• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TASAF SASA KUTUMIA MFUMO WA KIELECTRONIC KULIPA KAYA MASIKINI

Tarehe ya Kuanza: July 10th, 2020

Hayo yamesemwa na Meneja Miradi ambaye ni Kiongozi wa Timu ya Taifa kwa ajili ya kazi ya Uhakiki wa kaya kutoka TASAF Makao Makuu Ndg Shabani Abdumalick alipokuwa akiendesha kikao kazi kwa Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na mafunzo ya kuwajengea uwezo wawezeshaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali kuhusu utekelezaji wa kipindi cha pili awamu ya tatu ya Tasaf  na  zoezi la uhakiki wa walengwa wa kaya masikini siku ya terehe 09/07/2020.

Ndg. Shabani alisema kuwa malipo yote kwa sasa yanatarajiwa kulipwa kwa kutumia mfumo wa Kielectronic kwa wanufaika watakuwa wanapokea malipo yao kwa kutumia simu zao, kwa njia ya mawakala au dawati la Bank kwa lengo la kupunguza gharama za usafiri pamoja na changamoto zilizojitokeza katika awamu iliyopita.

 

“Zoezi la sasa linatarajiwa kufanyika kwa njia ya mfumo wa kielectronic, na baadae tutaacha kutumia magari kupeleka pesa vijijini, mlengwa atatakiwa kuleta namba ya simu iliyosajiliwa na kwa ambao hawatakuwa na simu tutawawekea utarabu unaofaa. Tunanza uhakiki kwa kutumia vishikwambi (Tablet) ambazo zitakuwa zikitumika kubeba dodoso fupi litakalofanya kazi ya uhakiki wa taarifa.

 

“kinachofanyika kwa sasa ni uhakiki ili kusafisha daftari libaki na kaya ambazo zina sifa za kuendelea kuwa kaya masikini ili ziweze kuendelea kupata rudhuku ya Serikali kutoka TASAF. Tunahakiki kaya zote zilizo kwenye mpango wa TASAF kwa nchi nzima na katika zoezi hili hakutaongeza kaya mpya, kaya ambazo hazitafika kufanyiwa uhakiki, hazitalipwa” Alisema Ndg Shabani

Akisoma taarifa wakati wa ufunguzi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Taifa Ndg. Ladislaus Mwamanga, Bwana. Shabani alisema kuwa utekelezaji wa kipindi cha kwanza cha TASAF awamu ya tatu umechangia kwa kiasi kikubwa azma ya Serikali kupunguza umaskini nchini kwani mahitaji ya msingi kwa Kaya yamepungua kwa asilimia 10 na umasikini uliokithiri umepungua kwa asilimia 12.

Aliongeza kuwa baada ya kukamilisha kipindi cha kwanza cha awamu ya tatu ya TASAF Serikali iliamua kuendelea  na kipindi cha pili ili kaya zote zinazoishi katika mazingira duni zipate usaidizi kwa kuwawezesha kufanya kazi na kupambana na umasikini.

 

“Kipindi hiki kitazifikia ya kaya 1,450,000 zenye jumla ya watu zaidi ya milioni 7 kote nchini ikiwa ni nyongeza ya kaya zaidi ya 350,000. Kutakuwa na miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwemo miradi ya Elimu, Afya na Maji”

 

“Itatengenezwa miradi ambayo itawalazimu walengwa waweze kufanya kazi ili waweze kupata kipato. Miradi hiyo itakuwa inatoa ajira za muda lengo likiwa mtu apate sababu ya kulipwa kwa kufanya kazi” alisema kwa Niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Aswege Kaminyoge, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha Tasaf awamu ya 3 kwani itaziwezesha kaya nyingi kufanya kazi kwenye miradi itakayoibuliwa na kuweza kujipatia kipato, na kwa niaba ya Halmashauri wapo tayari kutekeleza miaradi yote itakayoletwa kwa asilimia 100.

Akiongezea mratibu wa Tasaf Wilaya ya Mbarali Ndg. Zabron Abel alisema kuwa, kwa kupitia mafunzo yaliyotolewa kwa mfumo wa kielectronic kwa wawezeshaji ngazi ya Wilaya wanatarajia watapita katika vijiji 75 vilivyopo kwenye mpango kuzihakiki kaya 10,317 kwa lengo la kuwa na data safi za walengwa, na ili waweze kuhakikiwa watalazimika kuja na kitambulisho cha Mpango, daftali la mototo kwa wale ambao wanasoma, namba ya simu, pamoja na namba ya Nida au kitambulisho cha mpiga kura.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wawezeshaji kwa njia ya mfumo kwenye mafunzo hayo, Bi. Helen Ngowo na Bwana. Edwin Mgendwa wameishukuru Serikali kwa kuleta TASAF awamu ya 3 sehemu 2 kwani awamu hii inatumia zaidi mfumo kwa kutumia Vishikwambi (Tablet) ambazo zitawasaidia kupata kaya zenye sifa zitakazostahili kuwepo kwenye mpango na itawezesha kuondoa walengwa hewa.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.