• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kata ya Mapogoro

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA MAPOGORO

 

Mhe. NAFTARI PAULO KITHA

DIWANI WA KATA

Namba ya Simu ya Mkononi 


TAARIFA YA KATA YA MAPOGORO

  

1. UTANGULIZI

Kata ya Mapogoro ipo Wilaya ya Mbarali Tarafa ya Rujewa, upande wa Magharibi, umbali wa kilometa 15 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali. 



Kata hii imepakana na kata ya Lugelele upande wa Mashariki, Kata ya Luhanga upande wa Kaskazini Magharibi, kata za Ubaruku na Imalilo Songwe upande wa kaskazini, kata ya Itamboleo upande wa Kaskazini Magharibi. Vilevile kata hii imepakana na Hifadhi ya Mpanga Kipengele upande wa Kusini pamoja na Wiaya ya Makete upande wa Kusini Maghaaribi 

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vijiji kuna Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Maafisa watendaji wa Vijiji. 

Kata ya Mapogoro ina jumla ya watumishi 174 wa kada mbalimbali kama ifuatavyo: Utawala 10, Elimu watumishi 125, Afya watumishi 28, Maliasili watumishi 1, Kilimo watumishi 6, Mifugo watumishi 3 na Maendeleo ya jamii watumishi 1.

Kata ya Mapogoro ina Jumla ya Vijiji 9 ambavyo ni Kijiji cha Mabadaga, Kijiji cha Mbuyuni, Kijiji cha Nyanguru, Kijiji cha Itamba, Kijiji cha Msesule, Kijiji cha Mtamba, Kijiji cha Uturo, Kijiji cha Ukwama na Kijiji cha Ukwavila. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo …. 

Kata ya Mapogoro ina jumla ya wakazi wapatao 20,362 kati yao Wanaume 9,766 na Wanawake 10,596. Makabila yanayopatikana katika Kata ya Mapogoro ni Wasangu, Wabena, Wawanji, Wanyakyusa, Wasukuma, Wamasai na Wahehe.

Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata kwa wananchi ni kama, kilimo, ufugaji, Uvuvi, utalii na uchimbaji wa madini. 

Vyanzo vya Mapato katika kata hii inatofautiana kutokana na Kijiji kimoja hadi kingine, miongoni mwa vyanzo hivyo ni kama; faini/adhabu mbalimbali, pawatila za Vijiji, michango ya wananchi, ushuru mdogomdogo, Ruzuku kutoka Serikali kuu (Halmashauri ya Wilaya) pamoja na misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali. 

Vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kata ni pamoja na Misitu ya asili, Bwawa la Mdindimo katika Kijiji cha Msesule pamoja na Milima ya Hifadhi ya Mpanga Kipengele katika Vijiji vya Mabadaga, Nyanguru na Mbuyuni. 

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha kila Kijiji kina Kamati ya Ulinzi na Usalama ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana vilevile kuna Kituo vya Police Wilaya umbali wa Km 15 kutoka kata ilipo ambapo sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

 A. ELIMU

Kata ya Mapogoro ina Jumla walimu 125, shule za Msingi 8 pamoja na shule ya sekondari moja.

 i. ELIMU MSINGI

  • Shule ya Msingi Ifushilo
  • Shule ya Msingi Ukwavila
  • Shule ya Msingi Uturo
  • Shule ya Msingi Mtamba
  • Shule ya Msingi Mbuyuni
  • Shule ya Msingi Mabadaga
  • Shule ya Msingi Itamba
  • Shule ya Msingi Msesule

 ii. ELIMU SEKONDARI

Shule Sekondari Malenga

B. AFYA 

Kata ya Mapogoro ina watumishi wa idara ya afya ni 28, kituo cha afya 1, zahanati 6 katika Vijiji vya Mabadaga, Mbuyuni, Uturo, Msesule, Itamba na Ukwavila. magonjwa yanayosumbua mara kwa mara ni kuhara na UTI

C. KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA 

Kata ya Mapogoro ina jumla ya watumishi 6 wa Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, na ina jumla ya wakulima 9,138. Mazao yanayopatikana katika kata ya ni Mpunga, Mahindi, Mtama, Alizeti, Karanga, Maharage, Viazi Vitamu na Mbogamboga.

idadi ya skimu za umwagiliaji zilizopo ni Skimu ya Umwagiliaji ya Uturo, Skimu ya Umwagiliaji ya Mbuyuni, Skimu ya Umwagiliaji ya Isenyela, Skimu ya Umwagiliaji ya Msesule, Skimu ya Umwagiliaji ya Makangalawe na Skimu ya Umwagiliaji ya Ukwavila. Vilevile kuna chama cha ushirika kimoja Kijiji cha Uturo. 

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ; 

  • Huduma za ugani
  • Mashamba darasa juu ya Kilimo cha Kisasa
  • Hifadhi bora ya Mazao ya Chakula
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Kutatua Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao
  • Kukusanya takweimu za Mvua
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji ya kila robo mwaka na kuwasilisha wilayani.
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Kilimo katika Kamati ya Maendeleo ya kata.

D. MIFUGO NA UVUVI 

Kata ya Mapogoro ina jumla ya watumishi 3 wa idara ya mifugo na Uvuvi pamoja na wafugaji wapatao 921.

Idadi ya Mifugo ni kama ifuatavyo: 
  • Ng’ombe 19,209
  • Kondoo 4,713,
  • Mbuzi 9,687,
  • Punda 784,
  • Nguruwe 497,
  • Paka 559
  • Mbwa 1,108
  • Kuku 21,245

Magonjwa yanayosumbua mifugo mara kwa mara ni kama Mange,  Anaplasmosis, Babesiosis, East Coast Fever, Trypanosomiasis, Fasciolasis, CBPP, CCPP, PPR na New Castle (KIDERI)

Huduma zinazotolewa na Idara ni pamoja na; 

  • Tiba kwa magonjwa dhidi ya Mifugo
  • Huduma mbalimbali za Mifugo kama kuhasi, kukata pembe, kwato na midomo, kupiga chapa Mifugo, kukata meno, kuzalisha, kuogesha na Ukaguzi wa nyama
  • Ushauri juu ya ujenzi bora wa mabanda ya Mifugo
  • Kutoa elimu ya ufugaji bora wa namna ya ufugaji wa Mifugo yenye tija
  • Ukaguzi wa Nyama na usafi katika Machinjio
  • Kusimamia zoezi Endelevu la upigaji chapa wa mifugo

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata hii. Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.

E. MALIASILI

Kata ya Mapogoro ina mtumishi mmoja wa maliasili mpaka sasa, na Kata ya Mapogoro ina uhifadhi wa misitu wenye ukubwa wa hekali 900 katika kijiji cha Mabadaga ina uhifadhi mazingira na misitu kwa kusimamiwa na kamati za mazingira za vijiji. 

 i.Vivutio vya Utalii

  • Misitu ya asili Kijiji cha Mabadaga,
  • madhari nzuri ya  kuvutia kwenye milima iliyopo Mpakani mwa Hifadhi ya Mpanga Kipengere katika Kijiji cha Mabadaga

 ii. Hifadhi ya Misitu 

Kata ya Mapogoro inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzai wa hifadhi kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) katika Vijiji vilivyopakana na hifadhi hizo, kupanda miti, kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kuchoma mkaa na kukata miti hovyo bila ya kuipanda upya, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.

 iii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo. 

Kata inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya Misitu ya asili na vyanzo vya maji kwa matumizi Endelevu, kuanzisha bustani za miti au vitalu vya kuotesha miti, kuendelea kushauri kutengwa kwa Bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika Vijiji   

F. MAENDELEO YA JAMII

Kata ya Mapogoro ina watumishi mmoja wa Idara ya Maendeleo ya Jamii mpaka sasa, huduma zinazotolewa na kata ni kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • SALAMU ZA EID EL FITR

    March 31, 2025
  • DC MBARALI AANDAA HAFLA YA IFTALI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE,TASISI ZOTE NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU..

    March 28, 2025
  • DC MBARALI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA CHIMALA

    March 14, 2025
  • KIKAO CHA DCC KUPENDEKEZA MAJINA YA MAJIMBO WILAYANI MBARALI

    March 13, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.