• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

VIJIJI 102 KUWAKA UMEME IFIKAPO AGOSTI 2019 MBARALI

Tarehe ya Kuanza: April 22nd, 2018

Waziri wa Nishati Mhe. Medard Kalemani amevihakikishia vijiji vyote 102 vilivyopo Wilaya ya Mbarali kufikiwa na huduma ya umeme ifikapo august 2019.

Mhe. Waziri ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Igurusi siku ya jumamosi ya tarehe 21/04/2018 alipofanya ziara wilayani hapa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi pamoja na kuzindua Upanuzi wa Huduma za Umeme Vijijini.

“haya yote ni maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Magufuli katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi” alisema.

Akizunguzmza katika ziara hiyo Mhe. Kalemani alisema kuwa, Wilaya ya Mbarali ina Jumla ya vijiji 102, kati ya vijiji hivyo, vijiji 68 vimeunganishiwa umeme mwaka 2017 na vikaongezwa vingine 18 kufikisha Jumla ya vijiji 86 kwenye mradi wa Rea Awamu ya Pili. Kwa vijiji 16 vilivyobaki vitapatiwa umeme kwenye mradi unaotekelezwa kwa sasa Rea Awamu ya Tatu ambapo tayari Mkandarasi yupo kazini.

Vilevile Mhe. Waziri ametoa muda wa siku 10 kwa wananchi 330 ambao hawakuunganishiwa umeme katika mradi wa Rea Awamu ya Pili kuunganishwa mara moja vinginevyo Mhe. Mkuu wa Wilaya awachukulie hatua wote watakaokwamisha agizo hilo.

“Serikali imegharamia huu mradi kwa asilimia 100, mwananchi atalazimika kuchangia kiasi cha shilingi 27,000 tu, isitokee mtu akawalaghai mkatoa pesa zaidi ya hiyo, na kama kuna mwananchi ana nyumba ya nyasi, hiyo ndio ninataka ianze sasa” alisema.

Meneja wa TANESCO Wilaya ya Mbarali Ramadhani Mwanga katika taarifa yake alieleza kuwa, Mradi wa Rea Awamu ya Pili ambao umetekelezwa na Mkandarasi M/s JV State Grid Electronical ulihusisha ujenzi wa njia kubwa ya msongo wa KV33 yenye urefu wa Km 357.29 pamoja na msongo mdogo wa 0.4KV yenye urefu wa Km 144.29 ikihusisha na usimikwaji wa Mashine Umba (Transfomer) 89 na jumla ya wateja 6,449 kwa vijiji 68 wameunganishiwa katika awamu hii na mkandarasi anaendelea kuwaunganishia wateja 330 waliobaki.

Kwa mradi wa Rea Awamu ya Tatu unaotekelezwa na Mkandarasi Steg International Services, Mwanga alisema kuwa jumla ya vijiji 18 vimeshafikiwa na umeme kwani upimaji na usanifu umekamilika na wamefanikiwa kuwatambua wateja 1,507 ambao wapo ndani ya mita 30 na kwa sasa zoezi la kuunganisha umeme linaendelea na hadi kufikia tarehe 31/03/2018 wateja 472 wameunganishiwa kati yao 9 ni wa viwanda vidogo vidogo.

Aliongeza kuwa kwa Mradi wa Rea Awamu ya Tatu itaongeza vijiji 16 vilivyobaki kukamilisha idadi ya vijiji 102 vilivyopo Wilaya ya Mbarali kunufuika na huduma ya umeme na tayari Mkandarasi ameshaanza kusimamisha nguzo katika mtaa wa Mlimani ulipo katika kata ya Rujewa karibu na eneo la mnadani.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune aliongeza kuwa asilimia 83 ya wananchi wa Mbarali wanategemea Kilimo, umeme kwa Mbarali ni muhimu sana kuchochea Maendeleo kwani mara baada ya Kilimo Mazao yote yanachakatwa kwa njia ya umeme, vilevile amemshukuru Mhe. Waziri kwa Kufanya ziara katika Wilaya ya Mbarali kwani amejibu kero zote zinazowatatiza wananchi wa Mbarali.

Diwani wa Kata ya Igurusi Mhe. Hawa Kiwhele akizungumza kwa niaba ya wananchi, amemshukuru Mhe. Waziri kwa ujio wake, kwani ametatua kero kubwa ya umeme inayowasumbua wananchi wake wa Kata ya Igurusi na Wilaya ya Mbarali kwa ujumla.



Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.