• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Milioni 990 zatumika kununua nyumba 20 za Halmashauri kutoka NHC.

Tarehe ya Kuanza: July 24th, 2020

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya imenunua nyumba 20 zenye thamani ya shilingi milioni 990 kutoka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) zilizopo kata ya Lugelele eneo la Igawa kwa ajili ya matumizi ya watumishi wake.

Akiongea katika makabidhiano ya nyumba hizo siku ya tarehe 23/07/2020, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune ameipongea Halmashauri kwa kuwajali watumishi wake kwani kununua nyumba hizo kutaleta unafuu wa makazi kwa watumishi na zitawasaidia kutimiza majukumu yao ya kila siku.

“Nimekuja leo kushuhudia makabidhiano ya nyumba 20 ambazo zimeghalimu shilingi  milioni 990. Ni jambo zuri sana, niwapongeze Halmashauri kwa kuingia makubaliano na NHC kulipia nyumba hizi kwa awamu ndani ya miaka 6. Naagiza ndani ya wiki moja watumishi wote wanaostahili kuingia kwenye nyumba hizi wahamie haraka ili waanze kutoa huduma ya karibu kwa Hospitali ya Wilaya.”

“Kipaumbele cha kwanza katika ugawaji wa nyumba hizi kiwe kwa watumishi wa Idara ya Afya wanaotoa huduma katika hospitali yetu mpya ya Wilaya  kwani hospitali hiyo ipo kilometa 1.5 kutoka hapa na zitakazobaki wapatiwe watumishi wa Idara nyingine za Halmashauri.” Alisema Mhe. Mfune  

Mhe. Mfune ameahidi kuongea na wahusika akiwemo Meneja wa LATRA Mkoa wa Mbeya pamoja na Meneja wa TARURA Wilaya ya Mbarali  ili kuratibu na kutengeneza barabara itakayowafikisha wananchi  hospitali kwa  urahisi kupata Huduma za Afya.

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji, Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Emmanuel Kishimbo alisema kuwa Halmashauri imenunua nyumba hizo kwa kiasi cha shilingi milioni 990 na hadi kufikia sasa wameweza kulipa shilingi milioni 100 na wamepanga kulipa million 50 ambazo zimetokana na kuzidi kwa makisio ya  makusanyo ya ndani kwa mwaka wa fedha 2019/2020 vilevile kwa mwaka huu wa fedha 2020/2021 Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi milioni 150 ili kuendelea kulipa deni.

Ndg. Kishimbo ameishukuru NHC kwa kuiwezesha Halmashauri kujenga nyumba hizo 20 ambazo zipo jirani na ilipojengwa Hospitali mpya ya Wilaya ambayo kwa sasa imeanza kutoa huduma za Utawala, huduma za uzazi wa mpango, huduma za waviu kwa wajawazito, huduma za ustawi wa jamii, huduma za lishe pamoja na huduma ya uhifadhi wa dawa.

Naye Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa Mkoa wa Mbeya Ndg. Said Bungala amesema kwamba wamejenga nyumba hizo ikiwa kutekeleza wajibu wao ili kuhakikisha wananchi wanapata nyumba za makazi na biashara na katika eneo la igawa wamefanikiwa kujenga nyumba 20 ambapo nyumba moja imeghalimu shilingi milioni 49.5.

Aliongeza kuwa Nyumba walizozikabidhi kwa ni kwa ajili ya makazi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na zilianza kujengwa tangu 2015 na hadi kufikia sasa zimekamilika na zipo tayari kwa ajili ya matumizi.

Halmashauri imetenga nyumba 12 kwa ajili ya matumizi ya watumishi wa idara ya Afya na nyumba 8 zinazobaki zitagawanywa kwa watumishi wa idara nyingine.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.