• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC Akataa Siasa Katika Utekelezaji wa Mambo ya Maendeleo.

Tarehe ya Kuanza: November 6th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune, amewataka viongozi wote katika Wilaya ya Mbarali kuacha masuala ya kisiasa katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo kwenye wilaya yake kwani mambo hayo ya kisiasa wawaachie watu wanaohutubia kwenye majukwaani wakati wa kampeni za kuomba kura, yeye anachotaka ni kuona miradi ya maendeleo inatekelezwa.

Mhe. Mfune ameyasema hayo alipokuwa kwenye mwendelezo wa ziara zake katika kata za Igava, Miyombweni pamoja na Madibira siku ya tarehe 05/11/2018 kwa ajili ya kufuatilia maagizo aliyoyatoa kwa viongozi wa kata na vijiji  kuhusiana na ujenzi wa vyumba vya madarasa, Ujenzi wa zahanati, ujenzi wa vyoo, masuala ya lishe pamoja na uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5.

Kuhusiana na ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na zahanati, Mkuu wa Wilaya ameipongeza Kata ya Igava kwa kutekeleza maagizo aliyoyatoa kwa asilimia kubwa kwani wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na kufikia hatua nzuri kwenye ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji, ila amewataka zoezi hilo la ujenzi wa madarasa liende sambamba na utengenezaji wa madawati.

“Naridhika na Kata ya Igava katika utekelezaji wa maagizo ya Serikali, mnafanya vizuri katika ujenzi wa zahanati na madarasa endeleeni na spidi mliyonayo, tukikamilisha wote tutaunganisha nguvu katika ujenzi wa kituo cha afya”

Katika hatua nyingine, Mhe. Mfune amezipongeza Kata za Miyombeni na Madibira kwenye suala la uhamasishaji kwa wananchi kujenga vyoo, kwani kwa hatua walizofikia, ni kaya chache tu katika kata hizo ambazo hazijakamilisha ujenzi vyoo ukilingazisha na Kata ya Igava ambapo kuna kaya zipatazo 576 ambazo hazina vyoo kabisa.

“Kaya 576 kukosa vyoo ni tatizo kubwa, wote tunajua kwanini tunahamasisha watu kuhusu  ujenzi wa vyoo.  Lazima watu wajenge kwa vyoo kwa nguvu, hatuwezi kubembelezana suala linalogusa afya zetu, kila mtu lazima awe na choo, kilo 10 za simenti (saruji) zinaweza kutengeneza  choo kikasafishika na ukiweka sinki la plastiki aina ya SATTO unapata choo bora. Tuendelee kuhamasisha wananchi”

Aliongeza kuwa kufikia tarehe 01/12/2018 hataki kusikia kuna kaya ambayo haina choo katika Wilaya yake ya Mbarali sababu kwa sasa tunakoelekea kipindi cha masika, na safari hii hataki kusikia tena magonjwa ya milipuko kama kipindupindu na kuhara maana wote ni mashahidi kwa kilichotokea mwaka 2017 watu zaidi ya 800 waliugua ugonjwa kipindupindu na baadhi walipoteza maisha na moja ya sababu kubwa iliyopelekea ugonjwa huo ni kukosa vyoo kwa baadhi ya kaya.

Kuhusiana na Uandikishiji wa Vyeti vya Kuzaliwa pamoja na Masuala ya Lishe, Mhe. Mfune alisema kuwa, mambo haya ni endelevu, ni vyema tukatumia sehemu zetu za kuabudia katika kutoa elimu ya vitu hivi.

“Tutenge walau dk 10 kwa ajli ya kutoa elimu ya lishe na kupata vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5, tuwaelekeze wananchi umuhimu wake Katika kila mkutano wa hadhara wa kijiji kwa kuwa masuala haya ni endelevu.  Kwa sasa vyeti vya kuzaliwa vinatolewa bure kwa wototo wenye umri wa chini ya miaka 5, baada ya hapo watalazimika kuvilipia.  Wenyeviti wa vijiji pamoja na watendaji tengenezeni utaratibu na muwatangazie wananchi mzunguko wa uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa na katika shughuli zenu za kawaida muwe mnapita kwenye kaya zenu na kuuliza kama kuna watoto ambao hawajaandikishwa.”

“Siku 1000 ndio kipindi cha kujenga  ubongo wa mtoto, na hizo siku zinaanzia tangu mimba inapotungwa hadi mtoto anapotimiza miaka 2, na baada ya hapo haitawezekana tena kumrekebisha,  tunakusudia kutunga sheria ndogo ili wale watakaokaidi kuwapeleka watoto wao kupata utambuzi wa lishe wachukuliwe hatua, lengo letu ni kuepuka kuwa na kaya zenye watoto wenye udumavu au lishe duni. Tunataka kujenga taifa la kesho lililoelimika vizuri kupambana na changamoto na kupiga hatua katika maendeleo”

Mkuu wa Wilaya amemaliza ziara katika kata zote 20 kwa ajili ya kuhamasisha wananchi kujenga vyumba vya madarasa, kujenga zahanati kwa kila kijiji, kujenga vyoo, uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 pamoja na masuala ya lishe tangu inapotungwa mimba hadi mtoto anapofukisha umri wa miaka miwili (siku 1,000).

Mkuu wa Wilaya anatarajia kufanya mkutano na waandishi wa habari siku ya alhamisi ya tarehe 08/11/2018 na kutoa maelekezo ya ujumla kuhusiana na ziara alizozifanya.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.