• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kata ya Mahongole

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA MAHONGOLE


MHE. 

DIWANI WA KATA

Namba ya Simu ya Mkononi 

TAARIFA YA KATA YA MAHONGOLE

1. UTANGULIZI

Kata ya Mahongole ipo Wilaya ya Mbarali tarafa ya Ilongo umbali wa kilometa 83 kutoka makao makuu ya Wilaya ya Mbarali. Kata hii ipepakana na kata za Ruiwa, Kongolo Mswisi pamoja na Halmahsauri ya Wilaya ya Mbeya. 

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vijiji kuna Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Maafisa watendaji wa Vijiji.

Kata hii ina Jumla ya watumishi 108 ambao ni; Mtendaji wa Kata 1,Watendaji wa Vijiji 6, Elimu 84, Afya 9, Kilimo, Umwagiliaji na ushirika 5, Mifugo na Uvuvi 1, maliasili 1 pamoja na Maendeleo ya jamii 1. 

Kata ya Mahongole ina Jumla ya Vijiji 6 ambavyo ni Kijiji cha Ilongo, Kijiji cha Igalako, Kijiji cha Ilaji, Kijiji cha Nsonyanga, Kijiji cha Mahongole pamoja na Kijiji cha Kapyo. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo 31

Kata ya Mahongole ina Jumla ya wakazi wapatao 10,348 kati yao wanaume 4,980 na Wanawake 5,368. Makabila yanayopatikana katika kata ya Mahongole ni pamoja na Kabila la Wasangu, Wasafwa, Wasukuma, Wahehe, Wanyakyusa, Wabena, na Wawanji, shughuli kubwa za kiuchumi katika kata hii ni pamoja na Kilimo, ufugaji na Biashara. 

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha kila Kijiji kina Kamati ya Ulinzi na Usalama, sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.


2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

    A. ELIMU

Kata ya Mahongole ina Jumla ya walimu 84, shule za Msingi Tano (5) pamoja na shule ya sekondari moja shule hizo ni kama ifuatavyo; 

       i. Elimu msingi

  • Shule ya Msingi Ilongo
  • Shule ya Msingi Igalako
  • Shule ya Msingi Mkoji
  • Shule ya Msingi Kapyo na
  • Shule ya Msingi Nsonyanga

     ii. Elimu ya sekondari

  • Shule ya Sekondari Ruiwa

  B. AFYA 

Kata ya Mahongole ina Jumla ya Zahanati tatu (3) pamoja na watumishi tisa (9) ambapo kila zahanati kuna watumishi watatu (3). Zahanati hizo zinapatikana ndani ya Vijiji vya Ilongo, Kapyo na Mahongole. Magonjwa yanayosumbua katika kata ya Mahongole ni pamoja na Nimonia, Kuhara, Urti, Sti, Njia ya Hewa,Utapiamlo, kichochi na Malaria.

 

C. KILIMO NA USHIRIKA 

Idadi ya watumishi katika Idara ya Kilimo ndani ya kata ni watumishi watano (5). Kata hii ina wakulima wapatao 1,787 kupitia skim za umwagiliaji nne (4) ambazo ni skimu ya Ipatagwa, Motombaya, Azimio Mswisi na Nyasa Kapyo. Mazao yanayopatikana ndani ya kata ni pamoja na zao la Mpunga, zao la Mahindi, zao la mihogo, na aina mbalimbali za mbogamboga.

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ; 

  • Huduma za ugani
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi  ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao

  D. MIFUGO NA UVUVI

Idadi ya watumishi katika Idara hii ni mmoja (1) na idadi ya Mifugo iliyopo ndani ya kata ni kama ifuatavyo;

  • Ng’ombe                     4,454
  • Kondoo                       392
  • Mbuzi                          1,449
  • Punda                          68
  • Bata                             471
  • Kuku                           1,011
  • Nguruwe                     501
  • Paka                            113

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata ya Mahongole. Hali ya Uvuvi katika mwaka 2016/2017 haikuwa nzuri kutokana na kuto kuwa na mvua ya kutosha kitu kilischosababisha kupungua kwa uzaliano wa samaki.

Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.

 

  E. MALIASILI 

Idara ina mtumishi mmoja ambaye anahudumia kata 3 ambazo ni kata ya Mahongole, Mwatenga na Ruiwa. Kata ina

  i. Vivutio vingi vya utalii kama ifuatavyo;

  • Mapango ya watu wa kale
  • Bwawa lenye samaki wasioiva
  • Jiwe la maajabu ukiligonga linalia kama kengele
  • Nyumba ya matambiko ya kabila la wasangu ambayo imezungukwa na msitu mnene wa miti ya asili

  ii. Hifadhi ya Misitu

kata ya Mahongole imepakana na hifadhi ya Serikali kuu mbili ambazo ni Mwambalizi na Ilembo Usafwa. Idara hii inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzai wa hifadhi kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) katika Vijiji vilivyopakana na hifadhi hizo, pia kwa kushirikiana na TFS zimewekwa alama za mipaka (Mabango na Biacon) kwa ajili ya kuwatambulisha wanaotaka kuvuka mipaka hiyo. Idara inaendelea kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.

Vilevile kuna shughuli za ufugaji nyuki ndani ya kata, na kuna vikundi vitatu vya ufugaji vya watu binafsi.

  iii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo.

Idara inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya misituasili na vyanzo vya maji kwa matumizi Endelevu, kuendelea kushauri kutengwa kwa Bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika Vijiji na kuendelea kuhamasisha ufugaji bora wa nyuki kwa ajili ya kuongeza vipato, pia kuwashirikisha wananchi katika kulinda wanyamapori ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa punde wanyama waharibifu wanapohatarisha maisha ya watu ili kuweza kuwadhibiti.

   F. MAENDELEO YA JAMII

Idara hii ina mtumishi mmoja, na kazi zinazofanya na ni kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI YA MKATABA YA MTUNZA KUMBUKUMBU (DATA ENTRY CLERK) NA TABIBU (CLINICAL OFFICER II) TAREHE 02-12-2022 November 28, 2022
  • RE-ADVATISEMENT JOB VACANCIES November 10, 2022
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI KATIKA KATA YA UBARUKU

    March 03, 2023
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI KANALI DENIS MWILA AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA UPANDAJI WA MITI WILAYA YA MBARALI TAREHE 18/02/2023

    February 24, 2023
  • TIMU YA CMT MBARALI NA MENEJA WA MAJI WILAYA YA MBARALI WAKIKAGUA MRADI WA MAJI

    May 15, 2022
  • AFISA UTUMISHI NA UTAWALA

    June 09, 2022
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.