• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Maafisa Waandikishaji wa CHF iliyoboreshwa wakabidhiwa Simu Janja Mbarali

Posted on: October 23rd, 2020

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune amekabidhi vitendea kazi aina ya Simu janja 50 kwa maafisa waandikishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa (ICHF) kwenye ukumbi wa ofisi yake siku ya tarehe 23/10/2020 ili ziweze kuwasaidia kuwafikia wananchi wengi zaidi katika maeneo wanayofanyia kazi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mhe. Mfune amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma Msangi kwa kutekeleza agizo alilolitoa siku ya tarehe 13/05/2020 la  kununua simu 102 kwa awamu na hadi kufikia sasa ameweza kununua simu 50 zenye thamani ya kiasi cha shilingi 8,500,000 ili   kutatua changamoto zinazowakabili maafisa waandikishaji wa ICHF wilayani hapa.

“Simu zilizonunuliwa zitaongeza chachu ya kuandikisha kaya nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na kuhuisha kaya zilizoandikishwa awali zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Zingatieni lengo la kuandikisha angalau kaya 20 kwa mwezi kwa kila mwandikishaji ili kufikia lengo la wilaya la kuandikisha kaya 20,000 kwa mwaka.”

“Ninawataka maafisa waandikishaji wa CHF iliyoboreshwa mtunze simu hizi kama mali yenu ili muwendelee kuihudumia jamii mnayoishi nayo. Huduma ya uandikishaji imesogezwa kwenu mkiwa kama sehemu ya jamii ili kumwondolea usumbufu na umbali mwananchi kupata huduma hiyo mara anapoenda Hospitali au kituo cha afya.” Alisema Mhe Mfune

Mratibu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya iliyoboreshwa (ICHF) Ndg. Stephen Bitta alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imeanza utekelezaji wa mfuko huo mwezi Mei 2019 na hadi kufikia sasa Wilaya imeandikisha jumla ya kaya 1,614 sawa 2.3% ya lengo zima la kaya 69,667 au  sawa na 8.07% ya lengo la mwaka la kaya 20,000.

Aliongeza kuwa Uandikishaji wa wanachama wa ICHF umetofautiana kati ya Kitongoji, Kijiji na Kata moja na nyingine kutokana na sababu mbalimbali hususan mwitikio wa jamii, uwezo wa waandikishaji walioteuliwa, vitendea kazi pamoja na mwingiliano wa tatizo la maamubukizi ya ugonjwa wa Korona (Covid-19.)

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao kwenye zoezi wa ugawaji wa vitendea kazi hivyo, maafisa waandikishaji wa Mfuko wa Bima ya afya ya Jamii iliyoboreshwa wameushuruku uongozi wa Wilaya kwa kuwapatia vitendea kazi vya simu janja ambazo kwa sasa zitawaongezea ari ya kufanya kazi kwa bidii kwani simu hizo ni za kisasa na zinakwenda na wakati uliopo.

MWISHO

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.