• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Historia



  1. Uanzishaji wa Wilaya

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ni mojawapo ya Halmashauri zinazounda Mkoa wa

Mbeya. Halmashauri hii ilianzishwa tarehe 7 Julai 2000 kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za

Mitaa (Mamlaka za Wilaya) ya mwaka 1982 kupitia vifungu Na. 8 na 9. Cheti rasmi cha

uanzishaji kilisainiwa tarehe 5 Juni 2003. Kabla ya kuanzishwa, maeneo ya Mbarali yalikuwa

chini ya usimamizi wa Halmashauri jirani, na uanzishaji wake ulilenga kusogeza karibu

huduma kwa wananchi na kusimamia kwa ufanisi zaidi shughuli za maendeleo.


  1. Eneo na Jiografia

Wilaya ya Mbarali ina ukubwa wa takribani kilomita za mraba 16,000. Kwa upande wa

mipaka, inapakana na Wilaya ya Iringa Vijijini upande wa Kaskazini Mashariki, Wilaya ya

Njombe upande wa Mashariki, Wilaya ya Mbeya Vijijini upande wa Kusini, na Wilaya ya

Chunya upande wa Kaskazini. Mandhari yake inaundwa na tambarare za Bonde la Usangu,

vilima na maeneo ya misitu, na wilaya hii hugawanyika katika kanda tatu kuu: uwanda wa

juu wenye mvua nyingi, uwanda wa kati unaochanganya kilimo na ufugaji, na tambarare za

kusini ambazo kilimo chake hutegemea zaidi umwagiliaji


  1. Watu na Makabila

Wilaya ya Mbarali inakaliwa na makabila mbalimbali, makubwa yakiwa Wasangu, Wahehe,

Wabena, Wanyakyusa na Wakinga. Aidha, kuna makabila mengine wahamiaji kama

Wasukuma, Wanji, na Wagogo ambao wamehamia katika Bonde la Usangu kwa ajili ya

shughuli za kilimo na ufugaji. Mchanganyiko huu wa makabila umechangia katika utajiri wa

tamaduni na ujenzi wa mshikamano wa kijamii katika wilaya.


  1. Uchumi na Shughuli Kuu

Shughuli kuu ya kiuchumi katika Wilaya ya Mbarali ni kilimo, ambapo takribani asilimia 80

ya wananchi wanajihusisha moja kwa moja na shughuli hii. Mazao makuu ya chakula ni

pamoja na mpunga, mahindi, mihogo, na viazi, huku mazao ya biashara yakiwa ni alizeti,

pamba, karanga na bustani. Wilaya hii ni maarufu kitaifa kwa kilimo cha mpunga kupitia

skimu za umwagiliaji, ambapo kuna zaidi ya skimu 80 zinazochangia pakubwa uzalishaji wa

zao hilo. Uwepo wa miundombinu ya barabara kuu ya TANZAM na reli ya TAZARA

kumeongeza fursa ya biashara na usafirishaji wa mazao.


  1. Miundombinu na Huduma za Jamii

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imegawanyika katika tarafa, kata, vijiji na vitongoji

vinavyosimamiwa na serikali za mitaa. Huduma za jamii zinatolewa kupitia shule, vituo vya

afya, zahanati na vituo vya maji vilivyopo katika maeneo mbalimbali. Hata hivyo,

changamoto bado zipo ikiwemo upungufu wa watumishi wa serikali katika sekta muhimu,

uhitaji wa barabara za vijijini zinazopitika muda wote, na uhaba wa huduma za maji safi na

salama katika baadhi ya maeneo.


  1. Changamoto na Fursa

Changamoto kubwa zinazolikabili eneo hili ni pamoja na mabadiliko ya tabianchi

yanayoathiri upatikanaji wa mvua, ukosefu wa masoko ya uhakika kwa mazao, na upungufu

wa pembejeo bora za kilimo. Pamoja na changamoto hizo, Wilaya ya Mbarali ina fursa

kubwa za maendeleo kupitia kilimo cha umwagiliaji, uwepo wa ardhi yenye rutuba, na

vivutio vya utalii vinavyopatikana katika maeneo yanayopakana na Hifadhi ya Taifa ya

Ruaha.


  1. RAMANI YA WILAYA YA MBARALI





  1. Matokea ya Sensa ya Watu na Makazi 2022

Kulingana na sensa ya mwaka 2022, idadi ya watu wa Halmashauri / Wilaya ya Mbarali ni

446,336. “Number and Percentage Distribution of Population by Sex of Mbarali District

(446,336 persons) whereby 217,280 are male (48.7%) and 229,056 are female (51.3%)”.


Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • MBARALI YAKABIDHI MWENGE WA UHURU KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBEYA, YAPONGEZWA KWA USIMAMIZI WA MIRADI

    October 09, 2025
  • MWENGE WA UHURU WILAYANI MBARALI

    October 08, 2025
  • WANANCHI WA MBARALI WAFURIKA KUKESHA KWENYE MWENGE WA UHURU UBARUKU

    October 08, 2025
  • DC MBARALI APOKEA MWENGE WA UHURU

    October 08, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD
  • EPISOD002- ELIMU KWA WANANCHI JUU YA MATUMIZI YA MFUMO WA TAUSI PORTAL
  • MKURUGENZI MWELI AAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA WATENDAJI WALIOSITAFU
  • MKURUGENZI MWELI AAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA WATENDAJI WALIOSITAFU

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.