• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TANGAZO KWA UMMA

Posted on: July 1st, 2018

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI INAWATANGAZIA WADAU WA KILIMO NA WANANCHI WOTE KUWA, SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUPITIA SHIRIKA LAKE LA MAENDELEO (NDC), KUNA UUZWAJI NA UKOPESHWAJI WA MATREKTA AINA YA URSUS PAMOJA NA ZANA ZA KILIMO KWA BEI RAHISI NA MASHARTI NAFUU.

UTARATIBU WA KUPATA MATREKA HAYO NI KAMA IFUATAVYO:

Katika kuuza matrekta ya aina ya URSUS na zana zake, Shirika linatumia mifumo miwili yaani mfumo wa fedha taslim na mfumo wa mkopo.

1. MAUZO KWA FEDHA TASLIMU

Mteja atahitaji kulipia kwenye akaunti ya Shirika baada ya kuwasilisha mahitaji yake rasmi na kupewa Invoice ya NDC. Mteja atatakiwa kukabidhi kumbukumbu zake NDC kwa ajili ya usajili wa trekta. Kama sehemu ya huduma kwa mteja, Shirika litamkabidhi mteja trekta likiwa limeshasajiliwa.

2. MAUZO KWA MIKOPO KUPITIA TAASISI ZA FEDHA

I.) BENKI YA MAENDELEO YA KILIMO (TADB)

Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) limeingia mkataba na Benki ya Maendeleo ya Kilimo ya Tanzania (Tanzania Agricultural Development Bank (TADB) ili iweze kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa mkulima/kikundi. Mteja atachukua Proforma Invoice kutoka NDC na kuwasilisha kwenye TADB. Mteja akikidhi vigezo vya mkopo, utaratibu utafanyika ili kuijulisha NDC kwa bidhaa zitakazokuwa zimeidhinishwa na Benki hii. Baada ya Benki hii kuingiza fedha katika akaunti ya NDC, utaratibu wa kumkabidhi mteja husika bidhaa alizolipia utafanyika.

II.) MFUKO WA PEMBEJEO WA TAIFA (AGITF)

Utaratibu wa mikopo utafanyika vilevile kwa kupitia Mfuko wa Pembejeo wa Taifa (Agriculture Inputs Trust Fund (AGITF) ) ili uweze kutoa mkopo wenye masharti nafuu kwa mkulima/kikundi. Mteja atachukua Proforma Invoice kutoka NDC na kuwasilisha kwenye mfuko wa Pembejeo. Mteja akikidhi vigezo vya mkopo, utaratibu utafanyika ili kuijulisha NDC kwa bidhaa zitakazokuwa zimeidhinishwa na Mfuko huo. Baada ya Mfuko huo kuingiza fedha katika akaunti ya NDC, utaratibu wa kumkabidhi mteja husika bidhaa alizolipia utafanyika.

Shirika linaendelea kuzungumza na Taasisi mbalimbali za fedha ili ziweze kushiriki kutoa mikopo yenye masharti nafuu.

3. MAUZO KWA MIKOPO KUPITIA KWA WAAJIRI

I) KUPITIA OFISI YA BUNGE

Utaratibu unakamilishwa kuwawezesha Waheshimiwa Wabunge na wafanayakzi katika Ofisi ya Bunge waweze kununua matrekta haya kama mchango wao katika kuleta mapinduzi ya kilimo nchini. Shirika litawakopesha Waheshimiwa Wabunge na Wafanyakazi wa ofisi ya Bunge kwa utaratibu maalum baada ya kutoa malipo ya awali (down payment) siyo chini ya asilimia 40 na kiasi kilichobaki watakopeshwa. Ofisi ya bunge itadhamini mkopo huu kwa Waheshimiwa Wabunge na Wafanyakazi wa ofisi hiyo. Aidha, dhamana ya mkopo itakuwa ni mshahara na mafao ya mteja husika.

II) KUPITIA WAFANYAKAZI WA SERIKALI

Shirika, kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, linakamilisha utaratibu wa kuwawezesha Makatibu Wakuu wa Wizara husika kuwadhamini wafanyakazi wao wanunue matrekta ya aina ya URSUS na zana zake kwa njia ya mkopo. Wafanyakazi wa Serikali watatakiwa kulipa malipo ya awali (down payment) ya siyo chini ya asilimia 40 na kiasi kilichobaki watakopeshwa.

III) KUPITIA HALMASHAURI ZA MANISPAA/WILAYA

Takriban Halmashauri 16 zimewasilisha maombi yao ya kutaka kununua matrekta ya aina ya URSUS kwa njia ya mkopo. Baada ya kupata mahitaji ya matrekta ya wakulima wake, Halmashauri itakusanya fedha na kulipa katika akaunti ya NDC ambapo NDC itatoa matrekta kulingana na fedha iliyokusanywa. Halmashauri inaweza kununua matrekta haya kwa kupitia benki tajwa hapo juu au kutoa malipo ya awali (down payment) yasiyopungua asilimia 40 na kiasi kinachobakia kitakuwa mkopo wenye masharti nafuu, ikiwemo riba, muda wa kulipa deni na awamu za ulipaji (installments). Ofisi ya Rais – TAMISEMI ndiyo itakuwa mdhamini wa Halmashauri ambazo zitahusika katika mpango huu.

IV) KUPITIA TAASISI ZA UMMA

Taasisi za Umma zitaweza kinunua matrekta pamoja na zana zake kwa mkopo ama kwa kupitia Benki iliyotajwa hapo juu au kwa kuwasiliana na NDC ili kuangalia namna bora ya kununua matrekta haya.

 

KWA MAELEZO ZAIDI

Mteja anaweza kuwasiliana na nasi kwa anuani ifuatayo:

Mkurugenzi Mwendeshaji,

Shirika la Taifa la Maendeleo,

Jengo la Development House,

Mtaa wa Kivukoni Front/Ohio

S. L. P. 2669,

DAR ES SALAAM

Simu: +255 22 2112893, 2111494, 2111460

Barua Pepe: md@ndc.go.tz

AU

Fika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Ofisi ya Idara ya Kilimo Umwagiliaji na Ushirika


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI YA MKATABA YA MTUNZA KUMBUKUMBU (DATA ENTRY CLERK) NA TABIBU (CLINICAL OFFICER II) TAREHE 02-12-2022 November 28, 2022
  • RE-ADVATISEMENT JOB VACANCIES November 10, 2022
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI KATIKA KATA YA UBARUKU

    March 03, 2023
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI KANALI DENIS MWILA AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA UPANDAJI WA MITI WILAYA YA MBARALI TAREHE 18/02/2023

    February 24, 2023
  • TIMU YA CMT MBARALI NA MENEJA WA MAJI WILAYA YA MBARALI WAKIKAGUA MRADI WA MAJI

    May 15, 2022
  • AFISA UTUMISHI NA UTAWALA

    June 09, 2022
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.