• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Tuzo ya Tanapa ya Uhifadhi wa Mazingira

Tarehe ya Kuanza: November 24th, 2017

Wakazi Wilayani Mbarali wamelipongeza Shirika la Hifadhi za Taifa Tanapa kwa kuanzisha Tuzo ya Tanapa ya Uhifadhi wa Mazingira na hasa katika kipindi hiki ambacho changamoto ya uharibifu wa mazingira imekua ikiongezeka kwa kasi katika maeneo tofauti Nchini.

Zaidi ya watu 200 kutoka katika kata kumi wamepata semina ya uhifadhi wa mazingira Wilayani Mbarali ikiwa ni pamoja na Jumuia za Watumia Maji, Viongozi wa Serikali za Vijiji na Kata, Taasisi kama shule, na wananchi kwa ujumla.

Wakizungumza katika Mikutano ya Hadhara ya uhamasishaji wa ushiriki wa Tuzo ya TANAPA ya Uhifadhi wa  Mazingira iliyomalizika mwanzoni mwa wiki wilayani Mbarali walisema, Tuzo ya Tanapa ya Uhifadhi wa Mazingira imeleta tija katika uhifadhi wa mazingira kwani jamii sasa imeanza kutambua umuhimu wa kushiriki katika  shughuri za uhifadhi wa mazingira kwa maendeleo endelevu

Sanjari na hilo pia wamelalamikia vitendo vya unyanyasaji vinavyofanywa na baadhi ya askari wa wanyamapori ambavyo kwa kiasi kikubwa vimesababisha jamii kuwa na mtazamo hasi dhidi ya shirika la hifadhi za taifa TANAPA.

Juma Mwankani Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Ihahi amekili kuwa kabla ya semina iliyotolewa na muhifadhi wa Ruaha ndugu Sharifu Abdul walikuwa wakiamini kuwa TANAPA ni adui na haina faida yoyote kwa jamii. Aidha amelitaka Shirika la TANAPA kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu sheria mbalimbali za uhifadhi ili kupunguza ujangili na kulinda jamii kutokana na makosa wanayafanya kutokana na kutokujua sheria.

“leo katika hii semina nimejifunza mambo mengi ikiwa ni pamoja utunzaji wa vyanzo vya maji na misitu kwa ajili ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia Nchi ni somo zuri na niahidi tu kuwa nitafikisha ujumbe kwa wananchi ili tuweze kutekeleza hilo, lakini kubwa ni maelezo mazuri yaliyotolewa na muhifadhi wa TANAPA kuhusiana na shughuri zinazofanywa na Shirika la TANAPA na namna ambavyo wanaweza kusaidia miradi ya maendeleo kwa jamii kama vile Ujenzi wa shule, Visima vya maji, Hospitali na Maabara” alisema Mwankani.

Gerominasi Gisamo Mkuu wa Shule ya Sekondari Igumbilo  alisema Tuzo ya TANAPA ya Uhifadhi wa Mazingira imehamasisha kwa kiasi kikubwa jamii kushiriki katika uhifadhi wa mazingira lakini pia ameshauri waendelee kutoa elimu ya uhifadhi kwa jamii nzima ili kupata wadau wengi wa uhifadhi kwa maendeleo ya Wilaya ya Mbarali na Taifa kwa ujumla.

“katika semina hii nilichojifinza upo umuhimu wa kuwafundisha watoto umuhimu wa mazingira kwani wao ni mabalozi wazuri katika jamii zinazowazunguka lakini pia kwakufanya hivi tunazalisha kizazi kitakachokuwa na ufahamu wa masuala ya mazingira” alisema  Gisamo.

Kelvin Edisoni Luvanda mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mengele alisema Tuzo ya TANAPA ya Uhifadhi wa Mazingira inatoa hamasa kwa jamii kuongeza juhudi katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na hasa pale wanapopata tuzo jambo ambalo linasaidia kulinda mazingira ya maeneo yanayowazunguka.

Diwani wa Kata ya Igurusi Bi. Kihwele alisema “maisha ya watu yanategemea mazingira, Tuzo ya TANAPA ya uhifadhi wa Mazingira imeanzishwa wakati sahihi wakati ambao jamii ilikuwa ikihitaji elimu zaidi ya uhifadhi wa mazingira kutokana na kuongeza kwa changamoto ya ukosefu wa mvua za kutosha iliyosababishwa kwa kiasi kikubwa na ukataji hovyo wa miti na uharibifu wa vyanzo vya maji, ifike hatua sasa tuondoe ile dhana ya panda miti kata mti na badala yake iwe panda miti kwenye maeneo yaliyo wazi kwa maendeleo ya vizazi vijavyo”.

Tuzo ya TANAPA ya Uhifadhi wa Mazingira ilianzishwa mwaka wa fedha 2015/2016 lengo kuu ikiwa ni kushirikisha jamii ya nyanda za juu kusini na hasa katika mikoa ya Mbeya, Iringa na Njombe katika masuala ya uhifadhi wa mazingira na wanyama pori ambapo jumla ya Wilaya tano zinashiriki katika tuzo hiyo.Wilaya ya kilolo, Mufindi, Wanging’ombe, Makete na Mbarali.

Tuzo ya TANAPA ya Uhifadhi wa Mazingira ni endelevu na hutolewa katika Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani ambazo huanzimishwa tarehe 5 Juni kila mwaka kwa washindi watatu kutoka kila Wilaya. Makundi yanayoshindaniwa ni pamoja na Uhifadhi wa vyanzo vya maji, Uhifadhi wa misitu ya asili na Upandaji miti ya asili, Uhamasishaji, Uhifadhi wa maeneo yaliyoharibiwa na Uhifadhi wa Wanyama Pori.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.