• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Naibu wa Waziri Apongeza Utoaji Mikopo ya Vikundi vya Wanawake

Tarehe ya Kuanza: March 8th, 2018

Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Dr. Mary Mwanjelwa, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwa kuweza kutoa mikopo kwa vikundi vya Wanawake wa Wilaya ya Mbarali kwa asilimia 100 na ametoa wito kwa Halmashauri zingine zilizopo hapa Tanzania kuiga mfano wa Halmashauri ya Mbarali.

Mhe. Mwanjelwa ameyasema hayo alipokuwa Mgeni Rasmi kwenye maadhimisho ya Kilele cha siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa Kiwilaya katika kata ya Rujewa kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi Ibara siku ya tarehe 08/03/2018 Wilayani Mbarali

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imefanikiwa kutoa kiasi cha fedha tsh 191,700,000/= kwa mwaka wa fedha 2016/2017 na 2017/2018 kwa vikundi vya Wanawake 45.

Mhe. Naibu Waziri ameviomba vikundi vya wanawake wote waliopata mikopo katika Wilaya ya Mbarali, kuitumia mikopo hiyo kwa umakini na kufanya marejesho ili kuviwezesha vikundi vingine vya wananwake waweze kunufaika na mikopo hiyo.

Katina hotuba yake, Mhe. Mwanjelwa amezishukuru taasisi zote za kifedha zinazotoa mikopo kwa jamii hasa wanawake ila ameziomba taasisi hizo kupunguza riba pamoja na masharti magumu wanapotoa mikopo yao ili watanzania wengi waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na taasisi na taasisi zao.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune akizungumza katika maadhimisho hayo, amemshukuru Mhe naibu waziri kwa kuja kujumika na wananchi wa Wilaya ya Mbarali kwenye kilele cha shughuli hii muhimu ya kijamii, na ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kwa kuweza kutoa fedha za mfuko wa wanawake na vijana kwa asilimia 100 kwa miaka mitatu mfululizo, kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa miaka ya nyuma.

Wakizungumza katika risala, kwa umoja wao wanawake wa Wilaya ya Mbarali wamemuomba Mhe Naibu Waziri na uongozi Wilaya ya Mbarali kwa ujumla kuwapa uwakilishi mkubwa katika vikao vya maamuzi, na wameziomba taasisi za fedha kutoa mikopo yenye riba nafuu.

Wamewaasa wanawake wenzao kujiunga na Vikundi mbalimbali vya akina mama ili waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali vilevile wameiomba Serikali kujenga Zahanati kwa kila Kijiji pamoja na Vituo vya Afya kwa kila Kata sambamba na kuboresha huduma za uzazi ili kutokomeza vifo vya mama na mtoto.

Kauli mbiu ya siku ya Wanawake duniani mwaka 2018 ni “kuelekea Uchumi wa viwanda, tuimalishe usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake Vijijini”

Katika maadhimisho hayo, Mhe Naibu Waziri aliweza kutembelea mabanda mbalimbali yaliyokuwa yanaonyesha shuguli za Uchumi za kijasiliamali zinazofanya na Vikundi vya wanawake wa Wilaya ya Mbarali mabanda ya taasisi za kifedha pamoja na banda la damu salama.

Sherehe hizo zilishereheshwa na burudani mbalimbali, zikiwemo ngoma za asili, shairi, kwaya pamoja na mchezo wa kukimbiza kuku.

Daudi B. Nyingo
Afisa Habari na Mahusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
March 8, 2018

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.