• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mkuu wa Wilaya Awataka Wananchi Kupanda Mikorosho ili Kujiongezea Kipato

Tarehe ya Kuanza: February 8th, 2018

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mh. Reuben Mfune amewataka wananchi wa Wilayani Mbarali kupanda miche ya zao la Korosho kwenye mashamba makubwa pamoja na majumbani ili kujiongezea kipato pamoja na kuboresha afya.

Ameyasema hayo siku ya uzinduzi wa upandaji wa miche ya zao la Korosho Kiwilaya liliyofanyika katika Kata ya Mawindi Kijiji cha Manienga siku ya jumanne ya tarehe 06/02/2018

Mh. Mfune alisema kuwa, Watafiti kutoka kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele waliona hali ya hewa ya Wilaya ya Mbarali inafaa kwa upandaji wa zao la Korosho na waliahidi kushirikiana na wananchi wa Wilaya ya Mbarali kuanzisha kilimo cha zao la hilo na kuleta vilaba pamoja na vifaa kwa ajili ya kuotesha miche 21,000 na hadi sasa Wilaya imefanikiwa kuotesha miche ya Korosho 17,000 ambayo ni sawa na asilimia 81.

“Katika Wilaya yetu kila mtu anafikilia sehemu ambazo maji yanaingia kwa ajili ya kuotesha mpunga, katika maeneo ambayo hatuwezi kuotesha mpunga ndio sehemu sahihi ambayo tunaweza kuotesha korosho, kwa mwaka huu tunategemea kuotesha miche kwenye hekta 240. Nawasihi wananchi wa Wilaya ya Mbarali, tusitegemee zao la punga peke yake, tuwe za zao la biashara la mpunga lakini pia tuwe na zao korosho,” alisema

Mh. Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa Kilimo cha Korosho kina faida nyingi zikiwemo, kutupatia Korosho ambazo kwa sasa kilo moja inauzwa tsh. 4,000, inatunza vizuri moyo, ina madini ambayo yanaimarisha mifupa, kupunguza uzito, inatupatia matunda aina ya mabibo ambayo yanaweza kuliwa kawaida au kutengenezea kinywaji aina ya mvinyo au wine, kuongeza kipato, kutupatia mti wa kivuli, na ni rahisi kuutunza.

Naye Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Dickson Kamwela kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji aliongeza kuwa, Wilaya ya Mbarali katika msimu wa kilimo 2017/2018 imekusudia kuanzisha kilimo cha zao la korosho ili kuboresha maisha ya wananchi kwa lengo la kujiongezea kipato. Kilimo cha korosho kinaendeshwa kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti wa Kilimo Naliendele Mtwara na Bodi ya korosho Tanzania.

“Katika msimu huu wa kilimo, Wilaya kwa kushirikiana na watafiti wa kilimo Naliendele na Bodi ya korosho imeanzisha vitalu vya korosho katika kata za Madibira, Rujewa, Mapogoro na Chimala vyenye jumla ya miche 17,019, vitalu hivyo vinasimamiwa na kutunzwa na vikundi/taasisi na watu binafsi.” Alisema

Baadhi Wananchi wa Kata ya Mawindi waliohudhuria uzinduzi huo, walimpongeza Mh. Mkuu wa Wilaya na Wataalam wake kwa jitihada walizozichukua kuhakikisha kilimo cha Korosho kinafanikiwa wilayani Mbarali, kwani kuna sehemu nyingi wilayani hapa zao la mpunga halikubali, ujio wa zao la korosho litakuwa mkombozi mkubwa kwao kwani litaongeza kipato cha mtu mmoja mmoja.

Zao la Korosho linachukua miaka minne kukua na kuvuna mvuno wa kwanza. Tafiti zinaonyesha kuwa mvuno wa kwana unatoa kilo 0.5 na utakapotimiza miaka 10 unaweza kutoa kilo 25 kwa mti mmoja.

Ekali moja ya zao la korosho linaweza kupandwa miche 69 ambayo kwa muda wa miaka 10 inauwezo wa kuzaa kilo 1,725 ambayo kwa bei ya sasa ya sokoni inaweza kumuingiza mkulima kiasi cha tsh 6,900,000.

Zao la korosho halizuii kupanda Mazao mengine madogo magodo kama mikunde, mahindi na karanga kipindi mti unaendelea kukua

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.