• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Tuleteeni Changamoto Zenu Tuzitatue-Lubandamo

Posted on: May 2nd, 2021

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mhe. Twalib Lubandamo (Diwani) alipokuwa akiongea na watumishi wa Kata ya Imalilosongwe siku ya wafanyakazi Duniani ambapo kata hiyo iliandaa maadhimisho hayo kwa ajili ya kuwapongeza watumishi wote wa kata.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mhe. Twalib alisema kuwa Ofisi yake inafahamu ya kuwa kuna changamoto nyingi zinawakabili watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wapo tayari kuzipokea changamoto hizo na kuzitatua.

“Tunajua watumishi wetu mna changamoto nyingi, tunaomba mtuletee hizo changamoto zenu ili zile tunazoweza kuzitatua tuzitatue na zile ambazo zitakuwa nje ya uwezo wetu tutaziwasilisha sehemu husika ili ziweze kutatuliwa.”


Katika hotuba yake. Mhe. Lubandamo aliongeza kuwa yeye kwa kushirikiana na Madiwani wengine wamejipanga kumaliza tatizo la upungufu wa madawati katika shule zote za sekondari.

“Nilipoingia kwenye Halmashauri kama mwenyekiti, mimi na madiwani wenzangu kipaumbele chetu cha kwanza ilikuwa ni kuhakikisha watoto wetu hawakai chini katika shule zetu zote za sekondari, na hadi sasa tumefanikisha upatikanaji wa madawati Zaidi ya 900.”

 “Ni mategemeo yetu kwamba ndani ya miezi 6 ijayo tutakuwa tumemaliza changamoto ya Madawati katika shule zetu.” Mhe. Twalib


Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ambaye ni Diwani wa Kata ya Imalilosongwe.  Mhe. Chuki Mbwanjine amewapongeza watumishi wa kata hiyo kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwataka kuendelea kufanya kazi ili kuweza kutatua kero za wananchi.

Aliongeza kuwa ameandaa hafla hiyo ili kuwapongeza na kuendelea kukuza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya wafanyakazi, wananchi pamoja na viongozi wa kisiasa na ameahidi kuandaa sherehe za kupongezana kwa kipindi chote atakachokuwa madarakani.

Baadhi ya Madiwani waliohudhuria maadhimisho hayo, wamempongeza Diwani wa Kata ya Imalilosongwe kwa kuandaa sherehe kama hiyo kwani inawaongezea wafanyakazi ari ya kufanya kazi kwa bidii sambamba na kuweka mahusiano mazuri kati yao na jamii na wameahidi kufanya hivyo kwenye kata zao.

Sherehe hizo ziliweza kuhudhuriwa na baadhi ya madiwani kutoka kata mbalimbali ambao ni Mhe. Twalib Lubandamo (Mwenyekiti wa Halmashauri) Diwani kutoka kata ya Itamboleo, Mhe. Bahati Salum kutoka Diwani kata ya Ihahi na Mhe. Elia Bange kutoka Diwani kata ya Kongoro Mswisi.

Wengine ni Mhe. Catherine Madenge (Diwani Viti Maalum), Pascalina Ndungulu (Diwani Viti Maalumu), Zamda Mussa (Diwani Viti Maalum) na Veronica Saga (Diwani Viti Maalum)

Katika maadhimisho hayo burudani mbalimbali zilikuwepo zikiwemo, Mpira wa pete kwa wanawake, Mpira wa miguu kwa wanaume, kuvuta Kamba, kukimbia na chupa pamoja na mbio za mita 100.

MWISHO

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.