• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

kata ya Madibira

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA MADIBIRA



Mhe. 

DIWANI WA KATA 


Mhe. Paskalina E. Ndungulu

DIWANI VITI MAALUMU

 

TAARIFA YA KATA YA MADIBIRA

 

1. UTANGULIZI

Kata ya Madibira ipo Wilaya ya Mbarali Tarafa ya Rujewa, upande wa Magharibi, umbali wa kilometa 81 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.

Kata hii imepakana na kata ya Miyombweni upande wa Kusini.

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vijiji kuna Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Maafisa watendaji wa Vijiji.

Kata ya Madibira ina jumla ya watumishi 161 wa kada mbalimbali kama ifuatavyo: Utawala 8, Elimu watumishi 108, Afya watumishi 34, Maliasili watumishi 2, Kilimo watumishi 6, Mifugo watumishi 2 na Maendeleo ya jamii watumishi 1.

Kata ya Madibira ina Jumla ya Vijiji 7 ambavyo ni Kijiji cha Iheha, Kijiji cha Mahango, Kijiji cha Chalisuka, Kijiji cha Mkunywa, Kijiji cha Ikoga Mpya, Kijiji cha Nyamakuyu na Kijiji cha Nyakadete. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo 38.

Kata ya Madibira ina jumla ya wakazi wapatao 28,550 kati yao Wanaume 13,327 na Wanawake 15,223. Makabila yanayopatikana katika Kata ya Madibira ni Wasangu, Wabena, Wasukuma, na Wahehe.

Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata shughuli za kiuchumi kwa wananchi wake kama ifuatavyo; Kilimo, Ufugaji na Biashara.

Vyanzo vya Mapato katika kata hii inatofautiana kutokana na Kijiji kimoja hadi kingine, miongoni mwa vyanzo hivyo ni kama; faini/adhabu mbalimbali, pawatila za Vijiji, michango ya wananchi, ushuru mdogomdogo, Ruzuku kutoka Serikali kuu (Halmashauri ya Wilaya) pamoja na misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali.

Vivutio vya utalii vinavyopatikana katika kata ni Pori la wanyamapori la Waga ambalo lipo kwenye kiji cha Nyamakuyu na Nyakadete pamoja na hifadhi ya Misitu ya Asili.

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha kila Kijiji kina Kamati ya Ulinzi na Usalama ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana vilevile kuna Kituo cha ambapo sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

 

2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

 A. ELIMU

Kata ya Madibira ina Jumla walimu 108, shule za Msingi 8 za Serikali, binafsi moja pamoja na shule ya sekondari moja.

 i. ELIMU MSINGI

  • Shule ya Msingi Iheha
  • Shule ya Msingi Mahango
  • Shule ya Msingi Chalisuka
  • Shule ya Msingi Madibira
  • Shule ya Msingi Mkunywa
  • Shule ya Msingi Ikoga Mpya
  • Shule ya Msingi Nyamakuyu
  • Shule ya Msingi Nyakadete
  • Shule ya Msungi St. Maurus.

 ii. ELIMU SEKONDARI

Kuna  shule moja ya sekondali inayoitwa Madibira High School.

B. AFYA

Kata ya Madibira ina  watumishi wa idara ya afya 34, Kituo cha Afya 1, zahanati 3 za Serikali na moja ya Binafsi. Magonjwa yanayosumbua mara kwa mara ni ; Kuhara, Pnemonia, Magonjwa ya mfumo wa njia ya hewa na UTI

 

C. KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA

Kata ya Madibira ina jumla ya watumishi 6 idara ya kilimo na ushirika, na ina jumla ya wakulima 9,224. Mazao yanayopatikana  katika kata ya ni Mpunga, Mahindi, Karanga, Alizeti na Mtama.

Kuna skimu moja ya umwagiliaji ambayo inajulikana kwa jina la Skimu ya Umwagiliaji Igomero pamoja na vyama vya ushirika vitatu ambavyo ni MAMCOS, M-SACCOS na Mkunywa SACCOS.

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ;

  • Huduma za ugani
  • Mashamba darasa juu ya Kilimo cha Kisasa
  • Hifadhi bora ya Mazao ya Chakula
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Kutatua Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao
  • Kukusanya takweimu za Mvua
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji ya kila robo mwaka na kuwasilisha wilayani.
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Kilimo katika Kamati ya Maendeleo ya kata.

D. MIFUGO NA UVUVI

Kata ya Madibira ina jumla ya watumishi 2 wa idara ya mifugo na Uvuvi, na ina jumla ya mifugo kama ifuatavyo:

  • Ng’ombe                     14,445
  • Bata                            106,
  • Mbuzi                          3,400,
  • Punda                          100,
  • Nguruwe                     950,
  • Mbwa                          1,300
  • Kuku                           44,600.

Magonjwa yanayosumbua mifugo mara kwa mara ni nagama, CBPP, CCPP, Ndigana na Minyoo. 

 

Huduma zinazotolewa na Idara ni pamoja na;

  • Tiba kwa magonjwa dhidi ya Mifugo
  • Huduma mbalimbali za Mifugo kama kuhasi, kukata pembe, kwato na midomo, kupiga chapa Mifugo, kukata meno, kuzalisha, kuogesha na Ukaguzi wa nyama
  • Ushauri juu ya ujenzi bora wa mabanda ya Mifugo
  • Kutoa elimu ya ufugaji bora wa namna ya ufugaji wa Mifugo yenye tija
  • Ukaguzi wa Nyama na usafi katika Machinjio
  • Kusimamia zoezi Endelevu la upigaji chapa wa mifugo

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata hii. Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.

 

E. MALIASILI

Kata ya Madibira ina watumishi wawili upande wa Misitu na wanyamapori, na Kata ya Madibira ina uhifadhi wa misitu katika kijiji cha Iheha, Nyamakuyu na Nyakadete

 

  i.Vivutio vya Utalii

  • Pori la Wanyamapori la Waga,
  • Hifadhi ya Misitu ya asili.

 

 ii. Hifadhi ya Misitu

Kata ya Madibira inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzaji wa hifadhi kwa kushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) katika Vijiji vilivyopakana na hifadhi hizo, kupanda miti, kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kuchoma mkaa na kukata miti hovyo bila ya kuipanda upya, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.

 

 iii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo. 

Kata inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya misituasili na vyanzo vya maji kwa matumizi Endelevu, kuendelea kushirikia na taasisi ya JUWABONDECHI katika zoezi la upandaji wa miti rafiki na maji kila mwaka kwenye vyanzo vya maji na maeneo yenye chemchemu, kushauri kutengwa kwa Bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika Vijiji.

F. MAENDELEO YA JAMII

Kata ya Madibira ina mtumishi mmoja wa Idara ya Maendeleo ya Jamii mpaka sasa, huduma zinazotolewa na kata ni  kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • SALAMU ZA EID EL FITR

    March 31, 2025
  • DC MBARALI AANDAA HAFLA YA IFTALI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE,TASISI ZOTE NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU..

    March 28, 2025
  • DC MBARALI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA CHIMALA

    March 14, 2025
  • KIKAO CHA DCC KUPENDEKEZA MAJINA YA MAJIMBO WILAYANI MBARALI

    March 13, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.