• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kata ya Rujewa

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA RUJEWA

 

Mhe. MAIKO JEREMIA MAKAO

DIWANI WA KATA



Mhe. Rosemary A. Mbala

DIWANI WA VITI MAALUM

 

TAARIFA YA KATA 

1. UTANGULIZI

Kata ya Rujewa ipo Wilaya ya Mbarali Tarafa ya Rujewa, umbali wa kilometa 4 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na vilevile ipo ndani ya mamlaka ya Mji Mdogo wa Rujewa.

Kata hii imepakana na kata za Igurusi na Utengule Usangu upande wa Magharibi, Chimala upande wa Mashariki, Luhanga upande wa kaskazini, Ihahi na Mapogolo.

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vitongoji kuna Wenyeviti wa Vitongoji.

Kata ya Rujewa ina jumla ya watumishi 203 wa kada mbalimbali kama ifuatavyo: Utawala 1, Elimu watumishi 192, Afya watumishi 4, Maliasili watumishi 0, Kilimo watumishi 2, Mifugo watumishi 3 na Maendeleo ya jamii watumishi 1.

Kata ya Rujewa ina Jumla ya Mitaa 7 ambayo ni Mtaa wa Ihanga, Mtaa wa, Rujewa, Mtaa wa Ibara, Mtaa wa Isisi, Mtaa wa Uhamila, Mtaa wa Mabanda na Mtaa wa Nyeregete. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo 60.

Kata ya Rujewa ina jumla ya wakazi wapatao 34,424 kati yao Wanaume 16,633 na Wanawake 17,791. Makabila yanayopatikana katika Kata ya Rujewa ni wasangu, wabena, wahehe pamoja na makabila mengine madogomadogo.

Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata kwa wananchi wake ni pamoja na shughuli za viwandani, Kilimo, ufugaji pamoja na Biashara mbalimbali.

Vyanzo vya Mapato katika kata hii ni pamoja na faini/adhabu mbalimbali, pawatila za Mitaa, michango ya wananchi, ushuru mdogomdogo, viwanda, Ruzuku kutoka Serikali kuu (Halmashauri ya Wilaya) pamoja na misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali.

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha vyombo vyote vya ulinzi na usalama vipo kwenye kata ya Rujewa kikiwamo Kituo cha Police Wilaya ambapo sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

Taasisi za Serikari zinazopatikana katika kata ya Rujewa ni pamoja na:

  • Mamlaka ya Mji Mdogo Rujewa,
  • Mamlaka ya Maji Rujewa
  • Kituo Kikuu cha Police
  • Gereza Kuu la Mbarali
  • Hospitali ya Wilaya
  • Stand Kuu ya Rujewa
  • Ofisi za Tazara
  • Mahakama ya Mwanzo na Wilaya
  • PCCB
  • Zimamoto
  • TANESCO
  • TRA
  • TFS
  • MALIHAI
  • TAZARA
  • Posta
  • NIDA
  • Rufiji Basin
  • Ofisi ya Tarafa

Baadhi ya taasisi binafsi zinazopatikana ni pamoja na

  • Bank ya NMB
  • Bank ya CRDB
  • Zahanati ya Muslim
  • NGO’s
  • Taasisi za Mikopo
  • Taasisi za Kidini

2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

 A. ELIMU

Kata ya Rujewa ina Jumla walimu 192, shule za Msingi 9 na Sekondari 1

 i. ELIMU MSINGI

  • Shule ya Msingi Rujewa
  • Shule ya Msingi Ibara
  • Shule ya Msingi Ihanga
  • Shule ya Msingi Isisi
  • Shule ya Msingi Uhamila.
  • Shule ya Msingi Magwalisi
  • Shule ya Msingi Lyahamile
  • Shule ya Msingi Jangurutu
  • Shule ya Msingi Nyeregete

 ii. ELIMU SEKONDARI

Shule ya Sekondari Rujewa

B. AFYA

Kata ya Rujewa ina watumishi wa idara ya afya ni 3 kwenye Zahanati ya Serikali ambayo ipo moja.

Vilevile kuna Hospitali ya Wilaya pamoja na Zahanati moja ya Binafsi ambapo vyote kwa pamoja wanatoa huduma za afya kwa ujumla.

C. KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA

Kata ya Rujewa ina jumla ya watumishi 2 idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika, na ina jumla ya wakulima 6,438. Mazao yanayopatikana katika kata ya ni pamoja na Mpunga, Mahindi, Korosho, Ufuta, Alizeti, Mtama, Nugumawe, Maharagwe, Mihogo, Viazi, Matunda, mbogamboga na Mazao ya bustani.

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ;

  • Huduma za ugani
  • Mashamba darasa juu ya Kilimo cha Kisasa
  • Hifadhi bora ya Mazao ya Chakula
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Kutatua Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao
  • Kukusanya takweimu za Mvua
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji ya kila robo mwaka na kuwasilisha wilayani.
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Kilimo katika Kamati ya Maendeleo ya kata.

D. MIFUGO NA UVUVI

Kata ya Rujewa ina jumla ya watumishi 3 wa idara ya mifugo na Uvuvi, na ina jumla ya mifugo kama ifuatavyo:

  • Ng’ombe 10,935,
  • Kondoo 1,474
  • Mbuzi 4,236
  • Punda 134,
  • Nguruwe 1,198
  • Mbwa 854,

Magonjwa yanayosumbua mifugo mara kwa mara ni kama homa ya mapafu, foot and mouth diseases, anthrax, homa ya nguruwe

Huduma zinazotolewa na Idara ni pamoja na;

  • Tiba kwa magonjwa dhidi ya Mifugo
  • Huduma mbalimbali za Mifugo kama kuhasi, kukata pembe, kwato na midomo, kupiga chapa Mifugo, kukata meno, kuzalisha, kuogesha na Ukaguzi wa nyama
  • Ushauri juu ya ujenzi bora wa mabanda ya Mifugo
  • Kutoa elimu ya ufugaji bora wa namna ya ufugaji wa Mifugo yenye tija
  • Ukaguzi wa Nyama na usafi katika Machinjio
  • Kusimamia zoezi Endelevu la upigaji chapa wa mifugo

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata hii. Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.

E. MALIASILI

Kata ya Rujewa haina watumishi wa maliasili mpaka sasa,

 i. Hifadhi ya Misitu

Kata ya Rujewa inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzai wa hifadhi Misitu kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) katika maeneo yenye hifadhi hizo, kupanda miti, kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kuchoma mkaa na kukata miti hovyo bila ya kuipanda upya, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.

 ii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo. 

Kata inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya misituasili na vyanzo vya maji kwa matumizi Endelevu, kuendelea kushauri kutengwa kwa Bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika Vijiji

F. MAENDELEO YA JAMII

Kata ya Rujewa ina watumishi mmoja wa Idara ya Maendeleo ya Jamii mpaka sasa, huduma zinazotolewa na kata ni kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • SALAMU ZA EID EL FITR

    March 31, 2025
  • DC MBARALI AANDAA HAFLA YA IFTALI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE,TASISI ZOTE NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU..

    March 28, 2025
  • DC MBARALI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA CHIMALA

    March 14, 2025
  • KIKAO CHA DCC KUPENDEKEZA MAJINA YA MAJIMBO WILAYANI MBARALI

    March 13, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.