• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Ufafanuzi Kuhusiana na Kubomolewa Mabanio, Kufukiwa Mifereji na Kuwekwa Mipaka Katika Shamba la Mbarali Estate

Tarehe ya Kuanza: December 15th, 2017


Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune, ametolea ufafanuzi kuhusu malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya Wananchi pamoja na Vyombo vya Habari kuhusiana na zoezi linaloendelea la Kubomolewa kwa Mabanio ya maji, kufukiwa kwa Mireji pamoja na kuwekwa mipaka kwenye eneo la shamba la mwekezaji la Mbarali Estate linalopakana na Kata tatu za Wilaya ya Mbarali ambazo ni Ubaruku, Rujewa pamoja na Imalilo Songwe siku ya Alhamisi ya tarehe 14/12/2017 alipoitisha Kikao na waandishi wa Habari Ofisini kwake.

Mhe Mfune alisema kuwa, zoezi hilo linalenga kubomoa Mabanio ambayo yamejengwa bila kufuata utaratibu, kufukia mifereji ambayo haina kibali na kufunga matoleo ya maji yanayotoka kwenye mashamba makubwa ambayo yalikuwa yanatumika kimazoea na hayakufuata Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji  namba 11 ya mwaka 2009, Sheria ya  Usimazi wa Mazingira namba 20  ya mwaka 2004 pamoja na Sheria ya Misitu namba 14 ya mwaka 2002.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Wilaya alisema, Mashamba makubwa ya Kapunga na Mbarali Estate ambayo yamezuia maji ya matoleo kwenda kwenye mashamba mbalimbali, wamefanya hivyo kwa mujibu wa sheria, na hawajafanya kwa maamuzi yao binafsi kwani wao wamefuata maelekezo yanayotaka maji yote yaliyotumika kwenye mashamba, yarudi mtoni, na kuendelea na matumizi mengine kama Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kilimo pamoja na uzalishaji wa Umeme katika bwawa la Mtera na Kidatu.

Aliongeza kuwa, Kilitumwa kikosi kazi na Mhe Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi wa April na May 2017, pia Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya aliunda kikosi kazi mwezi wa February mwaka huu kwa ajili ya kuokoa ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu.

Vikosi kazi hivyo vilifanya uchunguzi wa kina katika maeneo mbalimbali kuangalia kitu gani kinasababisha maji kutoendelea na safari kwenye Mto Ruaha Mkuu kwa ajili ya matumizi mbalimbali, kwani maji hayo yameanzia Mkoa wa Njombe Wilaya ya Wanging’ombe na Makete, na  yanapita Wilayani ya Mbarali kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwemo kilimo na  matumizi ya wanyama kwenye Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Baada ya hapo yanakwenda kwenye bwawa la mtera kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, yanatumika katika kilimo bonde la Ruaha Mbuyuni, yanakwenda Kidatu kwa ajili ya uzalishaji wa umeme, yanateremka Rufiji kwa ajili ya matumizi mbalimbali na mwisho yanaelekea Baharini.

Mhe Mfune alieleza kuwa, Mhe Makamu wa Rais alitoa maagizo 18 ili yaweze kutekelezwa kwa kipindi hiki kwa ajili ya kuokoa ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu. Katika mapendekezo hayo, Wilaya ya Mbarali imeagizwa kutekeleza mapendekezo kumi (10) ambayo ni:

  • Kuainisha vyanzo vya maji, kuviwekea mipaka na kuvilinda kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo,
  • Kuwaondoa watu wote waliovamia maeneo ya hifadhi,
  • Kubainisha na kuondoa miti yote isiyo rafiki na maji na kupanda miti yote iliyo rafiki na maji,
  • Kufanya uhakiki wa haki miliki zote zilizotolewa katika maeneo oevu na kuzibatilisha,
  • Usitishwaji wa shughuli zote za kibinadamu zinazofanyika ndani ya mita 60 kutoka kwenye kingo za mito na vyanzo vya maji,
  • Kuhakikisha kuna ujenzi wa mabanio imara ya kudhibiti maji na kuweza kupima maji yanayopita kwenye mifereji na matoleo ya maji,
  • Kuhakikisha kilimo hifadhi katika bonde la Mto Ruaha ili kuongeza tija katika matumizi ya maji na Ardhi
  • Kuhakikisha kunafanyika usafi na usakafiaji wa mifereji mikuu, midogo na kati katika miradi yote ya umwagiliaji
  • Kusimamia utekelezaji wa sheria ya mazingira kwa kutoza adhabu (fine) kwa waharifu wote wa maji ili kuwa funzo na kuondoa utumiaji mbovu wa maji katika maeneo mbalimbali
  • Kuwezesha uandaaji na utekelezaji wa usimamizi wa mpango wa matumizi bora ya Ardhi

Wilaya ya Mbarali pia inasimamia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa kutoka kwenye Wizara mbalimbali

Aliongeza kuwa mnamo tarehe 07/12/2017 na 10/12/2017 Kazi  ilianza kutekelezwa, na imeelekezwa kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji na inatekelezwa na ofisi ya Bonde la Rufiji. Utekelezaji umeendelea kwa kubomoa banio lilillopo katika shamba la Kapunga, tarehe 10/12/2017 lilibomolewa banio la Mto Mbarali eneo la Mnazi na kurekebisha mto katika Banio la Itamba ambapo eneo hilo maji mengi yalikuwa yanapotea katika eneo ambalo halistahili.

Mhe Mkuu wa Wilaya amewaomba wananchi pale wanapoona kuwa Serikali inatekeleza jukumu ambalo linalenga kuokoa Ikolojia, waone kwamba inafanya kazi hii kwa maslahi mapana ya Nchi, na sio kwa maslahi ya mtu mmoja mmoja, watu wasione kwamba Mbarali peke yao ndio wanaostahili kutumia maji haya, na kuona wengine hawastahili.

“Sisi ni mapito ya maji kutoka kwenye vyanzo vya maji kuelekea maeneo mengine, kwa hiyo tufuate sheria na taratibu kama tunavyoelekezwa, Serikali haina lengo la kuwakomoa wananchi lakini ina lengo la kurekebisha mambo mengi ambayo yalikuwa yanafanyika kwa mazoea yafuate sheria ili watu wote waweze kufaidi  kwa maslahi mapana ya Nchi yetu” alisema

Mhe Mfune amewasihi baadhi ya wakulima kuangalia mazao mbadala ya kulima, wasiangalie tu zao la Mpunga kwani kuna baadhi ya maeneo ambayo tumekuwa tukiyalazimisha maji yaweze kufika lakini yanaweza kutumika kulima mazao mengine kama Korosho na Mihogo.

Aliongeza kuwa, mwaka huu Wilaya ya Mbarali imeotesha miche ya Korosho 21,000 na inapatikana katika maeneo ya Jeshi la Magereza ikiwa kama zao mbadala kwa kushilikiana na kituo cha utafiti wa Kilimo Naliendele, ambao walifanya utafiti na wamebaini kuwa Ardhi ya Mbarali inafaa kuotesha zao hilo.

Kuhusu Mihogo alisema kuwa, tumetangaziwa fulsa kupitia TPSF kwamba Nchi ya China wanahitaji sana Mihogo. Mihogo kutoka Wilaya ya Mbarali ndio zao linalolisha eneo kubwa la Mkoa wa Mbeya hasa Jiji la Mbeya.

“Ukomo wa Ardhi ya kilimo katika Wilaya ya Mbarali umefika mwisho, tukiendelea kupanua mashamba ya Mpunga inamaana maji yote yataishia Wilaya ya Mbarali, hiyo ndio sababu kubwa hatuwezi kuendelea kupanua mashamba hata kama hali ya hewa inaruhusu kilimo cha mpunga kuendelea, maji yatumike kwa maslahi mapana ya nchi kwa sababu tunaotakiwa kutumia sio Mbarali peke yetu”alisema

Kuhusu suala mpaka wa shamba la Mpunga la Mbarali Estate, alisema kuwa, mwekezaji alikabadhiwa shamba hilo mwaka 2006, baada ya kukabidhiwa na kutambua mipaka ikagundulika kuwa baadhi ya maeneo yanakaliwa na watu na yanatumika kwa ajili ya kilimo.

Kati ya mwaka 2012 hadi 2014 vikao mbalimbali katika Vijiji 12 ambavyo vipo katika kata tatu za Rujewa, Ubaruku na Imalilo songwe, zinazopakana na shamba hilo, viliitsha vikao vya kisheria vikisimamiwa na Wilaya ili kuangalia mustakabali na kufahamu maeneo yanayokaliwa na wananchi pamoja na mashamba kwa ajili ya kupunguzwa katika hati ya mwekezaji ambayo alikabidhiwa na Serikali.

Mwaka 2014 Vijiji 11 vilifikia makubaliano ya kitu gani kifanyke katika maeneo yao, isipokuwa Kijiji cha Nyelegete hawakufikia makubaliano.  Makubaliano katika kijiji hicho yalifanyika mwaka 2017 kupitia kamati ya huduma za Jamii Ujenzi na Mazingira baada ya kukutana na wananchi na kuridhiwa na kikao cha Baraza la Madiwani.

Jumla ya hekta 548 sawa na ekari 1,354.13 zimeondolewa kwenye shamba la Mwekezaji la Mbarali Estate kwa ajili ya kupisha shughuli za maendeleo ya wananchi ziweze kufanyika, na Mwekezaji amebakiwa na hekta 5,481.99 kati ya hekta 6,060 alizokabidhiwa awali.

Serikali imeweka mipaka ya kudumu kati ya Vijiji 12 na shamba la Mbarali Estate kwa kuondoa maeneo ambayo yalikuwa yanayalipiwa na Mwekezaji lakini yalikuwa yanatumiwa na wakazi wa maeneo ya Vijiji hivyo.

Ikumbukwe kuwa Mwekezaji hajajiongezea maeneo, ila amepunguza ukubwa wa eneo la shamba alilokuwa anamiliki ili wananchi waendelee kutumia katika maeneo yanayozunguka shamba.

Mhe. Mfune alihitimisha kwa kuwasihi wana Mbarali kutafuta ukweli wa mambo ambayo hawayaelewi kutoka kwenye ofisi yake, ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali au kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya badala ya kudanganywa na wapotoshaji wachache wasioitakia memaWilaya ya Mbarali.

“Watu wachache wamekuwa wakiwachangisha wananchi fedha nyingi bila kibali na kuwapotosha kwamba wanaenda kushughulikia mambo mbalimbali lakini hawana uwezo huo na wamekuwa wakiwatapeli” alisema

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.