• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DC MBARALI ATOA SIKU 14 KWA TAKUKURU NA MKAGUZI WA NDANI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI KUCHUNGUZA MATUMIZI YA FEDHA UJENZI WA BWENI SHULE YA MSINGI IGOMELO

Tarehe ya Kuanza: March 3rd, 2025

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mhe Kanali Maulid Hassan Surumbu, ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ndani ya siku 14  ahakikishe Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri amekagua  matumizi ya Fedha katika Ujenzi wa Bweni la watoto wenye Mahitaji maalumu  Shule ya Msingi Igomelo Kata ya Lugelele Wilaya ya Mbarali. Aidha, Mheshimiwa Maulid amemwagiza Mkuu wa  TAKUKURU Mbarali kuchunguza utaratibu wa Fedha zilivyotumika katika Ujenzi wa Bweni hilo ndani ya siku 14. 

"Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Mbarali inatoa maelekezo kwa Mkurugenzi; Kwanza Mkaguzi wa Ndani akague Matumizi ya Fedha yaliyotumikq kwenye ujenzi wa Jengo hili na ripoti yake ikamilike ndani ya siku 14. Pia namwagiza Mkuu wa  TAKUKURU Wilaya, naye aje achunguze utaratibu uliotumika katika Ujenzi huu kuanzia mwanzo mpaka mwisho tujue matumizi ya fedha yamekwendaje na ndani ya siku 14 aweze kuwasilisha taarifa ili yeyote ambaye ametenda kinyume na majukumu yake aweze kuwajibishwa"

Mheshimiwa Maulid ameyasema hayo mapema hii leo tarehe 03.03.2025 wakati Kamati ya Ulinzi na Usalama ikifanya Ziara ya kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

Aidha Kamati hiyo imesifia na kupongeza usimamizi wa Mradi wa Ujenzi wa vyumba Viwili vya madarasa  katika shule ya Msingi Majengo iliyopo Kata ya Ubaruku kijiji cha Majengo. Hata hivyo Kamati iliendelea na Ziara kwa kutembelea Viwanda vya Kuchakata Mpunga katika eneo la Viwandani Kata ya Ubarukuna kujionea namna shughuli zinavyoendeshwa katika viwanda hivyo.  

Mradi huo wa Viwanda umezalisha  Ajira zaidi ya 1500 kwa Vijana wa  Mbarali ambao wanafanya kazi katika Viwanda hivyo na kujipatia kipato ili kujikimu katika maisha. Hata hivyo  Umoja wa Wenye Viwanda Ubaruku wameibua Changamoto ya kukosa masoko ya uhakika pamoja na Miundombinu ya Barabara kuwa ya kupitika kwa msimu. Nao Wakuu wa Idara wa Halmshauri ya Wilaya ya Mbarali wameahidi kutatua Changamoto hiyo. Aidha Mheshimiwa Maulid amesema unapotafuta soko ni lazima kuwa na uzalishaji wa uhakika na sio kutafuta soko halafu baadae unakosa mazao ya kuwauzia wale ulioahidi kuwapelekea bidhaa yako.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • SALAMU ZA EID EL FITR

    March 31, 2025
  • DC MBARALI AANDAA HAFLA YA IFTALI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE,TASISI ZOTE NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU..

    March 28, 2025
  • DC MBARALI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA CHIMALA

    March 14, 2025
  • KIKAO CHA DCC KUPENDEKEZA MAJINA YA MAJIMBO WILAYANI MBARALI

    March 13, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.