Kituo cha Afya cha Utengule Usangu ambacho kinaboreshwa katika Kata ya Utengule wilayani ya Mbarali, kinatarajiwa kutoa huduma mbalimbali za kisasa kwa ajili ya kuhudumia wananchi mara baada ya kukamilika kwake.
Kituo hicho kinategemea kutoa huduma mbalimbali kwa jamii inayokizunguka zikiwemo huduma za upasuaji hasa kwa akina mama, huduma za uzazi za kujifungua kwa akina mama, huduma ya vipimo vya maabara, kulaza wagonjwa wa aina zote, kuhifadhi maiti, huduma kwa wagonjwa wa nje, kutakuwa na mifumo ya maji pamoja na nyumba kwa ajili ya kuishi watumishi watakaohudumu kituo cha afya.
Jumla ya majengo mapya saba yanatarajiwa kujengwa yakiwamo:- jengo la upasuaji, jengo la wazazi, jengo la kufulia nguo, jengo la maabara, jengo la kuhifadhia maiti, nyumba ya mtumishi inayojitegemea, jengo la wagonjwa wa ndani (wodi ya wanawake, wodi ya wanaume na wodi ya watoto) pamoja na njia ya kupitishia wagonjwa
Hadi kumalika kituo hiki, kiasi cha shilingi milioni mia tano na hamsini na tano, mia moja na tisa elfu mia nane kumi na mbili (555,109,812/=). kinakadiliwa kutumika. Kati ya fedha hizo kiasi cha shilingi Milioni Mia Nne (400,000,000/=) zimetolewa na Serikali kuu, shilingi milioni mia moja hamsini na tano, mia moja na tisa elfu mia nane kumi na mbili (155,109,812/=) Ni mchango wa Halmashauri ya Wilaya, Wadau mbalimbali pamoja na wananchi.
Kukamilika kwa Kituo hiki kutawezesha wananchi zaidi ya kata sita ambazo zinakizunguka kuhudumiwa. Kata hizo ni Kata ya Utengule Usangu, Kata ya Luhanga, Kata ya Mwatenga, Kata ya Igurusi, Kata ya Kongolo Mswiswi pamoja na Kata ya Mahongole.
Daudi Nyingo
Afisa Habari na Mahusiano
Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mbeya
March 21, 2018
Rujewa Road 3 km from main Road
Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya
Simu ya Mezani: 252957440/252957447
Mobile: +255713317374
Barua Pepe: ded.mbarali@mbeya.go.tz
Copyright ©2018 GWF . All rights reserved.