• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Baraza La Madiwani Mbarali Lawashusha Vyeo Watumishi Walevi

Tarehe ya Kuanza: July 19th, 2018

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, limewashusha vyeo watumishi watatu wa Idara ya Afya kutokana na makosa ya kulewa nyakati za saa za kazi na kusababisha kuto timiza majukumu yao ipasavyo.

Watumishi hao wameshushwa vyeo hivyo siku ya tarehe 18/07/2018 kwenye Kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani ambacho kiliitishwa kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali ya Maendeleo yanayoihusu Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Akizungumza katika Baraza hilo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Mhe. Broun Mwakibete alisema kuwa, pamoja na kuwashusha vyeo watumishi hao, Baraza la Madiwani litakuwa na jicho la karibu kuangalia kama watabadilika au hawatabadilika, na kama hawatabadilika watafukuzwa kazi.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Kivuma Msangi, alisema kuwa, kabla ya kufikia uamuzi huo, watumishi hao waliitwa na kupewa onyo kwa mdomo na baadae kuandikiwa barua lakini hawakubadilika.

Msangi aliongeza kuwa licha ya kuwapa onyo pia waliunda Tume ya kuchunguza suala hilo, ambapo walibaini na kuthibitisha watumishi hao kuingia kazini wakiwa tayari wamelewe kutoroka kazini nyakati za usiku kwenda kulewa.

“Tumewaadhibu watumishi hawa kwa kuwa kuwashusha vyeo na mishahara, lengo letu ni wabadilike lakini tukiona bado wanaendelea tutawafukuza kazi kabisa,” alisema.

Akitangaza uamuzi huo mbele ya kikao cha Baraza la Madiwani Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg.  Aswege Kaminyoge kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, aliwataja watumishi hao kuwa ni Elioth Msamila na Gervas Kasimbazi Mabibu daraja la kwanza hawa wanashuka kuwa  Matabibu daraja la pili, na mwingine ni Vocus Fedrick  Mhudumu wa Afya Hospitali anaenda kuwa Mhudumu wa Ofisi.

Kaminyoge aliongeza kuwa uamuzi wa kuwashusha vyeo umepewa Baraka na Baraza la Madiwani na kwamba watumishi hao mbali na kushushwa vyeo watapunguziwa mishahara yao.

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji ambaye ni Diwani wa Kata ya Miyombweni, Mhe. Mstaulo Sanzala alisema kuwa uamuzi huo uwe fundisho kwa watumishi wengine wanaoendekeza ulevi sehemu za kazi. Aliongeza kuwa endapo Kamati yake itapata taarifa na kuthibitisha kuwa kuna mtumishi ambaye anakunywa pombe mahali pa kazi watamchukulia hatua ikiwemo kushushwa cheo au kufukuzwa kazi bila kujali cheo wala umaarufu wake.

Katika Kikao hicho cha robo ya nne, Baraza la Madiwani lilijadili masuala mbalimbali ya Maendeleo yakiwamo, Mpango wa Motisha kwa Watumishi kwa mwaka 2018/2019-2020/2021, Mpango wa Kuondoa Biashara zinazofanyika kando kando ya barabara kuu ipitayo katika miji midogo ya Ilongo, Igurusi, Chimala na Igawa, Maombi ya Idhini ya Matumizi ya sh, 100,000,000.00 kwa ajili ya Ukamilishaji wa ukarabati wa kituo cha afya Utengule Usangu.

Ombi la kubadilisha Matumizi ya Soko la Igawa Kuwa Stendi ya Mabasi, Taarifa ya Shule ya Sekondari Rujewa kuto pewa wanafunzi wa kidato cha Tano mwaka 2018, Taarifa ya Idara ya Maji kuhamia Wizara ya Maji na Idara ya Ardhi na Maliasili kitengo cha Ardhi Kuhamia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Masuala ya kiutumishi ikiwemo Uteuzi wa Wakuu wa Idara, mapendekezo ya kukaimu nafasi za ukuu wa Idara pamoja na masuala ya kinidhamu.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • SALAMU ZA EID EL FITR

    March 31, 2025
  • DC MBARALI AANDAA HAFLA YA IFTALI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE,TASISI ZOTE NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU..

    March 28, 2025
  • DC MBARALI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA CHIMALA

    March 14, 2025
  • KIKAO CHA DCC KUPENDEKEZA MAJINA YA MAJIMBO WILAYANI MBARALI

    March 13, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.