• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kata ya Itamboleo

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA ITAMBOLEO



MHE. 

DIWANI WA KATA 



TAARIFA YA KATA YA ITAMBOLEO


1. UTANGULIZI

Kata ya Itamboleo ipo Wilaya ya Mbarali Tarafa ya Ilongo, upande wa Magharibi, umbali wa kilometa 63 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na ina jumla ya ukubwa wa hekari 28,137.563. Kata Itamboleo ilianzishwa kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa mwaka 2010 

Kata hii imepakana na kata za Igurusi na Utengule Usangu upande wa Magharibi, Chimala upande wa Mashariki, Luhanga upande wa kaskazini,  Ihahi na Mapogolo.

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vijiji kuna Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Maafisa watendaji wa Vijiji. 

Kata ya Itamboleo ina jumla ya watumishi 46 wa kada mbalimbali kama ifuatavyo: Utawala 5, Elimu watumishi 34, Afya watumishi 2, Maliasili watumishi 0, Kilimo watumishi 3, Mifugo watumishi 2 na Maendeleo ya jamii watumishi 0.

Kata ya Itamboleo ina Jumla ya Vijiji 4 ambavyo ni Kijiji cha Kapunga, Kijiji cha Itamboleo, Kijiji cha Mbalino na Kijiji cha Matebete. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo 24 

Kata ya Itamboleo ina jumla ya wakazi wapatao 9,698 kati yao Wanaume 4,735 na Wanawake 4,963. Makabila yanayopatikana katika kata ya Itamboleo ni wasangu, wabena, wawanji, wanyakyusa, wakinga, wasukuma, masai, wahehe n.k

Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata shughuli za kiuchumi kwa wananchi wake kama ifuatavyo; kilimo cha mpunga wa biashara, ufugaji wa ng’ombe na mbuzi, ufugaji wa mabwawa ya samaki na kilimo cha mbogamboga katika kijiji cha Itamboleo, 

Vyanzo vya Mapato katika kata hii inatofautiana kutokana na Kijiji kimoja hadi kingine, miongoni mwa vyanzo hivyo ni kama; faini/adhabu mbalimbali, pawatila za Vijiji, michango ya wananchi, ushuru mdogomdogo, mauziano ofisi, mauzo ya kuni kavu, uuzaji wa mawe na Mchanga, Ruzuku kutoka Serikali kuu (Halmashauri ya Wilaya) pamoja na misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali.

Vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kata ni pamoja na Misitu ya asili, madhari nzuri ya safu ya milima ya Itamboleo na chemichemi ya maji ya magadi ya chumvi yaliyopo kijiji cha Matebete ndani ya rachi. 

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha kila Kijiji kina Kamati ya Ulinzi na Usalama ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana vilevile kuna Vituo vya police kata za jirani, Igurusi na Chimala ambapo sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

 A. ELIMU

Kata ya Itamboleo ina Jumla walimu 34, shule za Msingi tano (5). 

 i. ELIMU MSINGI

  • Shule ya Msingi Itamboleo
  • Shule ya Msingi Mbalino
  • Shule ya Msingi Matebete
  • Shule ya Msingi Kapunga
  • Shule ya Msingi Kapunga B.

 ii. ELIMU SEKONDARI

 Kuna ujenzi wa shule mbili za sekondali unaendelea, shule ya sekondali Kapunga na Itamboleo 


B. AFYA

Kata ya Itamboleo ina  watumishi wa idara ya afya ni wawili (2), zahanati 1 kijiji cha Itamboleo kati ya vijiji vinnevilivyopo, lakini kuna kituo cha afya 1katika kijiji cha kapunga ambacho kinachoendelea kutengenezwa kwa msaada wa mwekezaji wa kapunga rice project LTD.  magonjwa yanayosumbua mara kwa mara ni ; Diarrhea, Intestinal worms, Magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa. Eg coughing na UTI


C. KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA

Kata ya Itamboleo ina jumla ya watumishi 3 idara ya kilimo na ushirika, na ina jumla ya wakulima 770,  wanawake 220 wanaume 550. Eneo linalofaa kwa kilimo ni (heka) 17,780, lakini eneo linalolimwa ni heka 9440.Mazao yanayopatikana  katika kata ya ni  – mpunga, mahindi, karanga, maharage, mihogo, n.k

idadi ya skimu za  umwagiliaji zilizopo ni kapunga small holder( inamiundombinu) na mpunga mmoja ( haina miundombinu) skimu nyingine ndogo ndogo ambazo hazijasajiliwa ni Mapula, Lwanjiri, Lambitari, Magagani, na Chimbachimba.

Pia kata ya Itamboleo inakampuni moja binafsi la kapunga rice project linalojishughulisha na kilimo cha mpunga lenye ukubwa wa hekta 5,500. 

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ;

  • Huduma za ugani
  • Mashamba darasa juu ya Kilimo cha Kisasa
  • Hifadhi bora ya Mazao ya Chakula
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Kutatua Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao
  • Kukusanya takweimu za Mvua
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji ya kila robo mwaka na kuwasilisha wilayani.
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Kilimo katika Kamati ya Maendeleo ya kata.

D. MIFUGO NA UVUVI

Kata ya Itamboleo ina jumla  ya watumishi 2 wa idara ya mifugo na Uvuvi, pia kuna ranch ya umoja wa wafugaji matebete madunguru nyenye ukubwa wa hekta 12,000na ina jumla ya mifugo kama ifuatavyo:

  • Ng’ombe                     11,139,
  • Ndama                        2800
  • Kondoo                       602,
  • Mbuzi                          2445,
  • Punda                          268,
  • Nguruwe                     109,
  • Paka                            121,
  • Mbwa                          395, Na
  • Kuku                           2395.

Magonjwa  yanayosumbua mifugo mara kwa mara ni kama  homa ya mapafu, foot and mouth diseases, anthrax, 

Huduma zinazotolewa na Idara ni pamoja na;

  • Tiba kwa magonjwa dhidi ya Mifugo
  • Huduma mbalimbali za Mifugo kama kuhasi, kukata pembe, kwato na midomo, kupiga chapa Mifugo, kukata meno, kuzalisha, kuogesha na Ukaguzi wa nyama
  • Ushauri juu ya ujenzi bora wa mabanda ya Mifugo
  • Kutoa elimu ya ufugaji bora wa namna ya ufugaji wa Mifugo yenye tija
  • Ukaguzi wa Nyama na usafi katika Machinjio
  • Kusimamia zoezi Endelevu la upigaji chapa wa mifugo 

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata hii. Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.


E. MALIASILI

Kata ya Itamboleo haina watumishi wa maliasili mpaka sasa, na kata ya Itamboleo ina uhifadhi wa misitu katika kijiji cha Itamboleo ina uhifadhi mazingira na misitu kwa kusimamiwa na kamati za mazingira za vijiji.

  i.Vivutio vya Utalii

  • Misitu ya asili,
  • madhari nzuri ya safu ya milima ya Itamboleo na
  • chemichemi ya maji ya magadi ya chumvi yaliyopo kijiji cha Matebete ndani ya rachi.

 ii. Hifadhi ya Misitu

Kata ya Itamboleo inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzai wa hifadhi kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) katika Vijiji vilivyopakana na hifadhi hizo, kupanda miti, kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kuchoma mkaa na kukata miti hovyo bila ya kuipanda upya, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.


 ii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo. 

Kata inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya misituasili na vyanzo vya maji kwa matumizi Endelevu, kuendelea kushauri kutengwa kwa Bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika Vijiji

F. MAENDELEO YA JAMII

Kata ya Itamboleo haina watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii mpaka sasa, huduma zinazotolewa na kata ni  kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini.




Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI YA MKATABA YA MTUNZA KUMBUKUMBU (DATA ENTRY CLERK) NA TABIBU (CLINICAL OFFICER II) TAREHE 02-12-2022 November 28, 2022
  • RE-ADVATISEMENT JOB VACANCIES November 10, 2022
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI KATIKA KATA YA UBARUKU

    March 03, 2023
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI KANALI DENIS MWILA AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA UPANDAJI WA MITI WILAYA YA MBARALI TAREHE 18/02/2023

    February 24, 2023
  • TIMU YA CMT MBARALI NA MENEJA WA MAJI WILAYA YA MBARALI WAKIKAGUA MRADI WA MAJI

    May 15, 2022
  • AFISA UTUMISHI NA UTAWALA

    June 09, 2022
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.