• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

"Tuna Upungufu wa Vyumba 39 vya Madarasa”

Posted on: December 12th, 2017

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune siku ya Jumatatu ya tarehe 11/12/2017 alipoitisha kikao cha pamoja kati ya Waheshimiwa Madiwani, Walezi wa Kata pamoja na Watendaji wa Kata ofisini kwake kwa ajili ya kujadili mapokezi ya Vijana wa kidato cha kwanza na namna ya kutatua changamoto ya upungufu wa Vyumba vya  Madarasa 39 na Madawati 2748 yaliyosababishwa na ongezeko la ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba mwaka 2017.

Jumla ya wanafunzi 6,556 walifanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi Darasa la saba, 4,264 wamefaulu mtihani wao, sawa na asilimia 63.5 ya ufaulu kutoka alilimia 53.9 ya mwaka 2016. Kati ya wanafunzi 4,264 waliofauru mtihani, Wanafunzi 2,686 wamechaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari ya kidato cha kwanza kwenye shule mbalimbali kwa mwaka 2018.

“Kila mmoja anajua umuhimu wa swala hili katika eneo lake, na kila mmoja amekuwa akijitahidi kwa jinsi anavyoweza kushirikiana na wananchi alionao kuhakikisha swala hili linafika mwisho, kwa hiyo nitoe wito kwamba kila mmoja wetu tunajua kwamba mwezi wa 12 umefika na ni mwezi wa kilimo, ni muda ambao wanafunzi wanatakiwa waende shule mbalimbali, lakini swala letu hili ni muhimu sana, na Wilaya hii haiwategemei watu wengine  zaidi ya sisi tuliomo ndani ya chumba hiki, viongozi woote ndio sisi tuliopo hapa, kila mmoja aone ananafasi kubwa sana ya kuhakikisha swala hili linafanikiwa” alisema Mhe Mfune

Mhe. Mkuu wa Wilaya ameagiza kutumika kwa fedha zilizopo kwenye akaunti za  Vijiji ili kumalizia ujenzi wa madarasa hayo, na  kwa Vijiji ambavyo havina fedha michango iendelee, vile Vijiji vyenye fedha navyo michango iendelee kwa ajili ya kuludishia fedha hizo kwenye akaunti zilikotolewa ili kuendelea na shughuli ambazo wamejipangia. Ameagiza kuwa fedha hizo ili kutoka zisisubili kikao cha Kijiji kiamue au WDC (Kamati ya Maendeleo ya Kata) iamue hayo ni maelekezo yake, na yeye ndie atakayejibu kuhusu hilo. 

Kuhusu mifuko ya saruji 75 iliyotolewa kwa kila Kijiji, kwa Vijiji vyote 102 na Mbunge wa Mbarali Mhe. Haroon Pirmohamed, Mhe Mfune ameagiza mifuko hiyo itumike katika ujenzi wa madarasa. Vilevile ameahidi kuanza kufanya ziara ya kukagua maelekezo aliyoyatoa akiongozana  na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kuanzaia siku ya Ijumaa ya 15/12/2017 na kuendelea.

Katibu Tawala wa Wilaya ya Mbarali Ndg. Ezekia Kilemile amemshukuru Mhe. Mkuu wa Wilaya kwa kuitisha kiakao hicho na amewaomba Wah. Madiwani, Walezi wa Kata na Watendaji wa Kata washirikiane kwani kwa sasa tumepandisha ufaulu kwa asilimia 10 na amemshukuru Mhe. Mkuu wa Wilaya kutoa ridhaa ya mifuko ya saruji iliyotolewa na  Mhe. Mbunge kutumika kujenga madarasa hayo na anaamini hadi kufikia tarehe 08/01/2018 tutakuwa tumekamilisha ujenzi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mhe. Francis Mtega amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa fursa aliyompa kwani kwa kawaida hotuba ya Mkuu wa Wilaya huwa ni maagizo, maagizo siku zote huwa hayajadiliwi, na ameahidi kwa niaba ya Wah. Madiwani wengine wanakwenda kutekeleza maagizo yote yaliyotolewa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbarali. Ndg. Kivuma H. Msangi amewashukuru Waheshimiwa madiwani wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri kwa kuhudhuria kikao hicho,na  amewataka Watendaji wote wa Kata na uongozi wao kwa ujumla kutoa ushirikia kwa walezi wa Kata, kwani wanamwakilisha Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi Mtendaji kwani wanajitoa kusafiri kwa gharama zao kwenda kutatua matatizo katika kata.

Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.