• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

“Kuna Utaratibu wa Kufuata Kuwaondoa Viongozi wa Vijiji”

Tarehe ya Kuanza: November 18th, 2017

Hayo yamesemwa  na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune kwenye mkutano wa hadhara aliouitisha kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za Wananchi wa Kijiji cha Ijumbi kilichopo Kata ya Ruiwa Wilaya ya Mbarali siku ya tarehe 17/11/2017.

Akiongea na wananchi wa Kijiji hicho katika mkutano huo, Mhe mfune alisema kuwa, alipokwenda katika Kijiji hicho mwezi uliopita aliwaambia kuwa jukumu la kumuondoa Mwenyekiti na Wajumbe ni la wananchi waliomchagua, na angeagiza Halmashauri ambayo inasimamia Vijiji waendelee na mchakato kama mwenyekiti hatoshi kwa mujibu wa tuhuma zake aondolewe kwa kwa kufuata utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria, wataalamu walishakuja na utaratibu umetumika kwa ajili ya kumuondoa mwenyekiti, vilevile  kama Mwenyekiti hajaridhika na maamuzi ya kumuondoa anaweza kwenda kukata rufaa kwa Mkuu wa Mkoa.

“Sikuja hapa kuja kuwalinda watu waliochaguliwa kama hawafai kuendeleza Kijiji, kama hawawezi kupeleka maendeleo yetu mbele,wapo kwa maslahi yao na tuna uhakika na ushaidi basi utaratibu ufuatwe kuwaondoa”

Kuhusu suala la kusoma mapato na matumizi ya Kijiji, Mhe Mfune ameagiza ndani ya siku saba uitishwe mkutano mkuu wa Kijiji kwa ajili ya kuwasomea wananchi mapato na matumizi ya Serikali yao, vilevile ameagiza kila baada ya miezi mitatu wananchi wasomewe mapato na matumizi ya Serikali yao.

Mhe. Mfune amewaasa Serikari ya Kijiji kutojichukulia madaraka ya kufanya kila kitu bila ya kupata ridhaa ya wananchi kupitia mikutano mikuu ya Kijiji, vitu vyote vinavyoletwa kwa ajili ya maslahi ya wananchi kutoka sehemu mbalimbali, mfano mabati, simenti na mengineyo  lazima kuwaeleza wananchi, Serikali ya Kijiji inatakiwa kupendekeza matumizi ya bidhaa hizo na kuwasilishwa kwa wananchi kwa ajili ya kupitisha matumizi yake.

Kuhusu suala la mifugo maeneo ya misitu katika Vijiji vya Motomoto na Malamba, Mhe Mkuu wa Wilaya alishapiga marufuku kwa wale wanaolima, wanaojenga na wanaochunga mifugo yao kwenye maeneo hayo au kwenda kufanya shughuli za kibinadamu kwani kufanya hivyo  kunaharibu eneo la hifadhi ya misitu ambayo ni vyanzo vikubwa vya maji katka maeneo Wilaya yetu, na kuna watu wanaohusika na amewaweka kwa ajili ya kulinda eneo hilo la hifadhi ya misitu, kwa maeneo ambayo watu wanakata miti na wanachoma mkaa hasa kata ya Ipwani, kuna  baadhi ya watu wameshawakamatwa na wapo polisi na magari yao na watachukliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

 Akizungumza katika mkutano huo, Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Ndg. Aswege Kaminyoge, alitoa utaratibu wa kuwaondoa viongozi wa Serikali za Vijiji ambapo alieleza kuwa, Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa, Majiji pamoja na Vijiji zimeanzishwa na sheria namba 7 ya mwaka 1982, ni utaratibu wa kisheria kwa Serikari ya Kijiji kufanya shughuri za kila siku za uendeshaji wa Kijiji.

“kwa mujibu wa sheria kwa Vijiji vilivyosajiliwa vinatakiwa kukutana kila baada ya miezi mitatu ambayo ni mara nne kwa mwaka, mwenyekiti wa Serikari ya kijiji pamoja na Mtendaji wa Kijiji kwa kushirikiana na wajumbe wa Serikali ya kijiji wana wajibu wa kuitisha mikutano hiyo”

Kaminyoge aliongeza kuwa, suala la kumuondoa Mwenyekiti madarakani pamoja na wajumbe wa Serikali, kwa  mujibu wa taratibu na kanuni zilizotungwa mwaka 1995, wenye mamlaka ya kumuondoa Mwenyekiti ni Halmashauri ya Serikali ya Kijiji yenye watu 25 kwa kupiga kura mara baada kupitia tuhuma zilizopatikana kwenye mikutano mikuu ya Vijiji kwa wananchi ambao walimchagua.

Kwa upande wa Wajumbe wa Serikali za Vijiji, alisema kuwa, wenye mamlaka ya kuwaondoa madarakani ni mkutano mkuu wa Kijiji, kama mjumbe ana tuhuma au ana mwenendo mbaya katika Serikali, kitakachofanika ni kwamba, itatolewa hoja ya kutokuwa na imani na mjumbe huyo, anaweza akawa mmoja au wawili au zaidi waliotuhumiwa, itajadiliwa kwenye mkutano huo, baada ya hapo itapigwa kura ya kutokuwa na imani nae au nao, ili kuweza kuwaondoa wanatakiwa kufuata utaratibu huo.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.