• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mbarali watakiwa Kupunguza Migogoro na Wawekezaji

Tarehe ya Kuanza: July 30th, 2018

WAKAZI wa kijiji cha Kapunga, kata ya Itamboleo wilayani Mbarali mkoani Mbeya wametakiwa kupunguza migogoro na mwekezaji Kampuni ya Kapunga Rice Project Limited na badala yake wajipange kunufaika na uwepo wa kampuni hiyo jirani nao.

Miongoni mwa mambo watakayonufaika nayo ni pamoja na ujenzi wa miradi ya maendeleo iwapo watakaa chini na kuiibua ili kampuni hiyo iwasaidie kuitekeleza.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitoa rai hiyo akiwa ziarani wilayani Mbarali alipoweka jiwe la msingi katika Kituo cha Afya kilichojengwa na kampuni ya Kapunga Rice ambapo hadi sasa zimetumika shilingi milioni 530 lakini hadi kukamilika kwa ujenzi zitatumika Shilingi Milioni 625.

Kwa mujibu wa Katibu Tawala wilaya ya Mbarali, Ezekiel Kilemile maandalizi ya ujenzi wa Kituo hicho yalianza Septemba 2017 na ujenzi ukaanza Januari mwaka huu na hadi sasa kazi inaendelea chini ya usimamizi wa Serikali ya kijiji cha Kapunga.

Kilemile alisema pia Kampuni ya Kapunga imeahidi kununua vitendea kazi mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa majengo na alivitaja vifaa hivyo kuwa ni vitanda,  meza, makabati, skrini na kompyuta vyenye gharama ya jumla ya shilingi milioni 70 hivyo mchango wa jumla wa kampuni utakuwa shilingi milioni 695 ikijumuishwa na ujenzi.

Katibu Tawala huyo alisema pia katika kuunga mkono juhudi za kampuni hiyo za kuwafikishia wananchi huduma za afya karibu, Halmashauri ya wilaya Mbarali imechangia zaidi ya shilingi milioni 14.6 kwaajili ya kufikisha umeme kwenye kituo hicho cha afya kitakachokuwa na uwezo wa kuwa na vitanda 42 kwa wakati mmoja kwa wagonjwa wa aina tofauti.

Kufuatia mchango huo, Mhe. Suluhu alisema ni wakati kwa wakazi wa kijiji cha Kapunga na vingine vilivyopo jirani na eneo la Kampuni hiyo kuacha kuzalisha migogoro isiyo na tija na badala yake waone manufaa yanayopatikana kutokana na uwepo wa kampuni husika.

“Kama awali Kampuni ilikuwa ijenge zahanati baadaye mkaiomba iwajengee Kituo cha afya na ikakubali hii ni faida kubwa kwenu.Sasa achene migogo maana huku Mbarali kumekuwa kila kukicha tunasikia migogoro.Tumieni fursa hii ili kila mwaka msaidiane na kampuni kufanya maendeleo.Wasaidieni pia wawekezaji wanaokuja huku ili nao wazalishe kwa faida ili nanyi mnufaike zaidi”alisisitiza makamu wa rais.

Mhe. Suluhu pia aliahidi Serikali kuchangia katika ujenzi wa nyumba za watumishi wa kituo hicho unaoendelea ambapo kwa sasa wananchi wanatoa michango ya hali na mali ili kuendeleza ujenzi wa jengo moja lenye uwezo wa kuishi familia za watumishi wawili.

Kwa upande wake Naibu Spika wa Bunge Mhe Tulia Akson Mwansasu aliahidi kuchangia mifuko 200 kupitia Taasisi ya Tulia Trust kama mchango wake kwenye ujenzi wa nyumba za watumishi wa kituo hicho cha Afya.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • SALAMU ZA EID EL FITR

    March 31, 2025
  • DC MBARALI AANDAA HAFLA YA IFTALI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE,TASISI ZOTE NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU..

    March 28, 2025
  • DC MBARALI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA CHIMALA

    March 14, 2025
  • KIKAO CHA DCC KUPENDEKEZA MAJINA YA MAJIMBO WILAYANI MBARALI

    March 13, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.