya Upungufu

Wanaohitajika

Waliopo

Upungufu

Hospitali ya Wilaya

211

164

47

22.3

Afya Kinga

26

11

15

57.7

Vituo vya Afya 5

195

87

108

55.4

Zahanati 34

510

185

325

63.7

JUMLA

942

447

495

52.5

3.3 MAJI

Wilaya ya Mbarali ina mtiririko wa mito inayoanzia safu ya milima ya kipengele na uproot, vyanzo hivi vimekuwa mtego wa maji ya bomba kwa vijiji 76 kati ya 93 vya Wilaya nzima.

JEDWALI VI:

NA

VYANZO VYA MAJI

IDADI

IDADI YA VIJIJI VINAVYONUFAIKA       NA HUDUMA

IDADI YA  WATU      WANAONUFAIKA NA HUDUMA

1

Miradi ya kutegwa (gravity scheme)

10

52

160,848

2

Visima virefu (Borehole)

36

15

36,104

3

Visima vifupi (Borehole)

47

10

13,533

 

JUMLA

93

77

210,485

3.4 BARABARA

Wilaya  ina mtandao  wa barabara zilizoanzishwa zenye urefu wa km 1,308.2 ambazo kati ya hizo, barabara zenye urefu wa km 305.5 zinahudumiwa na meneja wa TANROADS na km 1002.7 zinahudumiwa na Halmashauri. Barabara zinazohudumiwa na Halmashauri zimegawanyika kama ifuatavyo;

JEDWALI VII

NA

AINA YA BARABARA

UREFU

1

Barabara ya changarawe

Km 216.15

2

Barabara ya changarawe/udongo

Km 786.55

Aidha kuna km 555.95 ambazo hazijaandikishwa na zinahudumiwa na Halmashauri, baada ya kupitishwa na Baraza la Madiwani mwaka 1998 ili kuweza kufikia maeneo ya uzalishaji na utawala, ili kuboresha ujenzi wa uchumi katika Wilaya.  Kati ya km 555.95 km 86.7 ni za changarawe na km 469.25 ni za udongo.

3.5 VYAMA VYA USHIRIKA

Vyama vya ushirika ni vyombo muhimu katika kumkomboa mwananchi kutokana na umaskini.  Hali ya vyama vya ushirika katika wilaya ya Mbarali ni kama ifuatavyo:

JEDWALI VIII

NA

 

AINA YA USHIRIKA

WANACHAMA

MTAJI

Tshs.’000,000

MIKOPO Tshs.’000’000

IDADI

MOJA

MOJA

VIKUNDI

JUMLA

HISA

AMANA

AKIBA

TOLE

WA

REJESHA

1

Ushirika wa Akiba na Mikopo

24

7,191

209

7,400

1282.5

430.9

2028.8

23.404.7

14,347.3

2

Ushirika wa usafirishaji wa mazao ya kilimo

3

86

-

86

12.4

-

-

-

-

3

Ushirika wa kilimo na masoko

8

4,168

14

4,182

316.6

-

-

-

-

4

Ushirika wa wafugaji

1

18

-

18

0.64

-

-

-

-

5

Ushirika wa kilimo na umwagiliaji

9

2,808

8

2,816

12.3

-

-

-

-

6

Ushirika wa biashara ya samaki

4

170

0

170

13.85

-

-

-

-

7

Wabeba mifugo

1

19



1





 

JUMLA

50

15397

2028

15705

2593

378

2581

15801

12318

 

 

3.6. VIKUNDI VYA KIUCHUMI VYA WANAWAKE NA VIJANA

Katika kuhakikisha umaskini unapungua kwa jamii wa wilaya ya Mbarali huduma ya mikopo kwa vikundi vya kiuchumi vya wanawake na vijana imekuwa ikitolewa tangu mwaka 1998 hadi 2013 kama inavyoonyesha:-      

                                                                                                                            

JEDWALI IX: 

MWAKA

VIKUNDI

MKOPO TOLEWA

RIBA (10%)

MKOPO + RIBA

MAREJESHO

BAKI

% YA MAREJESHO

Bakaa 2006

82

70,993,000

9,122,800

80,115,800

79,626,554

1,233,454

99.39

2007

17

18,000,000

1,800,000

19,800,000

19,590,000

210,000

98.93

2008

14

15,200,000

1,520,000

16,720,000

16,180,000

540,000

96.77

2009

4

4,000,000

400,000

4,400,000

4,400,000

0

100

2010

12

10,350,000

1,755,000

11,385,000

11,385,000

0

100

2013

3

6,000,000

600,000

6,600,000

4,600,000

2,000,000

69.69

JUMLA

32

124,543,000

15,197,800

139,020,800

135,781,554

3.983,454

97.66

MIKOPO YA WANAWAKE CHINI YA  MFUKO WA WDF

 

 

JEDWALI X: 

MIKOPO YA VIKUNDI VYA VIJANA KUTOKA SERIKALI KUU NA H/WILAYA

MWAKA

KIKUNDI

MKOPO TOLEWA

RIBA (15%)

MKOPO + RIBA

MAREJESHO

BAKI

%

2006

7

3,000,000

450,000

3,450,000

3,450,000

-

100

2007

18

6,900,000

1,035,000

7,935,000

7,497,000

438,000

94.48

2008

4

2,000,000

300,000

2,300,000

1,885,000

415,000

81.96

2009

2

10,000,000

500,000

10,500,000

10,475,500

  24,500

9977

JUMLA

25

21,900,000

2,285,000

24,185,000

23,307,500

24,500

 

4.0: MIFUGO NA HUDUMA (MIUNDO MBINU)

Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa wilaya zenye ufugaji mkubwa wa mifugo kwa njia ya kienyeji na kisasa.

JEDWALI XI: 

MIFUGO

NA

MFUGO

AINA YA MIFUGO

JUMLA

MAZIWA

NYAMA

MAYAI

KIENYEJI

1

Ngo’mbe

2,524

-

-

168,580

171,104

2

Mbuzi

71

-

-

83,302

83,373

3

Kondoo

-

-

-

38,491

38,491

4

Punda

-

-

-

4,081

4,081

5

Mbwa

-

-

-

11,789

11,789

6

Nguruwe

-

-

-

11,889

11,889

7

Kuku

-

-

4,273

245,780

250,053

8

Bata

-

-

-

33,125

33,125

9

Bata Mzinga

-

-

-

53

53

10

Kanga

-

-

-

2,612

2,612

11

Paka

-

-

-

3,911

3,911

JUMLA

2,595

-

      4,273 
603,613

610,481

 

 

JEDWALI LA XII: 

MIUNDO MBINU (HUDUMA)

NA

MIUNDO MBINU

ILIYOPO

INAYOFANYA KAZI

MIBOVU

MAELEZO

1

Majosho

32

26

6

6 yanahitaji ukarabati.

2

Machinjio kubwa (Slaughter House)

9

9

-

6 Yanahitajika kujengwa

3

Machinjio ndogo (Makaro)

17

17

-

Yanafanya kazi

4

Malambo

5

3

2

2 yanahitaji ukarabati.

5

Mabanda ya ngozi

3

3

3

3 Yahahitaji ukarabati na 6 yanahitaji kujengwa

6

Minada

7

7

7

7 inatakiwa kuboreshwa

7

Vituo vya afya (VHC)

7

7

7

7 vinatakiwa kujengwa

8

Vituo vya kupakia/kushushia mifugo

2

1

1

6 vinatakiwa kujengwa na 1 kinahitaji ukarabati

9

Maduka ya pembejeo za mifugo

21

21

-

Yanafanya kazi

10

Mabirika ya kunyeshea Mifugo

8

6

2

2 yanahitaji ukarabati na 9 yanahitaji kujengwa

5.0: UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA MWAKA 2013/2014.

 

Katika kipindi cha mwaka 2013/2014, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ilipokea jumla ya Sh.8,348,327,271 kwa ajili ya miradi ya maendeleo kutoka Serikali Kuu na Wahisani mbalimbali. Vilevile Halmashauri ilikuwa na salio anzia la Sh.334,495,245 na hivyo kufanya kuwa na jumla ya Shs.8,348,327,271.  Kati ya fedha hizo Sh.7,399,192,417 sawa na 88% zilitumika na Sh.949,134,854.29 sawa na 12% zikiwa ni bakaa kama inavyoonyeshwa katika jedwali lifuatalo:

Salio anzia (Sh)

Mapato (Sh)

Jumla ya Mapato (Sh)

Matumizi (Sh)

Bakaa (Sh)

334,495,245

8,013,832,026

8,348,327,271

7,399,192,417

949,134,854.29

 

Fedha hizo zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya sekta mbalimbali. Mchanganuo ufuatao hapa chini unaonyesha mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 kulingana na taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kufikia tarehe 30 Juni, 2014.

 

 

6.0. HALI YA MAZINGIRA 

6.1 MISITU

Eneo la Misitu ya asili na Nchi kavu lina ukubwa wa km za mraba 7604.6, eneo lenye misitu ya Hifadhi ni km za mraba 17.4 eneo lenye misitu iliyopendezwa kuwa hifadhi ni km za mraba 162.  Wakati uwanda wa tambarare na ardhi oevu lina ukumbwa wa km za mraba 776.

6.2. UVUVI

Hali ya uvuvi Wilayani Mbarali hutegemea zaidi Mto Ruaha mkuu, Tindiga la Ihefu, Mito, na Mabwawa.  Mpaka sasa kuna  mabwawa 260 ambapo 231 yanamilikiwa na watu binafsi na moja ni la Halmashauri ya Wilaya.

6.3. WANYAMA PORI

Eneo la pori la akiba ni kilomita za mraba 5200, eneo la mapori ya wazi huchukua kilometa za mraba 11,852.  Aidha  kuna aina  mbili za uwindaji ndani ya wilaya (uwindaji wa kitalii na uwindaji wa kienyeji).

6.4. MIJI NA MAKAZI

Wilaya ya Mbarali ina Mamlaka ya mji mmoja mdogo wa Rujewa ambao ndio makao makuu ya Wilaya na miji midogo sita (Madibira, Ubaruku, Chimala, Igurusi, Ut/Usangu na Ruiwa. Kati ya miji hiyo ni miji 4 iliyoandaliwa mipango ya matumizi ya ardhi (Planning Proposals).

6.5 VYANZO VYA MAJI

Hali ya vyanzo vya maji katika Wilaya si nzuri kwani vyanzo vingi vimeathiriwa na ukataji wa miti ya asili, uchomaji wa moto na uchungaji wa mifugo kiholela na kulima kwenye vyanzo vya mito.

6.6. KILIMO

Maeneo mengi ya kilimo yako wazi kwa sababu ya ufyekaji wa miti na vichaka kwa ajili ya kilimo. Aidha mashamba yaliyoko mabondeni hujaa maji kutokana na mafuriko baada ya mito kujaa maji. Pia kupitia mradi wa kilimo cha kijani kibichi, miche ya miti rafiki na mazao ya kilimo inakuzwa kwenye vitalu na kusambazwa kwa wananchi katika vijiji 25 mwaka 2012/2013 jumla ya miche ya mipogoro na matunda ilikuzwa na kusambazwa.

6.7 MIFUGO

Wilaya ya Mbarali ina eneo la km za mraba 16,000 na kati ya hizo km za mraba 1,485 zinatumika kwa malisho ya mifugo.

7.0. VIKWAZO /VIZINGITI

7.1. UKIMWI

Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi imekuwa ni tatizo kubwa katika wilaya ya Mbarali kwani umekuwa ukiathiri makundi mbalimbali hasa vijana ambao ndiyo nguvu kazi kubwa katika uzalishaji na matokeo ya upimaji wa Virusi vya Ukimwi ni kama inavyoonyesha.

JEDWALI LA XIII: 

MWAKA

WALIOPIMA

WALIOKUTWA NA MAAMBUKIZI

% YA MAMBUKIZI

2002

  946

136

14.4

2003

  673

96

14.3

2004

 932

141

15.1

2005

1,358

598

44.0

2006

               1,317

548

41.6

2007

              16,504

5,109

30.9

2008

                7,513

3,005

39.9

2009

8,624

3,127

36.2

2010

6,362

2,053

32,2

2011

8,897

512

5.8

2012

10,375

924

8.9

2013

13,312

1,472

11

2014

16,445

2,544

15

7.2. MAGONJWA MENGINE

Magonjwa 10 makuu yanayoongoza kwa vifo kwa mwaka 2014/2015 kama inavyoonyesha hapo chini:-

 

JEDWALI LA XIV: 

NA

MAGONJWA

CHINI YA MIAKA 5

ZAIDI YA MIAKA 5

WAGO-NJWA

VIFO

WAGO-NJWA

VIFO

1

Vichomi

1,763

25

2,131

34

2

Magonjwa ya njia ya hewa

853

8

769

26

3

Kuhara

853

0

769

26

4

Malaria

676

26

1,167

32

5

Magonjwa ya watoto wachanga

192

10

0

0

6

Ajali

103

25

818

5

7

Upungufu wa damu

89

18

316

0

8

Kuungua

67

5

47

0

9

Sumu

40

5

97

9

10

UKIMWI

20

3

382

20

 

JUMLA 

4,656

125

6,496

152

8.0: UIMARA

Halmashauri ina umri wa miaka kumi na moja (11) na ni mtoaji wa huduma zote kwa jamii yake.  Uimara ufuatao umeifanya Halmashauri kuwa ni chombo kinachotegemewa kuwa mtoaji wa huduma zake:-

  • Uwezo wa kufanya kazi  kwa kushirikiana  na wadau wengine
  • Kuwepo na Tindiga la Ihefu
  • Miundo mbinu ya kilimo na mifugo.
  • Uwezo wa kupitisha/kutumia sheria ndogo ili kuhimiza utoaji wa huduma
  • Uzoefu wa kutumia rasilimali zake vizuri
  • Wataalamu wenye ujuzi na uzoefu.

9.0. CHANGAMOTO

Halmashauri inatambua kuwa na udhaifu ufuatao:-

  • Uvamizi wa wafugaji wa mifugo yao katika bonde la Usangu hasa katika  Tindiga la Ihefu, ambalo lina hifadhi  mtiririko wa maji yanayotumika kutoa umeme katika bwawa la Mtera.
  • Matukio ya uchomaji moto ovyo kwenye misitu na mapori ya hifadhi.
  • Uhaba wa masoko ya uhakika ya mazao mbalimbali ya kilimo.
  • Njia duni za mawasiliano hasa barabara hivyo kufanya baadhi ya maeneo kutofikika kipindi cha masika.
  • Wingi wa Mifugo.
  • Kuchelewa kutolewa fedha kutoka Hazina na Wadau wengine wa maendeleo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Adha baadhi ya miradi ya maendeleo kutoletwa fedha zake zilizotengwa kwenye bajeti.
  • Uhaba wa nyumba za kuishi watumishi.
  • Upungufu wa watumishi.
  • Mapato kupotea kutokana na mianya iliyokuwepo katika mikataba iliyopita  ya mikusanyo ya ushuru.
  • Kupungua kwa mapato kutokana na uzalishaji mdogo wa mazao ya kilimo kutokana na upungufu wa mvua.
  • Migogoro ya ardhi.

10.0. MKAKATI INAYOCHUKULIWA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

MIKAKATI YA MUDA MFUPI:

  • Kuhuisha ushuru wa huduma.
  • Kuandaa makisio yatokanayo na uzalishaji mazao.
  • Kutoa elimu kwa walipa kodi ili waweze kulipa ushuru/kodi.
  • Kuchukua hatua za kisheria kwa wakiukaji.
  • Kuboresha sheria ndogo za ukusanyaji ushuru.
  • Kuimarisha kitengo cha ukusanyaji ushuru.
  • Kuboresha mikataba ya ukusanyaji ushuru.
  • Kutoa elimu ya sheria ya ardhi na utatuzi wa migogoro.                                                                                                                                                                                                                    

MIKAKATI YA MUDA MREFU:                                                                                                           

  • Kuboresha miundombinu ya masokoya mazao ya kilimo na mifugo.                               
  • Ujenzi wa kituo cha maegesho ya magari makubwa.                                                                    
  • Uanzishaji wa kiwanda cha kusaga kokoto  -2013/14                                                           
  • Kuanzisha mradi wa ukodishaji wa mitambo ya ujenzi wa miundombinu-2013/14.                                                                                                  
  • Kuboresha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji -2007/2008.                                              
  • Mradi wa unenepeshaji mifugo  -2014/15.  

Usindikaji wa mazao ya kilimo ili kuongeza thamani.

Kuimarisha mfumo wa stakabadhi za mazao ghalani.

Kuimarisha barabara za vijijini na za kwenda mashambani kupitia DADP, TASAF, Road Fund na wahisani mbali mbali.

Kuboresha uzalishaji wa kilimo na ufugaji kwa kuwezesha wakulima kupitia vikundi kupata zana bora, mbegu bora, uhamilishaji (usambazaji wa madume bora), mashine za kupandia na kuvuna mpunga.

Ujenzi wa nyumba za watumishi kadri fedha zinavyopatikana.

                                                                               

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI April 16, 2021
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • KANUNI ZA UTOAJI NA USIMAMIZI WA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU TANGAZO LA SERIKALI NA. 217LA TAREHE 26.02.2021 March 02, 2021
  • MUHTASALI WA BAJETI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI YA MWAKA 2021-2022 February 11, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC AZITAKA KAYA ZINAZOWEZESHWA NA TASAF KUFUGA KUKU, BATA WA ASILI

    March 03, 2021
  • PESCODE VICOBA YATOA MEZA NA VITI 52 MBARALI

    February 26, 2021
  • TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

    February 11, 2021
  • Fanyeni Kazi kwa Bidii kwa Kutumia Taaluma zenu-DC Mbarali

    January 30, 2021
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255713317374

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2018 GWF. Haki zote Zimehifadhiwa.