• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Mbarali District Council

  • Home
  • About Us
    • Our History
    • Mission and Vision
    • Core Values
    • Strategies
  • Administrations
    • Organization Structure
    • Departments
      • Finance
      • Administration Natural Resources
      • Works and Fire
      • Primary Education
      • Economy Planning and Statistics
      • Land and Natural Resource
      • Agriculture
      • Secondary Education
      • Hearth
      • Rural Water and Sanitation
      • Livestock and Fisheries
      • Community Development
      • Environmental and Solid Waste
    • Units/Sections
      • Procurement and Surprises
      • ICT Units
      • Law
      • Internal Auditor
      • Bee
      • Election
  • Investment
    • Tourism
    • Agriculture
    • Livestock
  • Our Services
    • Health
    • Education
      • Primary Education
      • Secondary Education
    • Water Services
    • Agriculture
    • Livestock and Fisheries
    • Staff Services
  • Councilors
    • Councilors List
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Permanent Committee
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Projects
    • Planned Projects
    • Completed Projects
    • Ongoing Project
  • Publications
    • By Laws
      • Guidlines
    • Costumer Services Contract
    • Strategies
    • Reports
    • Forms
      • Application Form
    • Guidelines
    • Publications
  • Media Centre
    • Press Release
    • Speeches
    • Photo Gallery

Wasichana 4,511 Kupatiwa Chanjo Mbarali

Posted on: April 25th, 2018

Wilaya ya Mbarali inatarajia kutoa chanjo ya kukinga Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wasichana 4511 wanaotimiza umri wa miaka 14 kwa mwaka 2018,kupitia vituo 49 vya kutolea huduma za afya kwa kutumia Mkoba kwa shule 50 za sekondari pamoja na msingi ambazo zipo mbali na vituo vya kutolea huduma za afya.

hayo yamebainishwa kwenye uzinduzi wa Chanjo ya kinga ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana wote waliotimiza umri miaka 14 katika viwanja vya shule ya msingi rujewa siku ya tarehe 24/04/2018.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune alisema kuwa ili kupata kinga kamili wasichana wanatakiwa kupata dozi mbili ambapo kwa dozi ya kwanza itatolewa muda wowote binti anapofikisha umri wa miaka 14 na dozi ya pili itatolewa baada ya miezi sita kupita.

akiwa katika uzinduzi huo, Mhe. Mfune alitoa rai kwa Viongozi wa Serikali, Viongozi wa Kisiasa pamoja na Viongozi Dini, kusaidia kufikisha ujumbe wa uanzishwaji wa chanjo hiyo ya kuzuia Saratani ya Mlango wa Kizazi kwa wazazi na walezi wa mabinti wote waliotimiza miaka 14 waweze kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kutolea huduma za afya ili waweze kupata kinga muhimu katika maisha yao.

Aidha Mhe. Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa katika kukabiliana na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kumekuwa na mafanikio makubwa hapa nchini, mfano magonjwa ya Ndui na Pepopunda kwa watoto wachanga yametoweka katika jamii kwa muda mrefu.

Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Dkt.Godfrey Mwakalila ameiomba jamii kutopotosha kuhusu chanjo hiyo inayotolewa na badala yake kuhamasisha watoto wote waliotimiza umri wa miaka 14 kufika katika maeneo na vituo vinavyotoa chanjo hiyo kwa manufaa yao ya baadae.

Dkt.Mwakalila aliongeza kuwa jamii inatakiwa itambue zoezi hili muhimu kwa wasichana waliotimiza mikaka 14 kwani kumekuwa na vifo vingi vitokanavyo na uzazi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Rujewa, Mhe Mkude Msasi alisema kuwa kumekuwa na tabia kwa baadhi ya wazazi kunapokuwa na matukio muhimu ya kitaifa hujaribu kukwamisha kwa kutowaleta watoto wao ili waweze kupatiwa chanjo.

“Wazazi na walezi wakishaona matukio kama haya makubwa huenda kwa Diwani wa eneo husika au Mwenyekikti ili kumkatalia mtoto kuwa hawezi kumpeleka na kutoa sababu mbali mbali, ndungu wazazi na walezi tuone kuwa tukio hili ni la muhimu sana kwa watoto wetu kwani litasaidia kuepuka vifo” alisema Diwani.





Announcements

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MBARALI DC- STRATEGIC PLAN WORD 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • View All

Latest News

  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIZINDUA NYUMBA YA WALIMU SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • MKUU WA WILAYA YA MBARALI MHE KANALI MAULID HASSAN SURUMBU AKIPANDA MTI WAKATI WA KUTEMBELEA MRADI WA KUSINDIKA MAZIWA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA UNAOTEKELEZWA NA KIKUNDI CHA NOPADEO WOMEN GROUP CHA KATA YA ITAMBOLEO KIJIJI CHA MATEBETE

    June 06, 2025
  • MKUU WA MKOA WA MBEYA DKT JUMA ZUBERI HOMERA AKIPANDA MTI KATIKA SHULE YA SEKONDARI NYEREGETE

    June 05, 2025
  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • View All

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
More Videos

Quick Links

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Related Links

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Postal Address: 237 Rujewa Mbeya

    Telephone: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Email: ded@mbaralidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.