• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mhe. Rais Magufuli awataka wananchi wa Mbarali wasubiri uamuzi wa Serikali juu ya hatma ya Vijiji 33 vilivyopo ndani ya Hifadhi

Tarehe ya Kuanza: May 3rd, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakazi wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kuendelea kuvuta subira wakati wakisubiri uamuzi wa Serikali juu ya hatma ya vijiji 33 ambavyo kutokana na Tangazo la Serikali namba 28 la mwaka 2008 (GN namba 28) inavitaja kuwepo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Mhe.Rais Magufuli aliyasema hayo siku ya tarehe 02/05/2019 alipohutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Barafu uliopo katika Kata ya Rujewa wilayani Mbarali.

Alisema kuwa, ripoti ya Tume ya Mawaziri nane iliyoundwa ilikwisha kamilisha kazi yake na kukabidhi taarifa kitakachofuata ni kumalizia mgogoro huo.

Amewataka wakazi wa Mbarali kuondoa hofu kwani atahakikisha maamuzi yatakayofanyika yanabeba maslahi mapana ya wananchi wa Mbarali hasa ikizingatiwa kuwa wana uhitaji mkubwa wa ardhi kwaajili ya shughuli za kilimo na ufugaji

 “nataka niwaambie ndugu zangu wa Mbarali, Serikali mliyoiweka madarakani kamwe haiwezi kuwaonea, naomba mtuamini tufanyie kazi ripoti ya Mawaziri na tutaleta majibu, lakini kile kijiji cha machimbo ambacho wananchi wake walidai fidia na walilipwa takribani shilingi Milioni 800, hao itabidi waondoke” 

Aidha Mhe. Rais amewaagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Willium Lukuvi, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma Msangi, kumpelekea orodha ya wananchi waliogawiwa ekali 6027 kutoka kwa wawekezaji waliogawiwa mashamba ya Mpunga ya Kapunga na Highland Estate.

Pamoja na kuagiza apatiwe orodha hiyo Mhe. Rais Magufuli amempongeza mwekezaji wa shamba la Highland Estate ambae ni Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mhe. Haroon Mulla Pirmohmed kwa kuachia sehemu ya shamba na kutoa Matrekta madogo 102 (Power Tillers) kwa vijiji vyote vya Jimbo la Mbarali na amewaonya watu wanoafanya udalali wa kuwakodisha wakulima mashamba  kwa gharama kubwa ikilinganishwa na kiwango kilichowekwa na wawekezaji hao.

Vilevile amewaonya wananchi wa Wilaya ya Mbarali kuacha majungu dhidi ya viongozi wao akiwemo Mhe. Mbunge na amewasihi kushikamana na kujielekeza kuijenga Wilaya yao ya Mbarali kwani  majungu wanayoyafanya kwa viongozi wao yanawachelewesha kufanya maendeleo.

Kwa upande wake Mhe. Waziri Lukuvi alisema ripoti ya tume ya Mawaziri nane iliyokuwa maalumu kwaajili ya kupitia maeneo yenye mgogoro wa ardhi kati ya vijiji na hifadhi za Taifa nchini ilikwisha kabidhiwa kwa Katibu Mkuu Kiongozi ikiwa na mapendekezo yaliyozingatia maoni ya wananchi wakiwemo wa Mbarali.

Mhe. Lukuvi alisema ripoti hiyo imebeba kwa asilimia kubwa ukweli wa unafuu kwa wakazi wa wilayani hapa hivyo muhimu kwao ni kuvuta subira.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbarali, Mhe. Mhe. Haroon Mulla Pirmohmed aliishukuru Serikali kwa jitihada inazofanya katika kushughulikia suala la GN namba 28 akisema ni jambo linaloleta faraja kwa wananchi wanyonge.

Mwisho.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.