• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Nimeridhika na kazi inayofanyika kwenye Miradi ya Maji inayoendelea - DC-Mfune

Tarehe ya Kuanza: May 7th, 2021

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune siku ya tarehe 05/05/2021 alipofanya ziara ya kutembelea miradi ya Maji ya Luduga-Mawindi utakaonufaisha vijiji vitano vya kata za Ipwani na Mawindi pamoja na Mradi wa Maji wa Ilongo uliopo kata ya Mahongole utakaovinufaisha vijiji 3.

Akiwa katika ziara hiyo ambayo aliambatana na Kamati ya Usalama pamoja na wataamu mbalimbali kutoka Ofisi ya RUWASA Mbarali Mhe. Mfune alifurahishwa na utekelezaji wa agizo la Naibu Waziri wa Maji Mhe. Eng. Maryprisca Mahundi alipotembelea Wilaya ya Mbarali.

“Kama mnavyojua Serikali ilileta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji, na Naibu waziri wa Maji alishatembelea na alitoa maelekezo. Nimefurahi utekelezaji hadi sasa ni mzuri  na nimeambiwa kuwa wiki hii wanafanya majaribio na wiki ijayo maji yataanza kutoka Kijiji cha Kangaga kilichopo kata ya mawindi.”

“Na kuhusiana na mradi wa Ilongo kwa sasa upo katika hatua nzuri kwani vitu vingi vya muhimu vimeshakamilika kilichobaki kwa sasa ni kusambaza miundombinu kutoka kwenye tank kwenda kwa wananchi na tunaendelea kuwasiliana na Wizara ili fedha zilizobaki ziweze kuletwa kumalizia mradi huu” alisema Mhe. Mfune

Meneja wa Maji RUWASA Wilaya ya Mbarali Eng. Samweli Heche alisema kuwa  mradi wa Maji Luduga-Mawindi hadi sasawamekamilisha uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba kuu umbali wa km 6, pamoja na bomba la usambazaji maji kijiji cha Kangaga umbali wa km 11.5, ujenzi wa tanki la maji la ujazo wa Lita 150,000, Ujenzi wa Tanki la kupunguza mgandamizo (BPT) pamoja na Ujenzi wa Vituo vya kuchotea maji 12.

Eng. Heche aliongeza kuwa kwa upande wa Mradi wa maji wa ilongo kazi zilizofanyika ni Uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa bomba km 8, Ujenzi wa Tanki la kuhifadhia maji lenye ujazo wa lita 150,000 na Ujenzi wa Chumba cha Mitambo (Pumphouse), Ujenzi wa njia ya umeme mkubwa pamoja na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji.

Mradi wa Maji Luduga-Mawindi unatarajia kuvinufaisha vijiji 5 vya kata za Mawindi na Ipwani ambavyo ni kijiji cha Kangaga, Mkandami, Ipwani, Matemela, Itipingi na Manienga na Mradi wa Maji Ilongo utavinufaisha vijiji 3 vya kata ya Mahongole ambavyo ni Ilaji na Igalako ambavyo vyote vipo kata ya Mahongole.

Mradi wa Maji wa Luduga-Mawindi hadi kukamilika kwake unatarajia kugharimu kiasi cha Tsh. Billion 9,666,262,149 kwa awamu 5 za ukamilishaji wake na hadi sasa mradi huo upo katika awamu ya 3. Mradi wa maji Ilongo unatarajia kughalimu kiasi cha shilingi million 846,788,006 hadi kukamilika kwake.

 

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • KIKAO CHA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI NA WATUMISHI WOTE WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

    June 16, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI YAPATA HATI SAFI BAADA YA UKAGUZI WA CAG

    June 17, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MAAFISA WATENDAJI WA HALMASHAURI BAADA YA KIKAO KAZI

    June 16, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.