• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

DC amaliza Mgogoro wa Mpaka kati ya Mtamba na Uturo uliodumu miaka 11

Posted on: March 8th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe Reuben Mfune, amehitimisha mgogoro wa mpaka uliodumu takribani kwa muda wa miaka 11 kati ya kijiji cha Uturo na Kijiji cha Mtamba vilivyopo kata ya Mapogoro wilayani hapa.

Mkuu wa Wilaya amemaliza mgogoro huo siku ya tarehe 07/03/2019 alipoitisha mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji hivyo viwili kwa ajili ya kuwasikiliza na kufikia hitimisho kwani kwa kipindi kirefu wamekuwa wakiishi bila ya maelewano.

Katika kumaliza mgogoro huo, Mhe. Mfune alisema kwamba, kwa kuwa kila upande unaendelea kushikilia msimamowake, maamuzi yake ya mwisho ya kumaliza ni kuwa eneo linalobishiwa litagawanywa lakini mgawanyo wake hautakuwa kama wengine walivyopendekeza.

kijiji cha uturo kitaishia eneo linaloitwa kwa maboga na kijiji cha Mtamba kitaishia eneo linaloitwa kwa Mpendwa upande mwingine wa barabara.

“haiwezekani tukaendelea kubishana kuhusu jambo moja miaka yote, na tunakaacha kufanya shughuli za maendeleo tunakuja kushinda hapa kwa ajili ya jambo moja. Wote hapa nyie ni ndugu halafu mnaleta migogoro isiyo na tija” alisema Mhe Mfune

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Aswege Kaminyoge, alisema kuwa, kwa mujibu wa sheria Mamlaka yenye mapendekezo ya kugawa eneo ndani ya kijiji ili kiweze kugawanyika ni mkutano mkuu wa kijiji husika, baada ya hapo unaandaliwa muhtasali ambao unapelekwa halmashauri, na mara baada ya muhtasari huo kukubaliwa, unapelekwa kwa Waziri mwenye dhamana ili aweze kugawa vijiji.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, walimshukuru Mkuu wa Wilaya ya Mbarali kwa kutatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kwani ulikuwa unawakwamisha kufanya shughuli zao za maendeleo kama ujenzi wa vyumba vya madarasa na zahanati.

Kijiji cha Uturo kiligawanyika mwaka 2009 na kuzaliwa vijiji vitatu, Kijiji cha Uturo, Kijiji cha Mtamba na Kijiji cha Ukwama.

Mgogoro kati ya Kijiji cha Uturo na Kijiji cha Mtamba ulianza mwaka 2009 mara baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa wakati wa ugawanyaji wa mali ambapo halmashauri ya vijiji vitatu Kijiji cha Uturo, Ukwama na Mtamba viliketi vikiwa na ajenda ya kugawanya mali za vijiji pamoja na kuoneshana mipaka kitu kilichopelekea vijiji vya Uturo na Mtamba kutofikia muafaka.

Eneo lililokuwa linagombaniwa ni kitongoji cha kilambo ambapo kila kijiji kiliingia zaidi kwa mwingine kwenye eneo lenye upana wa mita 260.

MWISHO

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.