• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC Awakemea Wanaosuasua Kuanza Ujenzi wa Zahanati

Tarehe ya Kuanza: October 31st, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune, amevitaka vijiji vyote ambavyo havijaanza ujenzi wa Zahanati katika Wilaya ya Mbarali kuanza mara moja ndani ya mwezi wa 11.

Mhe. Mfune ameyasema hayo alipokuwa kwenye mwendelezo wa ziara zake katika kata za Mawindi na Ipwani zilizopo tarafa ya Rujewa siku ya tarehe 30/10/2018 kwa ajili ya kufuatilia maagizo aliyoyatoa kwa viongozi wa kata na vijiji  kuhusiana na ujenzi wa vyumba vya madarasa, Ujenzi wa zahanati, ujenzi wa vyoo, masuala ya lishe pamoja na uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5.

“Nataka ndani ya mwezi wa 11, zahanati zote wilayani mbarali ambazo hazijaanza kujengwa, ziwe zimeanza kujengwa”

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amewapongeza viongozi wote wa kata ya Ipwani wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Marcusi Kalinga kwa hatua nzuri waliyofikia katika kukamilisha ujenzi wa shule ya sekondari Ipwani kwani kukamilika kwake kutasaidia  upatikanani wa elimu kwa wanafunzi wa kata ya Ipwani.

“Nimevutiwa na hatua ya Ujenzi mliyofikia, hadi sasa kuna mabadiliko makubwa tangu nilivyofika awamu iliyopita mwezi julai, wananchi wamejitahidi sana nipo tayari tuitishe harambee ili kumalizia vitu vilivyobaki, kwani kukamilika kwa shule hii kutapunguza mzigo katika shule jirani ya Mawindi”

Vilevile Mhe. Mfune ameendelea kuwasititiza wananchi wote kujenga vyoo bora ili ifikapo tarehe 01/12/2018 suala la kutokuwa na vyoo liwe historia katika wilaya ya Mbarali na amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya kata hadi vijiji kuwafikisha kwenye mabaraza ya kata wale wate ambao hawana vyoo mpaka sasa.

“Kuna baadhi ya watu wanajua kula tu, ila kujenga vyoo hadi tulazimishane, majadilianao ya kujenga vyoo yafikie mwisho, tunataka kufikiria kujenga zahanati, vyumba vya madarasa pamoja na mambo mengine ya maendeleo, vilevile adhabu itolewe kwa wale waliojenga  vyoo ila hawavitumii”

“Niwapongeze Kata ya Ipwani kwa kufanyia kazi suala la kutokuwa na vyoo, sasa tuhame kutoka kwenye vyoo vya asili kwenda kwenye vyoo bora, choo bora ni choo kilichojengwa kwa tofari, kinachosafishika, kilichoezekwa na kuwa na mlango, hatufanyi haya ili kujifurahisha ila ni kuepukana na magonjwa ya mlipuko”

Kuhusiana na Masuala ya lishe na uandikishaji wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kupata vyeti vya kuzaliwa, Mhe. Mfune alisema kwamba mambo haya ni endelevu, yanahitaji kutolewa elimu kila mara, viongozi wa vijiji na kata wanatakiwa kutoa japo dakika 10 kwa waelimishiji kwenye kila mikutano hadhara ili elimu hii ziweze kutolewa.

“Vyeti vya kuzaliwa vina faida nyingi sana, sasa hivi mtoto ni lazima awe na cheti cha kuzaliwa, vyeti hivi chini ya miaka 5 vinatolewa bure, baada ya hapo watatakiwa kuvilipia, tuendelee kuhamasisha ili kila mtoto aweze kuandikishwa.”

“Mtoto akikua na hali ya udumavu kila kitu kinavia, sababu ubongo unakuwa haujakua vizuri, tuendelee kuelimisha wananchi madhara na faida zake na ifike mahali ambapo mtu ambaye hampeleki mtoto wake kupimwa utambuzi wa hali ya lishe (ukondefu, uzito pungufu na udumavu) apigwe faini na faini hizo zitumike kusidia kuwajengea vyoo wale ambao hawajiwezi.”

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.