• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Tarehe ya Kuanza: February 11th, 2021

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI 

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, limepitia na kupitisha mapendekezo ya mpango wa Bajeti kiasi cha Sh. 45,890,254,767.49 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 kutoka vyanzo mbalimbali vya Mapato siku ya tarehe 11/02/2021.

Kati ya fedha hizo, Mapato kutoka Serikali Kuu na Wadau wa Maendeleo ni Sh. 40,990,998,767.49 na Mapato kutoka katika vyanzo vya ndani (Own Source) Sh. 4,899,256,000.00. Mgawanyo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo Sh. 31,036,186,000.00 ni Mishahara, Sh. 5,176,754,785.49 ni Matumizi ya kawaida na Sh. 9,677,313,982.00 ni Miradi ya Maendeleo.

Mpango na Bajeti ya Miaka Mitatu 2021/22- 2023/24 na Makisio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2021/22 umeandaliwa kwa kuzingatia, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala (CCM) 2020-2025, Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. John Pombe Joseph Magufuli wakati wa kufungua rasmi Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma Tarehe 13 Novemba, 2020.

Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti Serikali kwa mwaka 2021/22 uliotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango, Vipaumbele vya Serikali ya awamu ya tano, Maagizo ya Viongozi wa Kitaifa, Mpango Mkakati wa Halmashauri wa Mwaka 2018/19 - 2023/24, Mpango Mkakati wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI),

Mpango Mkakati wa Lishe wa Taifa, Sheria ya Bajeti Na. 11 ya mwaka 2015 na Kanuni zake, Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025, Mpango wa Maendeleo Endelevu 2030, Mapitio ya Utekelezaji wa Bajeti ya mwaka 2020/21, pamoja na Vipaumbele vya wananchi wa Wilaya ya Mbarali kupitia Mfumo ulioboreshwa wa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (Improved Opportunities and Obstacles to Development- O&OD)

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali inafikia malengo ya kuwahudumia wananchi wake kupitia Mpango wa Miaka Mitatu 2021/22- 2023/24, Sekta za Kilimo, Mifugo, Elimu Msingi, Elimu Sekondari, Ardhi na Maendeleo ya Jamii zitaonesha matokeo chanya ya malengo katika kutekeleza mpango wa miaka mitatu

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali katika bajeti yake ya mwaka 2021/22 itajikita katika kuendelea na Ujenzi Miradi ya Kimkakati iliyopata fedha kutoka Serikali kuu ambayo ni Kituo cha Afya Utengule Usangu na Hospitali ya Wilaya, Kuwezesha ukamilishaji wa ujenzi wa banio katika Skimu ya Umwagiliaji Ukwavila, Kuwezesha ujenzi wa vivusha maji vitatu (3) katika Skimu ya Umwagiliaji Msesule, Kuwezesha usakafiaji wa mfereji mita 40 skimu ya umwagiliaji Azimio Mswiswi (FAO).

Kuendelea na ujenzi wa kituo cha Afya Mahongole, kuwezesha uchimbaji wa visima katika Shule za Sekondari za Ihanga- Mbarali na Ipwani, Kujenga shule ya Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza (English Medium Primary School), Kuwezesha wakulima 70 kuzalisha mbengu za kuazimia ubora (QDS) tani 210 katika Kongani 3 za Rujewa, Madibira na Igurusi.

Kuendelea na ujenzi wa Shule ya Wasichana Uturo, Kuendeleza ujenzi wa miundombinu katika Shule za Sekondari na Msingi, Kutoa usaidizi katika Jitihada mbalimbali za wananchi katika Vijiji na Kata, Kuboresha miundombinu katika Sekta ya Kilimo na Mifugo, Kuboresha Lishe kwa watoto, Ulipaji wa madeni mbalimbali, Kuwezesha vikundi vya wanawake, vijana na walemavu.

Kuendelea kupambana na Maambukizi ya VVU/UKIMWI, Kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika Uchumi wa Viwanda, Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi (Climate Change) pamoja na kutambua jitihada za Jamii katika Kukabiliana na Mabadiliko hayo pamoja na Kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Halmashauri kwa kuboresha vyanzo vya mapato vilivyopo pamoja na kubuni vyanzo vipya.

Katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2020/21, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali iliidhinishiwa matumizi ya jumla ya Sh. 45,930,332,615.00  kati ya hizo Sh. 32,090,368,000.00 ni matumizi ya mishahara, Sh. 3,937,500,000.00 ni Mapato ya ndani, Sh. 1,159,244,999.00. ni matumizi mengineyo NHIF Sh. 300,000,000.00, CHF Sh. 100,000,000.00, User Fee Sh. 150,000,000, Ada za Wanafunzi Sh. 40,250,000.00, Michango ya Jamii (EK, Minara, nk) Sh. 144,256,000.00 na Sh. 8,008,713,616.00 ni matumizi ya miradi ya maendeleo.

Hadi kufikia Disemba, 2020, Jumla ya Sh. 18,596,749,460.65 zilipokelewa kati ya hizo, Sh. 13,939,100,697.00 ni fedha za mishahara, Sh. 718,750,500.00 ni fedha za matumizi mengineyo, Sh. 1,650,395,929.81 ni miradi ya maendeleo na Sh. 2,120,112,010.95 ni makusanyo ya ndani, NHIF Sh. 28,109,060.00, CHF Sh. 48,281,266.29 na User Fee Sh 48,399,496.60 na ada za wanafunzi Sh. 43,600,500.00.00. Hii ni sawa na asilimia 40.49 ya fedha zilizoidhinishwa kwa mwaka 2020/2021.

Kwa taarifa zaidi tembelea http://mbaralidc.go.tz/announcement/muhtasali-wa-bajeti-ya-halmashauri-ya-wilaya-ya-mbarali-ya-mwaka-2021-2022


Daudi B. Nyingo

Afisa Habari

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

11/02/2021

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.