• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Madiwani Kyela Wafanya Ziara ya Mafunzo Mbarali

Tarehe ya Kuanza: November 29th, 2017

Waheshimiwa Madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyela wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo  Mhe. Hunter A. Mwakifuna pamoja na baadhi ya Wataalamu wamefanya ziara ya kujifunza namna ya matumizi ya bora ya “Force Account” na namna bora ya kuzuia vifo vya mama na mtoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali siku ya tarehe 28/11/2017.

Akiwakaribisha wageni hao Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mhe. Francis Mtega, alishukuru ujio wa wageni hao na kuwatajia fursa mbalimbali zinazopatikana Wilayani hapa, ikiwemo kilimo cha mpunga ambacho kinatumia maji kidogo na ndio chanzo kikubwa cha mapato ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Katika ziara hiyo wameweza kujifunza matumizi ya “Force Account (utekelezaji wa kazi kwa kutumia mafundi wa kawaida bila ya kutumia wakandarasi)” kutoka shule ya Sekondari Rujewa ambapo, Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiaa na Wizara ya Elimu Sayansi na Technolojia kupitia Program ya Lipa Kulingana na Matokeo (P4R) ilitoa fedha za ujenzi na ukarabati kupitia akaunti ya shule ya Sekondari Rujewa kiasi cha Tsh. 259,000,000.00/=. Fedha hizo zilitakiwa zitumike katika Ujenzi wa Miundombinu, kama Ujenzi wa Mabweni Mawili (2) kwa ajili ya kidato cha tano na sita pamoja na vitanda,mabweni hayo yana uwezo wa kuchukua wanafunzi 80 kwa kila moja kwa gharama ya Tsh. 150,000,000.00, Ujenzi wa vyumba vinne (4) vya madarasa vyenye meza na kiti kwa thamani ya Tsh. 80,000,000.00/=, Umaliziaji/ukarabati wa maabara kwa thamani ya Tsh.18,000,000.00 pamoja na Ujenzi wa matundu kumi ya vyoo kwa thamani ya Tsh.11,000,000.00

Wakiwa katika zahanati ya Uturo ambayo ndio zahanati ya mfano kitaifa katika kudhibiti vifo vya mama na mtoto, zahanati hiyo kwa muda wa miaka 19, Tangu mwaka 1998 hakuna vifo vya watoto wachanga wala wazazi vinavyotokana na matatizo ya uzazi vilivyotokea katika kijiji cha Uturo. Wakiwa katika zahanati hiyo iliyopo Wilaya ya Mbarali kata ya Mapogoro kijiji cha Uturo wameweza kujifunza mambo mablimbali ambayo yatasaidia kupunguza na kukomesha vifo dhidi ya mama na mtoto.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Mhe Hunter A. Mwakifuna amemshukuru Mganga mfawidhi ndugu Wilson Chotamganga na Wananchi wa Kijiji cha Uturo kwa juhudi zao na kuweza kufanikisha jambo hilo.

“Wananchi wameelewa kuwa zahanati hii ni mali yao, na wametusubiri tangu asubuhi, namshukuru Mganga mfawidhi ndugu Wilson Chotamganga na namtakia kila la kheri katika likizo yake ya kustaafu” alisema Mhe. Mwakifuna

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Ndg Mussa J. Mgata amepongeza ubunifu uliofanyika katika zahanati hiyo na kuahidi kuwachukua baadhi ya wataalamu na akinamama waliounda kikundi cha kupambana na vifo vya mama na mtoto kwenda Wilayani Kyela kutoa mafunzo.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mhe. Broun Kwakibete amewashukuru kwa kufanya ziara ya kuja kujifunza mambo kuhusu matumizi ya "Force Account" na namna ya Kuzuia Vifo vya Mama na Mtoto, na ameahidi kuwa nao watakwenda kujifunza mambo mbalimbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.