• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kata ya Kongolo Mswisi

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA KONGORO MSWISWI

 

MHE. 

DIWANI WA KATA


TAARIFA YA KATA

1. UTANGULIZI

Kata ya Kongoro Mswisi ipo Wilaya ya Mbarali tarafa ya Ilongo upande wa Kusini Mgharibi umbali wa kilometa 80 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na ina ukubwa wa hekta 4,663.379, Kata hii ipepakana na kata za Utengule Usangu upande wa Kaskazini, Igurusi upande wa Mashariki, Mahongole upande wa Magharibi na upande wa Kusini imepakana na pamoja na Halmahsauri ya Wilaya ya Mbeya

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vijiji kuna Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Maafisa watendaji wa Vijiji.

Kata hii ina Jumla ya watumishi 104 ambao ni; Mtendaji wa Kata 1, Watendaji wa Vijiji 5, Walimu 91, Kilimo na ushirika 5, Mifugo na Uvuvi 1, pamoja na Maendeleo ya jamii 1.

Kata ya Kongoro Mswisi ina Jumla ya Vijiji 5 ambavyo ni Kijiji cha Kongoro Mswisi, Kijiji cha Mambi, Kijiji cha Azimio Mapula, Kijiji cha Azimio Mswisi, pamoja na Kijiji cha Kongolo Mkola. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo 26.

Kata ina Jumla ya wakazi wapatao 7,448 kati yao wanaume 3,244 na Wanawake 4,204. Makabila yanayopatikana katika kata ya Igurusi ni pamoja na Kabila la Wasangu, Wanyakyusa, Wabena, Wasafwa, Wasukuma na Wandali.

Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata hii ni pamoja na Kilimo, ufuga pamoja na Ujasiliamali.

Vyanzo vya Mapato katika kata hii inatofautiana kutokana na Kijiji kimoja hadi kingine, miongoni mwa vyanzo hivyo ni kama; faini/adhabu mbalimbali, pawatila za Vijiji, Ruzuku kutoka Serikali kuu (Halmashauri ya Wilaya) pamoja na misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali.

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha kuna kituo cha Polisi ndani ndani ya shirika la TAZARA na Kituo cha Polisi kata ya jirani ya igurusi ambavyo sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.


2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

  A. ELIMU

Kata ya Kongoro Mswisi ina Jumla ya shule za Msingi s5 pamoja na shule ya sekondari moja shule hizo ni kama ifuatavyo;

     i. Elimu msingi

  • Shule ya Msingi Mswisi
  • Shule ya Msingi Mkola
  • Shule ya Msingi Azimio Mswisi
  • Shule ya Msingi Azimio Mapula
  • Shule ya Msingi Mambi

    ii. Elimu ya sekondari

  • Shule ya Sekondari Jakaya

   B. AFYA 

Kata ya Kongoro Mswisi ina Zahanati  ambayo ipo chini ya Shirika la TAZARA pamoja na zahanati iliyopo katika Kata ya Jirani ya Igurusi. Homa zinazosumbua katika kata hii ni pamoja na homa ya matumbo na VVU.

    C. KILIMO NA USHIRIKA

Idadi ya watumishi katika Idara ya Kilimo ndani ya kata ni watumishi 5. Kata hii ina wakulima wapatao 1,400 na wanalima kwenye eneo lipatalo ukubwa wa hekta 3,690. Kata na Jumla ya skumu 4 za umwagiliaji ambazo ni skimu ya Kongolo Mswisi, Skimu ya Chang’ombe, Skimu ya Mashala, na Skimu ya Azimio Mswisi.  Mazao yanayopatikana ndani ya kata ni pamoja na zao la Mpunga, zao la Mahindi, zao la Mihogo, Alizeti, Viazi, Vitunguu, pilipili hoho, nyanya, tangawizi, karanga, tikiti maji pamoja na mboga za aina mbalimbali.

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ;

  • Huduma za ugani
  • Mashamba darasa juu ya Kilimo cha Kisasa
  • Hifadhi bora ya Mazao ya Chakula
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi  ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao
  • Kutatua changamoto na Kero mbalimbali za wakulima
  • Kuwatambua wakulima na shughuli zao
  • Kuweka takwimu sahihi za uzalishaji
  • Kusimamia skimu za umwagiliaji

  

  D. MIFUGO NA UVUVI

Idadi ya watumishi katika Idara hii ni 1 na idadi ya Mifugo iliyopo ndani ya kata ni kama ifuatavyo;

  • Ng’ombe                     3,549
  • Kondoo                       278
  • Mbuzi                          828
  • Mbwa                          171
  • Punda                          107
  • Kuku                           2,714
  • Nguruwe                     209
  • Paka                            64

Huduma zinazotolewa na Idara ni pamoja na;

  • Tiba kwa magonjwa dhidi ya Mifugo
  • Huduma mbalimbali za Mifugo kama kuhasi, kukata pembe, kwato na midomo, kupiga chapa Mifugo, kukata meno, kuzalisha, kuogesha na Ukaguzi wa nyama
  • Ushauri juu ya ujenzi bora wa mabanda ya Mifugo
  • Kutoa elimu ya ufugaji bora wa namna ya ufugaji wa Mifugo yenye tija
  • Kusimamia ujenzi wa machinjia na ukaguzi wa Nyama na usafi katika Machinjio
  • Kusimamia zoezi Endelevu la upigaji chapa wa mifugo

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata hii. Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.

   

    E. MALIASILI 

        i. Hifadhi ya Misitu

kata ya Kongoro Mswisi inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzai wa hifadhi kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) katika Vijiji vilivyopakana na hifadhi hizo, kupanda miti, kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kuchoma mkaa na kukata miti hovyo bila ya kuipanda upya, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.

       ii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo.

Idara inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya misituasili na vyanzo vya maji kwa matumizi Endelevu, kuendelea kushauri kutengwa kwa bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika vijiji.

   

    F.MAENDELEO YA JAMII

Idara hii ina mtumishi mmoja, na kazi zinazofanya na ni kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI YA MKATABA YA MTUNZA KUMBUKUMBU (DATA ENTRY CLERK) NA TABIBU (CLINICAL OFFICER II) TAREHE 02-12-2022 November 28, 2022
  • RE-ADVATISEMENT JOB VACANCIES November 10, 2022
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI KATIKA KATA YA UBARUKU

    March 03, 2023
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI KANALI DENIS MWILA AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA UPANDAJI WA MITI WILAYA YA MBARALI TAREHE 18/02/2023

    February 24, 2023
  • TIMU YA CMT MBARALI NA MENEJA WA MAJI WILAYA YA MBARALI WAKIKAGUA MRADI WA MAJI

    May 15, 2022
  • AFISA UTUMISHI NA UTAWALA

    June 09, 2022
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.