• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Wafugaji Wapata Suluhu ya Muda Mgogoro wa Mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha

Tarehe ya Kuanza: April 10th, 2019

Wafugaji wa Wilaya ya Mbarali wamepata suluhu ya muda kuhusiana na malalamiko yaliyotolewa na wafugaji dhidi ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha (RUNAPA) kukamata mifugo yao na kulipishwa faini ya shilingi laki moja (100,000) kwa kila mfugo katika maeneo ambayo wafugaji wanayodaiwa kuwa sio ya Hifadhi.

Kutokana na malalamiko hayo Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Mhe. Reuben Mfune aliamua kufanya ziara kuanzia tarehe 03/04/2019 na kumalizika 08/04/2019 ya kupita maeneo yote ambayo yamekumbwa  na changamoto hizo na kuzipatia suluhu ya muda mfupi huku tukiwa tunasubiri mchakato wa upatikanaji wa suluhu ya kudumu ambao upo katika hatua za mwisho za umaliziwaji wake.

“Nilichokifanya sio maamuzi ya mwisho, nimefanya ziara ili tuweze kuoneshana maeneo ya msingi ambayo yalikwishalipwa fidia na ambayo bado hayajalipwa ili wafugaji waweze kujua wanaishia wapi wanapokwenda kulisha mifugo yao,  tukisubili maelekezo ya mwisho ya mpaka wa kudumu.” 

“Tumeshaelekezana maeneo yote ya mpaka, na maeneo ambayo watu walishalipwa hairuhusiwi kuingiza mifugo, kwa wale watakaotaka kuturudisha nyuma tutawachukulia hatua kwa mujibu wa sheria, hifadhi ni mali ya wananchi wote.” Alisema Mfune

Mhe Mfune ametoa rai kwa wafugaji wote wa wilaya ya Mbarali kuto watuma watoto kwenda kuchunga mifugo, ila watumwe watu wazima wenye akili timamu ambao wanaifahamu mipaka ya muda ambayo wameoneshana na na akasisitiza kuwa isitokee mtu akaja kulalamika kama atawatumia watu ambao hawaifahamu mipaka hiyo.

Aliongeza kuwa Wafugaji na Askari wasiwe chanzo cha kuchochea rushwa na badala yake wawe mstari wa mbele kukemea rushwa, vilevile kwa wafugaji watakaokiuka maelekezo yaliyofanyika na kuingiza mifugo kwenye Hifadhi watatozwa faini isiyozidi kiasi cha shilingi laki moja (100,000) kwa kila ng’ombe kwa mujibu wa sheria zilizopo, faini zote zilipwe kwa njia ya Bank na sio kulipana mikononi.

Nae Kiongizi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Ndg. Agricola R. Lihiru amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kutatua changamoto hiyo kwani wafugaji wengi walikuwa wanahisi wanaonewa pindi inapokamatwa  mifugo ndani ya Hifadhi ya RUAHA.

Baadhi ya wafugaji waliweza kumshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufanya ziara katika maeneo yao na kupata suluhisho la muda, kwani kwa kipindi kirefu mifugo yao ilikuwa ikikamatwa kutokana na kutofahamu mipaka inapoishia.

Mara baada ya kumalizika ziara ya kwenda kutafuta suluhu ya muda, ilibainika kuwa tatizo kubwa lililokuwa linawakabili wafugaji sio kutofahamu mipaka ya Hifadhi bali ni Uhaba wa maji pamoja na malisho kwa ajili ya mifugo.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya aliongozana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Viongozi na Askali wa Runapa, Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Viongozi wa Wafugaji, Viongozi wa maeneo husika ambao walikutwa kwenye maeneo pamoja na wafugaji wa maeneo hayo.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • KIKAO CHA MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI NA WATUMISHI WOTE WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

    June 16, 2025
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI YAPATA HATI SAFI BAADA YA UKAGUZI WA CAG

    June 17, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA MAAFISA WATENDAJI WA HALMASHAURI BAADA YA KIKAO KAZI

    June 16, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.