• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

MILIONI 151 ZIMEPATIKANA KUWEZESHA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA MBARALI- RC MBEYA

Posted on: December 18th, 2019

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila siku ya tarehe 18/12/2019 kwenye Harambee kubwa iliyoitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune katika ukumbi wa Polisi uliopo Rujewa Mbarali kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miundombinu ya vyumba 36 vya madarasa.

Mhe. Chalamila alisema kuwa jumla ya kiasi cha cha Tsh. 151,677,583/= Miloni zimepatikana kwenye Harambee hiyo kati ya shilingi 288,705,000/= ambazo zilikuwa zinahitajika kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi ili ifikapo Januari 9, 2020 wanafunzi wote waliochagulia waweze kuanza kidato cha kwanza.

Kati ya fedha zilizopatikana, shilingi 61,017,583/= milioni ni fedha taslimu, shilingi 51,680,000/= milioni ni ahadi pamoja na shilingi 38,583,000/= milioni ni vifaa vya ujenzi.

“Ndugu zangu mlichokifanya leo hii ni majitoleo na sadaka kubwa sana kwa Mungu na kwa watoto wetu tunaowahangaikia. Sio jambo dogo kwa kipindi hiki cha kilimo watu kujitoa na kupatikana kiasi chote hiki cha fedha, huu ni upendo wa kipekee mno, niwashukuruni sana lakini niushukuru uongozi Mbarali kwa kuwa wabunifu kwa kiasi kikubwa”.

“Kwa Mkoa wote wa Mbeya tuna upungufu wa vyumba vya madarasa 59, ila kwa Mbarali peke yake kuna upungufu wa vyumba 36 ambapo ni zaidi ya alilimia 50, tatizo hili limetokana na elimu bure inayotolewa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muunngano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli, tuchangie maendeleo, Mbarali ni yetu sote.” Alisema Mhe. Chalamila

Vilevile Mkuu wa Mkoa amemshukuru Msanii Masanja Mkanamizaji (Emanuel Mgaya) kwa kushereheza vizuri Harambee hiyo na kupelekea watu kujitoa kwa wingi kuchangia ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune alisema kuwa wananchi wa Mbarali wanafanya kazi kwa bidii sana kwani kuna ujenzi wa shule 9 mpya unaendelea, na vilevile kuna ujenzi vyumba vya madarasa unaoendelea kwenye shule zilizokuwepo.

Mhe. Mfune aliongeza kuwa vyumba vyote 36 vinatakiwa kukamilika kabla ya Januari 9 2020 ili watoto wetu waweze kuanza kidato cha kwanza na fedha ambazo zitapatikana hapa zitawaongezea nguvu wananchi ili waweze kupata vifaa mbalimbali vya ujenzi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mhe. Francis Mtega alisema kwamba elimu ni kitu muhimu sana, watu wengi ni mahodari kuchangia kwenye harusi na kusahau kuwa elimu ni urithi halisi wa kila kijana, namshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kutekeleza ahadi zote alizozitoa na ametufundisha kwa vitendo kwamba tuheshimu na kuijali sana elimu.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma H. Msangi alisema kuwa Wilaya ya Mbarali ina jumla ya shule za sekondari 25 kati ya hizo 18 ni za Serikali na uhitaji wa vyumba vya madarasa na madawati unatokana na ongezeko kubwa la ufaulu wa wanafunzi waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2019 ambapo jumla ya wanafunzi wa 5,578 walifanya mtihani na wanafunzi 4,800 walifaulu sawa na asilimia 86.6 ikilinganishwa na ufaulu huo kwa mwaka 2018 ambao ulikuwa ni asilimia 70.1.

MWISHO

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.