• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

DC AZINDUA KUANZA KWA MASOMO KWA SHULE MPYA 6 MBARALI

Posted on: August 6th, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune amezindua kuanza masomo kwa shule mpya 6 za Sekondari zilizosajiliwa wilayani hapa ili wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza na walioanza  masomo kwenye shule za kata za jirani warudi kwenye shule za kwenye kata zao kuendelea na masomo.

Mhe. Mfune amefanya uzinduzi wa shule hizo alipofanya ziara ya kuweka mawe ya msingi pamoja na kuzitembelea shule hizo kuanzia tarehe 22/07/2020 hadi tarehe 30/07/2020 wilayani hapa. 

Akiwa katika uzinduzi huo Mhe Mfune amewataka wananchi kuendelea kuongeza majengo mengine muhumu ili shule hizo ziweze kukamilika kuanzia vyumba vya madarasa, maabara, vyoo pamoja na majengo ya utawala.

“Hatuwezi kujua mwaka kesho watafaulu wanafunzi wangapi, maoteo ya madarasa mmeshapewa, tuhakikishe malengo yetu ya kuongeza vyumba vya madarasa yanatimia, kwani tukifuata maelekezo tuliyopewa tutakuwa na vyumba vya kutosha, tufanye kazi kwa bidii sasa hivi ili baadae tupate ahueni.”

“Najua bado tuna changamoto kwani kuna vijiji bado vipo mbali na shule, ila tuamini kuwa tumepungaza umbali tofauti na ilivyokuwa awali, mtoto hawezi kuzaliwa siku hiyo hiyo na akaweza kufanya kila kitu, changamoto zinanendelea kuatuliwa, na nina imani ndani ya miaka miwili shule zetu zote zitasimama na zitakuwa bora zaidi.” Alisema Mhe. Mfune 

Mkuu wa Wilaya amewashukuru wananchi kwa kufanikisha ujenzi wa shule hizo kwani zimekuwa faida kwa watoto wetu kwani kwa sasa wanafunzi wanauwezo wa kuwahi kwenda shuleni na kurudi muda unaotakiwa.

Kwa upande wake Kaimu Afisa Elimu Sekondari Bi. Anna Shitindi alisema kwamba, kwa sasa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ina shule 24 za sekondari, kati ya shule hizo shule 16 ni kongwe, shule mbili zilianza kutoa elimu mwaka 2019 na shule mpya 6 zimeanza kutoa elimu mwaka huu 2020.

Bi. Shitindi aliongeza kuwa kuna shule mbili ambazo ni Luhanga Sekondari pamoja na Haroon sekondari zipo katika hatua ya kuridhisha na zinategemewa kupata usajiri pamoja na kuanza kutoa elimu mwaka 2021. Vilevile Halmashauri imefanikiwa kuanzisha shule mbili mpya za kidato cha tano na sita na kufanya kuwa na jumla ya shule nne.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria uzinduzi wa shule hizo, wameishukuru Serikali kwa kufanikisha kufunguliwa kwa shule hizo kwani kabla ya hapo watoto wao walikuwa wanasafiri umbali mrefu kutafuta elimu. Vilevile wamewashukuru wadau wote wa maendeleo walioshiriki na wanaoendelea kushiriki kuinua sekta ya elimu wilayani hapa.

Shule mpya sita zilizowekewa mawe ya msingi pamoja na kuzinduliwa uanzaji ni Shule ya Sekondari Nyamakuyu, Shule ya Sekondari Muwale, Shule ya Sekondari Itamboleo, Shule ya Sekondari Kapunga, Shule ya Sekondari Mkanyageni pamoja na Shule ya Sekondari Mwatenga.MWISHO

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.