• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Atakaezidisha Ujazo wa Kilo 100 au Debe Saba za Mpunga Kwenye Gunia Akamatwe, Atozwe Faini - Mfune

Tarehe ya Kuanza: May 31st, 2018

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune tarehe 31/05/2018 katika kata ya Madibira Kijiji cha Mahango Kitongoji cha Chalinze, Kwenye mkutano wa hadhara aliouitisha kwa ajili ya kuzungumza na kutoa elimu ya vipimo na ujazo wa magunia kwa wananchi wanaolima maeneo hayo.

Mhe. Mfune amewataka wananchi wote wa kata ya Madibira, Wilaya ya Mbarali pamoja na wafanyabiashara wote wa Mazao kufuata sheria zilizoweka ili kila mmoja aweze kunufaika, kwani hadi sasa kuna baadhi ya wafanyabiashara wanawaibia wakulima kwa kutumia magunia yenye ujazo usiokubalika kisheria.

 “Wale waliokuja na viroba vikubwa waviondoe, kuanzia kesho sitaki kuviona mashambani, na yeyote atakaekutwa na roba la zaidi ya debe saba au kazidisha ujazo wa kilo 100 akamatwe, agizo hili nalitoa kwa Wilaya nzima, nimeunda kikosi kazi kwa ajili ya kufuatilia maagizo yote niliyoyatoa” alisema

Akijibu hoja mbalimbali za wananchi wa maeneo hayo, Mhe. Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi wa maeneo hayo kuunda utaratibu ambao utawasaidia wakulima kuwa na umoja unaofanana ili waweze kuongea lugha moja kwani hadi sasa hakuna bei elekezi ya zao la mpunga iliyotolewa, bei zilizopo zinategemeana na nguvu ya soko, kikubwa ni kutumia teknolojia walizonazo hasa simu za mikononi kuangalia bei iliyopo sokoni kwani bila kufanya hivyo watu wachache watawaumiza.

Akijibu kuhusu suala la mikopo, Mhe. Mfune ameahidi kufanya mazungumzo na taasisi za kifedha ili waje kutoa elimu na kwa wale watakaokidhi vigezo waweze kukopeshwa fedha zitakazowasaidia kuendesha shughuli zao za Kilimo.

Kuhusiana MAMCOS (Madibira Agriculture Marketing Co-operative Society)  Mhe. Mfune amesema kuwa, kuanzia msimu ujao na kuendelea ni lazima shirika hilo lifanye kazi yao ipasavyo ikiwemo kukopa mikopo kwenye taasisi za kifedha na kuwakopesha wakulima wanachama ili iweze kuwasaidia.

Akitoa elimu ya Vipimo katika mkutano huo, Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoa wa Mbeya Ndg. Richard Mbonabucha alisema kuwa, kipimo cha kilo kwa kutumia mizani ndio kipimo kinachojulikana Kitaifa na Kimataifa na sio kama ilivyozoeleka kwa baadhi ya wafanyabiashara kutumia ndonya.

Kuhusiana na zao la mpunga Ndg. Mbonabucha aliongeza kuwa, sheria ya sasa inaruhusu utaratibu wa kufunga mpunga kwa ujazo wa kilo 75 pindi mpunga unapotoka shambani, ukiwa umehifadhiwa katika maghala ya chakula au ukiwa unapelekwa sokoni, kukiuka kufanya hivyo unakuwa umevunja sheria.

Ndg. Mbonabucha aliongzea kuwa  kwa sasa tukiwa tunasubiri mchakato wa sheria kufanyiwa marekebisho na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ujazo uwe wa kilo 100 au debe saba za mpunga, kinyume na hapo hatua za kisheria zitachukuliwa pamoja na adhabu ya faini kuanzia shilingi laki 1(TZS 100,000/=) hadi milioni 50.

Naye Diwani wa Kata ya Madibira Mhe. Erick Ngelyama amewaomba wananchi wa kata hiyo kufuata sheria zilizopo na kufuata taratibu walizokubaliana ili kuepuka kapata hasara. Vilevile amewataka kusimama imara hasa wanavyoitana kwenye mikutano yao na MAMCOS pamoja na kuvunja makundi kwani mkuu wa Wilaya yupo kwa ajili ya maslahi ya wanamadibira na wananchi wote wa Mbarali kwa ujumla.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.