• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

DC Apiga Marufuku Watoto Kuonekana Maeneo ya Machimbo.

Posted on: May 12th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune, amepiga marufuku watoto wote wenye umri chini ya miaka 18 kuonekana kwenye maeneo yote yanayojihusisha na uchimaji wa madini wilayani Mbarali kwani maeneo hayo sio salama kwao.

Mhe Mfune ameyasema hayo kwenye Mkutano wa hadhara yanapochimbwa Madini ya Dhahabu Kata ya Mapogoro na Lugelele siku ya tarehe 11/05/2021 alipofanya ziara na Kamati ya Usalama Wilaya kutembelea, kukagua pamoja na kutoa elimu ya Afya na Mazingira kwa wachimbaji wa maeneo hayo.


 “Marufuku kuleta watoto kwenye maeneo ya machimbo, tukija tena na tukakuta watoto huku, utakachokipata utasimulia, kwanza hairuhusiwi kuajili watoto wadogo, ukimleta mtoto hapa unamuweka kwenye mazingira hatarishi, acheni watoto nyumbani na nyie mje huku fufanya kazi.”

“Leo tumekuja kutoa elimu, tukija siku nyingine tutakuja kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria, watakaokiuka watapata sadaka zao, nachowaomba tulinde usalama wetu, na mtu wa kwanza kulinda usalama wako ni wewe mwenyewe.”  Alisema Mhe. Mfune

Mhe Mfune amewataka wachimbaji wote kuendelea kuchukua taadhari ya maisha yao kwa kujikinga na mambo mbalimbali ikiwemo kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya Corona na Ukimwi, uvutaji wa bangi, unywaji wa pombe kupita kiasi, na wakumbuke kuwa kuna watu wanawategemea, na kama wataona kuna kitu hakipo sawa washauri ili taratibu ziweze kufuatwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma Msangi alisema kwamba hategemei Dhahabu inayopatikana Mbarali ikawa kama laana ya kuleta ugomvi na migogoro, kwani watu wote wamekuja kutafuta pesa. Amewataka waachane na Imani potofu kwani masuala hayo yatasababisha kuvurugika kwa Amani.

“Yakitokea masuala ya Imani potofu tutaanza na nyie hakuna sehemu inayosema ili madini yapatikane ni lazima muue mtu.” Alisema Msangi

Naye Afisa Usafishaji na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Raphael Shitindi alisema kuwa wamiliki wa maendeo ya uchimbaji wa madini wanatakiwa kufanya tathimini ya athari ya mazingira ili kukabiliana na mambo mabaya ya uharibifu wa mazingira kwa ajili ya usalama wa watu wote.

Wakiongea katika nyakati tofauti baadhi ya wachimbaji wadogowadogo wameiomba Serikali kuendelea kutoa elimu ya mazingira, kuwatafutia soko pamoja kuwasaidia kupata maslahi mazuri kwa wamiliki wa mashimo ya madini na wamiliki wa makarasha kwani wamekuwa wakifanya kazi kubwa ila maslahi ni madogo.

Katika ziara hiyo vilevile Mkuu wa Wilaya aliweza kutembelea mradi wa Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi VETA, Ujenzi wa Stendi ya Igawa, kukagua uharibifu unaofanyika kwenye Reli ya TAZARA, Maeneo ya Hifadhi yanayosimamiwa na TAWA ambayo yanayovamiwa na wananchi pamoja na eneo la Machimbo ya Dhahabu.

MWISHO

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.