• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

DED Mbarali awataka Tume ya Utumishi wa Walimu kuzingatia Sheria na Miongozo wanapofanya maamuzi.

Tarehe ya Kuanza: July 13th, 2020

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma H. Msangi amewataka wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu ngazi ya Wilaya (TSC) kushughulikia masuala ya kinizamu ya walimu kwa kufuata sheria zilizopo ili waweze kutenda haki kulingana na makosa yaliyofanywa.

Ameyasema hayo siku ya tarehe 13/07/2020 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbarali ulipo Kata ya Lugelele alipokwenda kusimamia zoezi la kuwaapisha wajumbe wapya wa kamati   hiyo walioteuliwa kushughulikia masuala ya ajira na nidhamu, rufaa ngazi ya Wilaya pamoja na masuala ya maendeleo kwa watumishi wa shule za msingi na sekondari walio katika Utumishi wa Serikali.

“Ni jambo la heshima sana kupewa nafasi ya uteuzi kwa ngazi yeyote ile kwenda kuwatumikia watu. Mnakwenda kushughulikia maslahi na maisha ya watu, jambo hili linahitaji umakini sana, kikubwa kinachohitajika ni uadilifu katika kufanya uchunguzi pamoja na maamuzi kwa kufuata Miongozo, waraka na sheria bila ya kumuonea yeyote.”

“Wakuu wa shule za sekondari na msingi mnatakiwa kufanya ufuatiliaji wa walimu walio chini yenu kabla ya kuniletea ili nipeleke kwenye Tume kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na maamuzi.”

Katika hotuba yake Msangi aliongeza kuwa mwaka 2019 Wilaya ya Mbarali imepata usajili wa shule 2 za sekondari, mwaka huu 2020 wamepata usajili wa shule 6 za sekondari pamoja na za kidato cha tano na sita mbili, pamoja na usajili wa shule 4 za msingi na wanatarajia kupata usajili wa shule za sekondari 3 ifikapo mwaka 2021.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake walioapishwa Mwenyekiti ya Kamati Mpya ya Tume ya Utumishi wa Walimu Mwl. Stella Mbinda ameushukuru uongozi wa TSC Taifa kwa nafasi ya pekee waliyoapa na ameahidi kwenda kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, kufuata maadili na umakini mkubwa bila ya kumuonea yeyote.

Naye Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Mbarali Mwl. Issa Shemgei alisema kuwa kwa mwaka 2016 hadi 2020 wamepokea masuala ya kinidhamu 37, kati ya mashauri hayo walimu 24 wamefukuzwa kazi, 7 wamepewa karipio, 1 amepewa onyo, 1 ameshushwa cheo na 4 wanasubili uchunguzi na maamuzi ya kamati.

Mwl. Shemgei aliongeza kuwa, kati ya mwaka 2016 hadi 2020 jumla ya walimu 99 wameajiliwa na katika kipindi hicho walimu 377 wamepandishwa vyeo na walimu 76 wamebadilishiwa vyeo vya kimuundo baada ya kujiendeleza kielimu kwa ngazi mbalimbali.

Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Mbarali ni pamoja na Mwl. Stella Mbinda (Mwenyekiti), Mwl. Issa Hemgei (Katibu), Mwl. John Luena (Mjumbe), Mwl. Grolia Spotwa (Mjumbe),  Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Mwl. Anna Shitindi (Mjumbe) pamoja na Katibu Tawala Wilaya ya Mbarali Ndg. Michael Semindu (Mjumbe).

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.