• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mtega Amaliza Mgogoro wa Diwani na Wenyeviti Mbarali.

Tarehe ya Kuanza: July 6th, 2019

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mhe. Francis Mtega (Diwani), amemaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya Diwani wa Kata ya Madibira Mhe. Erick M. Ngelyama  (CHADEMA) na wenyeviti 7 wa vijiji vya kata hiyo (CCM) kupitia kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC) kilichofanyika siku ya tarehe 05/07/2019 kwenye ukumbi wa ofisi ya kata.

Wenyeviti hao wa Vijiji saba walikuwa wanamtuhumu Diwani wa kata yao kutumia lugha ya kuwadhihaki kwenye mikutano ya hadhara aliyoifanya katika vijiji vyao kitu ambacho kilipelekea wenyeviti hao kuamua kuacha kufanya kazi na Diwani huyo.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mtega alisema kuwa, Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali limemtuma kwenda kujua ni kwanini vikao vya kisheria vya Maendeleo ya Kata (WDC) havifanyiki katika kata ya Madibira kwani ni kwa kipindi kirefu sasa Baraza halijapokea taarifa ya Maendeleo ya Kata.

“Kama vikao vya kisheria havifanyiki, ni athari kwa maendeleo ya kata pamoja na Taifa kwa ujumla. Kukosea kwa binadamu ni kawaida, ila sifa kubwa ya kiongozi ni kutambua unayoyafanya kama ni mazuri au ni mabaya, vilevile unavyokumbushwa na wenzio ni vyema kuyatafakari, kuyakubali na kuyafanyia maamuzi.”

“Leo iwe mwanzo mpya kwa siku zinazoendelea, migogoro haina faida zaidi ya kuchafua sifa ya kata yetu ya Madibira, Halmashauri na Mkoa wetu wa mbeya.”

“Binadamu wote tuna mapungufu, kikubwa ni kuvumiliana, sitarajii kusikia kitu kama hiki kinajirudia, natarajia tuliyoafikiana hapa yatafanyiwa kazi na sisi tunasubili matokeo.” Alisema

Diwani wa Kata ya Madibira Mhe. Erick M.  Ngelyama alikili kosa la kutumia lugha isiyofaa kwa Wenyeviti wake wa vijiji kupitia mikutano ya hadhara na kuomba asamehewe kwa maneno aliyoyatoa ambayo yaliwagawa katika safu yao ya uongozi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma Msangi amewaomba wenyeviti wote wa vijiji kutoa ushirikiano kwani ni vigumu kufanya kazi kama unakinzana na wenzio.

Amewashukuru wenyeviti hao kwa kukubali kusamehe kwani migogoro haitatuliwi na watu wa nje, inatatuliwa na wao wenywewe, uongozi wa wilaya unasimama kama refa kwa ajili ya kuwaongoza.

Kikao cha kutatua Mgogoro kati ya Diwani wa kata hiyo pamoja na Wenyeviti wa Vijiji Kiliwahusisha Viongozi Kutoka ngazi ya Halmashauri ambao ni Mwenyekiti wa Halamshauri Mhe. Francis Mtega, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashari Kivuma Msangi, Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Aswege Kaminyoge na Afisa Habari Daudi Nyingo.

Wengine ni Kamati ya Maendeleo ya Kata (WDC), Viongozi wa CCM na Chadema ngazi ya Kata, Viongozi wa Dini, Wazee Maarufu pamoja na wataalamu ngazi ya kata.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.