• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kata ya Ubaruku

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA UBARUKU


Mhe. Kiswaga A. Charles 

DIWANI WA KATA 

Mhe. Salome Stemile

Viti Maalumu

TAARIFA YA KATA YA UBARUKU

1. UTANGULIZI

Kata ya Ubaruku ipo Wilaya ya Mbarali Tarafa ya Rujewa, upande wa Kusini Mashariki na umbali wa kilometa 16.5 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na ina jumla ya ukubwa wa kilomita za mraba 9,826.589. Kata ya Ubaruku ilianzishwa kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa mwaka 2000

Kata hii imepakana na kata za Rujewa upande wa Kaskazini, Imalilosongwe Upande wa Kusini na  upande wa Mashariki imepakana na Mapogoro.

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vijiji kuna Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Maafisa watendaji wa Vijiji.

Kata ya Ubaruku ina jumla ya watumishi 207 wa kada mbalimbali kama ifuatavyo: Utawala 9, Elimu watumishi 180, Afya watumishi 8, Maliasili watumishi 0, Kilimo watumishi 5, Mifugo watumishi 2 na Maendeleo ya jamii watumishi 3.

Kata ya Ubaruku ina Jumla ya Vijiji 8 ambavyo ni Kijiji cha Ibohora, Kijiji cha Ubaruku, Kijiji cha Utyego, Kijiji cha Mkombwe, Kijiji cha Mwakaganga, Kijiji cha Mbarali, Kijiji cha Mpakani na  Kijiji cha Majjengo. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo 50

Kata ya Ubaruku ina jumla ya wakazi wapatao 29,197 kati yao Wanaume 14,257 na Wanawake 14,940. Makabila yanayopatikana katika Kata ya Ubaruku ni Wasangu, Wabena, Wagogo, Wasukuma, Wamasai na Wahehe.

Shughuli kubwa za kiuchumi kwa wananchi wa kata hii ni Kilimo, Mifugo na Biashara.

Vyanzo vya Mapato katika kata hii inatofautiana kutokana na Kijiji kimoja hadi kingine, miongoni mwa vyanzo hivyo ni kama; faini/adhabu mbalimbali, pawatila za Vijiji, michango ya wananchi, Ushuru wa mashamba na ushuru mdogomdogo, Ruzuku kutoka Serikali kuu (Halmashauri ya Wilaya) pamoja na misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali.

Vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kata ni pamoja na Misitu ya asili.

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha kila Kijiji kina Kamati ya Ulinzi na Usalama ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana vilevile kuna kituo cha police cha kata pamoja na kituo cha polisi Wilaya kilichopo kata ya jirani ya Rujewa umbali wa Km 11 ambapo sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

 

2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

 A. ELIMU

Kata ya Ubaruku ina Jumla walimu 180 wa Serikali, shule za Msingi za Serikali 7, shule za msingi za binafsi 2 shule ya sekondari binafsi 1, Na shule ya sekondari ya Serikali 1.

 i. ELIMU MSINGI

Shule za Serikali

  • Shule ya Msingi Ubaruku
  • Shule ya Msingi Ibohora
  • Shule ya Msingi Ujewa
  • Shule ya Msingi Mpakani
  • Shule ya Msingi Mkombwe
  • Shule ya Msingi Utyego.
  • Shule ya Msingi Mbarali

Shule za Msingi Binafsi

  • Shule ya Msingi Gamaliel
  • Shule ya Msingi St. Ann’s

 

 ii. ELIMU SEKONDARI

     Shule za Serikali

  • Shule ya Sekondari Mbarali,

    

Shule za Binafsi

  • Shule ya Sekondari Montfort

B. AFYA

Kata ya Ubaruku ina watumishi wa idara ya afya 8, Kituo cha Afya 1 (Binafsi) na zahanati 3 ambazo ni Zahanati ya Ubarku, Mahungurulo Zahanati na A&A zahanati. Magonjwa yanayosumbua mara kwa mara ni ; Diarrhea, URTI upper respiratory Infection, Pneumonia, UTI- Unary track Infection, fracture –(Dislocation), Surgical condition, Burn, Skin Infection Fungal, Skin Infection non fungal na Fungal Infection non skin.

C. KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA

Kata ya Ubaruku ina jumla ya watumishi 5 idara ya kilimo na ushirika, na ina jumla ya wakulima 9,082, wanawake 3700 wanaume 3,727. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 7,005. Mazao yanayopatikana katika kata ya ni Mpunga, Mahindi, Alizeti, Mtama, Viazi Vitamu, Maharage, Karanga, maharage, mihogo na Vitunguu

idadi ya skimu za umwagiliaji zilizopo ni Ibohora na Mwendamtitu. Vilevile kuna chama cha ushirika kimoja ambacho ni Ubaruku SACCOS

Pia ndani ya Kata ya Ubaruku kuna kampuni moja binafsi ijulikanayo kama Mbarali Estate inalojishughulisha na kilimo cha mpunga lenye ukubwa.

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ;

  • Huduma za ugani
  • Mashamba darasa juu ya Kilimo cha Kisasa
  • Hifadhi bora ya Mazao ya Chakula
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Kutatua Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao
  • Kukusanya takweimu za Mvua
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji ya kila robo mwaka na kuwasilisha wilayani.
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Kilimo katika Kamati ya Maendeleo ya kata.

D. MIFUGO NA UVUVI

Kata ya Ubaruku ina jumla ya watumishi 2 wa idara ya mifugo na Uvuvi.

Magonjwa yanayosumbua mifugo mara kwa mara ni kama homa ya mapafu, foot and mouth diseases, anthrax,

Huduma zinazotolewa na Idara ni pamoja na;

  • Tiba kwa magonjwa dhidi ya Mifugo
  • Huduma mbalimbali za Mifugo kama kuhasi, kukata pembe, kwato na midomo, kupiga chapa Mifugo, kukata meno, kuzalisha, kuogesha na Ukaguzi wa nyama
  • Ushauri juu ya ujenzi bora wa mabanda ya Mifugo
  • Kutoa elimu ya ufugaji bora wa namna ya ufugaji wa Mifugo yenye tija
  • Ukaguzi wa Nyama na usafi katika Machinjio
  • Kusimamia zoezi Endelevu la upigaji chapa wa mifugo

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata hii. Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.

E. MALIASILI

Kata ya Ubaruku haina watumishi wa maliasili mpaka sasa, na Kata ya Ubaruku ina uhifadhi wa misitu katika kijiji cha Ubaruku ina uhifadhi mazingira na misitu kwa kusimamiwa na kamati za mazingira za vijiji.

 i.Vivutio vya Utalii

  • Msitu ya asili uliopo eneo la kanisa Katoriki.,

 ii. Hifadhi ya Misitu

Kata ya Ubaruku inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzai wa hifadhi kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), kupanda miti, kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kuchoma mkaa na kukata miti hovyo bila ya kuipanda upya, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.

 ii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo. 

Kata inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya misituasili na vyanzo vya maji kwa matumizi endelevu, kuendelea kushauri kutengwa kwa bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika Vijiji.

 

F. MAENDELEO YA JAMII

Kata ya Ubaruku ina watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii 3 mpaka sasa, huduma zinazotolewa na kata ni kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA KAZI YA MKATABA YA MTUNZA KUMBUKUMBU (DATA ENTRY CLERK) NA TABIBU (CLINICAL OFFICER II) TAREHE 02-12-2022 November 28, 2022
  • RE-ADVATISEMENT JOB VACANCIES November 10, 2022
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI KATIKA KATA YA UBARUKU

    March 03, 2023
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI KANALI DENIS MWILA AKISHIRIKI ZOEZI LA USAFI NA UPANDAJI WA MITI WILAYA YA MBARALI TAREHE 18/02/2023

    February 24, 2023
  • TIMU YA CMT MBARALI NA MENEJA WA MAJI WILAYA YA MBARALI WAKIKAGUA MRADI WA MAJI

    May 15, 2022
  • AFISA UTUMISHI NA UTAWALA

    June 09, 2022
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.