• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

DC amshukuru Mdau wa Maendeleo kwa Kuguswa na Uhaba wa Madawati

Posted on: February 18th, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Rauben Mfune amemshukuru Ndg. Leopord Mwadembe kwa kuchangia viti pamoja na meza 10 zenye thamani ya shiling 500,000 kwa ajili ya kusaidia kupunguza uhaba wa Viti na Meza kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule za sekondari wilayani hapa.

Mhe. Mfune amezitoa shukrani hizo siki ya jumatatu ya tarehe 18/02/2019 katika Karakana ya magali ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali iliyopo makao makuu ya Halmashauri alipokuwa akikabidhiwa madawati hayo ili yakasaidie baadhi ya shule zenye uhaba mkubwa.

Akizungumza katika makabidhiano hayo alisema kuwa amewaandikia barua pamoja na kuwaomba wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani hapa ili waweze kusaidia upungufu wa viti na meza 4,616 kwani kwa mwaka jana 2018 kulitokea ongezeko kubwa la ufaulu wa wanafnzi wa darasa la saba tofauti na miaka nyuma.

“Tumewataarifu wananchi wote ambao shule zao zina upungufu wa viti na meza, vilevile tumewaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kutuchangia, tunamshukuru Ndg. Mwadembe kwa kuguswa na uhaba huu na kuamua kutuchangia viti pamoja na meza 10 vyenye thamani ya shilingi laki tano (500,000).”

“Nawaomba na wadau wengine ambao wamepokea wito na ambao hawajapokea wito, tunawakaribisha waweze kutuchangia madawati ili watoto wetu waweze kusoma katika mazingira mazuri.”

Naye Ndg. Leopord Mwadembe Mdau wa maendeleo anaetokea Kata ya Ubaruku  Wilaya ya Mbarali amewasihi wadau wengine wa maendeleo kuchangia madawati kama alivyofanya yeye, kwani watoto hawana sehemu ya kusemea, na kama mtu hana pesa bora akachangia hata nguvu kazi kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea.

“Hakuna mtu ambaye hana mtoto anayesoma sekondari, kama sio wa kwako kabisa basi ni wa ndugu yako, rafiki yako au jirani yako, na hatuwezi kuitegemea serikali peke yake ikafanya kila kitu, napenda kuonyesha hisia zangu kwa vitendo na kusonga mbele”

Ndg. Mwadembe aliongeza kuwa kuna fedha ambazo anaidai skimu ya umwagiliaji ya Mwenda Mtitu iliyopo wilayani hapa kiasi cha shilingi 8,500,000/=  ambazo alifanya kazi ya kutengeneza mfereji, kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi 3,500,000/= zikatwe kama mchango wake mwingine katika kuchangia upungufu wa madawati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma Msangi alisema kwamba anawapenda wadau kama hawa wa maendeleo ambao hawana itikadi za kisiasa katika masuala ya maendeleo, ofisi yake kwa kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya wanapokea mchango wowote ule, uwe mchango wa fedha au dawati hata kama likiwa moja kwani kwa sasa kuna uhitaji mkubwa sana wa viti pamoja na meza.

MWISHO

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.