• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mazingira na Udhibiti wa Taka Ngumu

Mkuu wa Idara: Ndg. Raphael Shitindi

Majukumu ya Msingi ya Idara;

Hifadhi ya Mazingira

  • Kutenga maeneo ya Upandaji Miti, Majani, Maua, ukataji Miti na Upendezeshaji Mazingira na kusimamia Kampeni ya Taifa ya upandaji miti.
  • Kuhamasisha Jamii kupanda Miti, Majani na Maua, ili kupendezesha Miji na maeneo mbalimbali.
  • Kuandaa na kufuatilia utekelezaji wa Mipango ya Halmashauriya Wilaya ya Mbarali ya usimamizi wa Mazingira kwa kuzingatia Mpango kazi wa Taifa wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
  • Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo na miongozo ya kulinda Mazingira ikiwa ni pamoja na bioanui, Ardhi, Mazingira ya Mito, Maziwa Bahari na Mabwawa,
  • Kubaini maeneo ya hatari yanayohitaji usimamizi maalumu na kumshauri Waziri mwenye dhamana ya Usimamizi wa Mazingira kuhusu njia bora zinazoweza kutumika.
  • Kuandaa Taarifa ya Hali ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
  • Kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji kwa Kudhibiti utekelezaji wa shughuli yoyote inayoweza kuleta athari katika maeneo ya mito, maziwa, Bahari na Mabwawa.
  • Kubaini Bioanui zilizopo katika Halmashauriya Wilaya ya Mbarali na hali ya uharibifu na uhifadhi wake.
  • Kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi bora ya Ardhi ya Halmashauriya Wilaya ya Mbarali.
  • Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na programu za Halmashauriya Wilaya ya Mbarali kwa kuzingatia Mkakati wa matumizi Salama ya Teknolojia ya Kisasa (Biosafety).
  • Kuhamasisha matumizi ya teknolojia ya nishati mbadala pamoja na majiko banifu.
  • Kuandaa na kutekeleza miradi mbalimbali kuhusu Usimamizi wa Hifadhi ya Mazingira.
  • Kutoa mapendekezo na kufuatilia hatua za kukabiliana na uharibifu wa maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizo endelevu (kama uchimbaji madini, kilimo, ujenzi, ufugaji n.k);

Udhibitiwa uchafuzi wa Mazingira(Ardhi,Maji na Hewa)

  • Kuandaa na kutekeleza programu za kutoa elimu ya Mazingira kwa Jamii kuhusu njia bora za kudhibiti uchafuzi wa Mazingira na athari zake.
  • Kuweka miongozo ya kupunguza athari za uchafuzi wa hewa ya ndani ya makazi (in-door pollution) inayosababishwa na shughuli mbalimbali kama vile matumizi ya nishati ya kuni, vinyesi vya mifugo na uchomaji wa madini ya zebaki.
  • Kufatilia na kutathimini athari za uchafuzi wa Mazingira katika makazi, viwanda, migodi, ujenzi, biashara, kilimo na ufugaji.
  • Kuandaa na kusimamia miongozo ya kutenganisha maeneo ya makazi ya watu, ofisi na taasisi za elimu na shughuli za kiuchumi kama vile ujenzi wa viwanda, madampo ili kudhibiti athari kwa afya na Mazingira.

Tathmini ya Athari ya Mazingira

  • Kufuatilia utekelezaji wa tathmini ya athari ya Mazingira [TAM] kwa shughuli zinazotakiwa kufanyiwa.
  • Kufuatilia utekelezaji wa mpango na masharti ya TAM kwa kila shughuli/mradi uliofanyiwa tathmini hiyo au kukaguliwa.
  • Kushirikisha umma katika maamuzi yanayoweza kuathiri Mazingira na katika uandaaji wa sera, mikakati, mipango na kufanya utafiti/uchunguzi wa uharibifu au athari ya Mazingira unaosababishwa na shughuli za kiuchumi au kijamii na kutoa taarifa kwa Mkurugenzi mkuu NEMC.
  • Kufuatilia na kutoa ushauri kuhusu maeneo yaliyoathirika kutokana na shughuli za uchumi zisizoendelevu kama vile uchimbaji madini holela, uvuvi haramu, kilimo kisichokuwa endelevu, ujenzi holela, ufugaji wa kuhamahama usiozingatia uwezo wa marisho n.k.
  • Kusimamia/kuratibu utekelezaji wa kazi za kamati za Mazingira na kamati za kudumu za Halmashauriya Wilaya ya Mbarali zinazoanzishwa na sheria ya usimamizi wa Mazingira ngazi ya Halmashauriya Wilaya ya Mbarali hadi kitongoji/mtaa;
  • Kuandaa na kutekeleza mikakati, mipango na program za Halmashauriya Wilaya ya Mbarali kwa kuzingatia mkakati wa kitaifa wa kuhimili na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Udhibiti wa Taka Ngumu

  • Kubuni mbinu za kupunguza taka na kusimamia utekelezaji wake ili kupunguza uchafuzi wa Mazingira.
  • Kufanya tafiti/uchunguzi ili kubaini aina za taka zinazozalishwa kutoka katika masoko, makazi, maeneo ya barabara na taasisi pia kubuni njia bora za kupunguza, kutenganisha, kuhifadhi na kutupa taka;
  • Kusimamia Usafi katika mifereji ya kukusanya maji ya mvua na kuhakikisha inafanya kazi muda wote.
  • Kuweka vyombo vya kuhifadhi taka katika maeneo yote ya umma.
  • Kuainisha na kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa dampo za kisasa.
  • Kutoa amri za kuzuia utupaji ovyo wa taka wa aina zote katika fukwe, maeneo ya wazi, mito na mifereji ya maji ya mvua.

Changamoto za Mazingira

  • Uharibifu wa Misitu ya asili (Deforestation / Forest degradation).
  • Uharibifu wa Mifumo ya ikologia ya Maji (River and Wetland Degradation).
  • Mifumo na Vyanzo.
  • Uharibifu wa Ardhi (Land Degradation).
  • Kupotea kwa Bionuai ( Loss of Biodiversity).
  • Uharibifu na Uchafuzi wa Mazingira.
  • Mabadiliko Tabianchi (Climate Change).

Shinikizo (Pressure) 

  • Kasi ya uharibifu wa Mazingira inasababishwa na utupaji wa taka ovyo, ukosefu wa madampo ya kisasa, Kilimo cha Kuhamahama, upanuzi wa mashamba, Matumizi makubwa ya nishati ya kuni na mkaa, mifugo mingi kupita kiasi, uchimbaji holela wa madini, ukataji miti kwa ajili ya kuni, mkaa, nguzo na mbao, ujenzi wa miundombinu ya barabara unaoambatana na ufyekaji miti na misitu ovyo, ni mashinikizo yanayosababisha uharibifu wa Mazingira.

Hatua zinazochukuliwa kukabiliana na uharibifu wa mazingira

Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali imechukua na inaendelea na mikakati na mipango endelevu ifuatayo:-

  • Kuondoa watu waliovamia Misitu kwa ajili ya makazi na shughuli za kilimo,uchimbaji wa madini na ufugaji.
  • Kutoza faini kwa wavamizi wa Misitu.
  • Kuhamasisha upandaji miti, utunzaji misitu na ufugaji nyuki wa kisasa kwenye misitu kwa wadau 234 wenye mizinga zaidi ya 1590).
  • Kuhamasisha jamii na kutoa elimu juu ya kilimo cha kutumia makinga maji na matumizi ya mbolea ya asili.
  • Kuhamasisha jamii na kutoa elimu kwa jamii juu ya utunzaji wa mazingira; kusimamia utekelezaji wa sheria ya Misitu 2002 na Usimamizi wa sheria ya Mazingira 2004 na kanuni zake.
  • Kushirikisha wadau mbalimbali muhimu katika kusimamia utunzaji wa mazingira.
  • Kuandaa miongozo ya kuzuia uharibifu wa Misitu katika maeneo ya uwekezaji,
  • kuendelea na kampeni ya upandaji miti million 1.5 kila Mwaka na kuhifadhi Misitu ya asili.
  • Kuhakikisha kuwa miradi yote inafanyiwa EIA na kuandaa mpango wa usimamizi wa mazingira (EMP).
  • Kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara.
  • Kuhamasisha jamii na kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi ya nishati mbadala, majiko banifu na vyanzo mbadala vya kipato rafiki wa mazingira (Ufugaji samaki,nyuki, kuku, kilimo cha matunda).
  • Kusimamia zoezi la Usafi wa Mazingira kwa kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • SALAMU ZA EID EL FITR

    March 31, 2025
  • DC MBARALI AANDAA HAFLA YA IFTALI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE,TASISI ZOTE NA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUMU..

    March 28, 2025
  • DC MBARALI ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KATA YA CHIMALA

    March 14, 2025
  • KIKAO CHA DCC KUPENDEKEZA MAJINA YA MAJIMBO WILAYANI MBARALI

    March 13, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.