• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KILICHOJIRI KWENYE MAHOJIANO YA LIVE BOMBA FM SIKU YA TEREHE 03/07/2021 MKUU WA WILAYA YA MBARALI

Tarehe ya Kuanza: July 4th, 2021

KILICHOJIRI KWENYE MAHOJIANO YA LIVE BOMBA FM SIKU YA TEREHE 03/07/2021 MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE. REUBEN MFUNE ALIPOONGOZANA NA BAADHI YA WATAALAM KUTOKA TAASISI MBALIMBALI ZINAZOJITEGEMEA

 

MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE REUBEN MFUNE

Nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hasan kwani kwa mwezi juni Tumepokea kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya utengenezaji wa barabara ya kutoka chimala hadi kapunga yenye umbali wa km 26.

Vilevile tumepokea kiasi cha shilingi milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi 3 za wagonjwa kwenye hospitali yetu mpya ya wilaya.

Mwaka ujao 2021 kwa idadi tuliyonao ya wanafunzi wa darasa la 7 tutakuwa na upungufu wa vyumba vya madarasa 127, tumeshapeana upungufu na nimeshatoa maelekezo ya vitu vya kufanya kwani muda wa kuanza ujenzi ni sasa.

Niwaombe wananchi tutumie fursa hii kuhakikisha watoto wetu wanasoma katika mazingira bora kwa kushiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Mtu wa kwanza kuanza kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa CORONA ni wewe mwenyewe usisubiri hadi uambiwe na Serikali, Mhe. Rais ameshaelekeza wananchi tuchukue hatua na tunapokea maelekezo ya Viongozi mbalimbali wa kitaifa kupitia vyombo vya habari, tuamini zile ni taarifa rasmi, usisubiri kuambiwa na mtu mwingine.

Nampongeze Meneja wa TANESCO kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya na timu yake, amekuwa akitoa ushirikiano mkubwa, na tunakoelekea tatizo la umeme litakuwa historia.

Nitoe wito kwa wananchi kubadilika, hakuna malipo ya Serikali yanayofanyika mkononi malipo yote yanafanyika kwa kutumia control namba ambayo unapewa na TANESCO na kwa wale wanaofanya ujanja ujanja nawaomba wananchi wawe wanatoa taarifa mapema ili tuwashughulikie.

Hali ya upatikanaji wa maji sio nzuri ila kuna juhudi za kuridhisha na hadi sasa imefanyika kazi kubwa na kazi inaendelea kwani tangu amekuja meneja mpya naona anafanya kazi nzuri sana.

Nilishapiga Marufuku kwa vijiji na skimu za umwagiliji kukopa kwa watu binafsi, kuna taasisi za za kifedha zilizo rasmi, wananchi waende wakakope huko kwa ajili ya shughuli zao za kilimo.

Suala la vipimo tupo vizuri, ofisi yangu kwa kushirikiana na Wakala wa Vipimo tulishatoa maelekezo maeneo yote ya Mbarali.

Tulipiga marufuku mifuko yenye ujazo mkubwa yenye mistari ya rangi nyekundu ambayo ina ujazo wa kilo 140 na tuliruhusu yenye mistari ya rangi ya kijani na blue ambayo ujazo wake ni kilo 100, kwa sasa hatujafikia hatua ya kuweka mizani kwa kila kijiji.

Kwa mwaka ujao wa mavuno 2022 tutakuwa na vituo vya kuuzia mazao vitakavyotumia mizani

Kuhusiana na bei ya mazao, mazao kwa sasa yanaendeshwa na soko lililopo, tuna Maghala ya Serikali ya kuhifadhia nafaka ambayo yapo ili mkulima ahifadhi kusubiri soko zuri.

Tuna mifugo Zaidi ya laki 2, lakini uwezo wa maeneo ya malisho ni kuwa na mifugo 65,000 ili tuweze kuondoa tatizo la muingiliano kati ya wafugaji na wakulima itafika muda lazima tupunguze mifugo ili iendane na maeneo ya malisho tuliyonayo.

Tuna utaratibu wa kusikiliza kero za wananchi kila siku za Jumanne kwenye ngazi ya kata, kwa yale ambayo yatashindikana huko tuna dawati kila siku ya Alhamasi kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya, lakini tunakusudia kufanya wiki la utatuzi wa kero ambalo tutawaita watoa huduma wote ili mtu atoe kero zake na zitatuliwe siku hiyo hiyo.

MHANDISI WA UMWAGILIAJI WILAYA KAROLI RIHALA

Kwa sasa hatuhamasishi kilimo cha umwagiliaji sababu Mbarali watu wameshaelewa faida ya kilimo hicho, tunachokifanya ni kutoa elimu ya umwagiliaji ikiwemo matumizi sahihi ya maji. Kwa sasa wastani mkulima anapata zaidi ya gunia 25 kwa hekali moja ya mpunga.

MENEJA WA TANESCO MHANDISI NICODEMUSI KAPANGE

Vijiji 82 kati ya 102 vilivyopo Mbarali vimeshaunganishiwa huduma ya umeme. Kwa sasa tunamalizia vijiji 20 vilivyobaki na baada ya hapo tutaanza kuunganisha kwenye vitongoji.

Kuna watu wanaojurikana kama vishoka wamekua wakiingilia shughuli za TANESCO wamekuwa wakiwatoza wananchi pesa ili wawaunganishie umeme, tunaendelea kuwashughulikia hao watu na mara tunapopata taarifa huwa tunawafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Gharama ya kuunganishiwa umeme ni shilingi 27,000 na tangu kulipia inachukua siku 30 tu mteja anakuwa ameshaunganishiwa umeme.

Shida tunayoipata wananchi wengi wanawapa pesa wakandarasi wanaotengenezea mifumo ya umeme kwenye nyumba zao ili wawasaidie kulipia umeme. Usimkabidhi mtu pesa akakulipie umeme, mara nyingi fedha hizo hazifiki sehemu husika nawashauri wananchi waje kwenye ofisi zetu kulipia ili wapatiwe huduma kwa haraka.

Hadi sasa tumebadili nguzo 232 zenye urefu wa mita 12 na tumekata miti iliyo kwenye njia kuu ya umeme umbali wa kilometa 234 hii yote ni kuhakikisha suala la kukatika umeme Mbarali linakuwa historia

WAKALA WA VIPIMO EMMANUEL MALANGA

Ndoo sio kipimo sahihi kupimia mazao, kile ni kifungashio au kibebeo, kipimo sahihi ni mzani ambao umekaguliwa na Wakala wa Vipimo.

 

MENEJA WA RUWASA MHANDISI HECHEI SAMWELI

Vijiji 25 ambavyo havijafikiwa na huduma ya maji vipo kwenye mpango kwa mwaka huu wa fedha 2021/2022, kwani tumetenga kiasi cha shilingi bilioni 2.3. Na vijiji ambavyo miradi yake imechakaa tumetenga kiasi cha shilingi milioni 450 kwa ajili ya ukarabati.

Kwa sasa tunaendelea kutoa elimu ya matumizi ya maji kwani maji ni uhai, lazima tuyatunze ili tuweze kuyagawanya kulingana na mahitaji.

 

KAIMU MENEJA WA TARURA JAMES MKIDANGE

Tuna mtandao wa barabara za kawaida wa km 645 na zilizowekwa Rami tangu kuanzishwa kwa TARURA ni km 1.23. Na zile nyingine za Rami zipo chini ya TANROAD.

Kwa mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.4 Ili kurekebisha miundombinu ya barabara.

AFISA LISHE: BI ZUBEDA MAHENGE

Kuna makundi 6 ya chakula ambayo tunatakiwa tuyatumie ili kuweza kuwa na lishe bora na kuondoa utapiamlo Mbarali, makundi hayo ni 1. Nafaka, mizizi na ndizi za kupika. Mfano mchele, mahindi, ngano, mtama, mihogo, viazi, magimbi 2. Vyakula vya asili ya wanyama  na jamii ya kunde pamoja na wadudu aina zote. Mfano maziwa, nyama, mayai, njegere, njugu, senene na kumbikumbi.

3. Mboga mboga mfano mchicha, figiri, karoti, hoho, bamia, nyanya 4. Matunda mfano chungwa, papai, parachichi, pera, nanasi, 5. Sukari, mafuta na asali. Mafuta yanayotokana na mimea ndiyo yanayoshauriwa na 6. Maji.

Masuala ya lishe kipindi cha nyuma yalikuwa hayasikiki, tumejitahidi kutoa elimu na kwa sasa wananchi wengi wanafahamu, hii ni shughuli endelevu huwa tunatumia njia ya kampeni kwenye vijiji ili kutokomeza utapamlo

Tumewajengea uwezo watoa huduma 2 kwa kila kijiji ili waweze kupita nyumba kwa nyumba kutoa elimu kwa walengwa kwani watu kila siku wanazaliwa.

MGANGA MKUU WA HALMASHAURI: DR. GODREY MWAKALILA

Tusiwe na hofu na tuendelee kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona, tunakumbushwa kufuata taratibu zote za afya zilizotelewa na viongozi wakuu wa nchi pamoja na wizara ya Afya zikiwemo kuvaa barakoa sehemu zenye mikusanyiko, kuepuka misongamano isiyo ya lazima na tuwe na utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuifanya miili yetu kuwa imara.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DED MPYA AWASILI MBARALI

    June 30, 2025
  • KIKAO CHA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI NA WATUMISHI WOTE WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

    June 16, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI YAPATA HATI SAFI BAADA YA UKAGUZI WA CAG

    June 17, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MAAFISA WATENDAJI WA HALMASHAURI BAADA YA KIKAO KAZI

    June 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.