• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Councelors Time Table
      • District Chair Personal Time Table
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Kata ya Mwatenga

HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI

KATA YA MWATENGA

MHE. MASHAKA MGONJWA 

DIWANI WA KATA 


TAARIFA YA KATA YA MWATENGA

1. UTANGULIZI

Kata ya Mwatenga ipo Wilaya ya Mbarali Tarafa ya Ilongo, upande wa Magharibi, umbali wa kilometa 119 kutoka makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali na ina jumla ya ukubwa wa hekta 17172.149. Kata Mwatenga ilianzishwa kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa mwaka 2010 ikimeguka kutoka kata ya Mahongole.

Katika ngazi ya Kata kuna Viongozi ambao ni Diwani wa Kata na Afisa Mtendaji wa Kata na kwa upande wa Vijiji kuna Wenyeviti wa Vijiji pamoja na Maafisa watendaji wa Vijiji.

Kata ya Mwatenga ina jumla ya watumishi 37 wa kada mbalimbali kama ifuatavyo: Utawala 5, Elimu watumishi 25, Afya watumishi 2, Maliasili 1, Kilimo watumishi 2, Mifugo na Uvuvi watumishi 2 na Maendeleo ya jamii watumishi 0.

Kata ya Mwatenga ina Jumla ya Vijiji 4 ambavyo ni Kijiji cha Mwatenga, Kijiji cha Mapogoro, Kijiji cha Igunda Mhwela na Kijiji cha Kilambo. Aidha kata hii ina vitongoji vipatavyo 26 na kaya 2,056.

Kata ya Mwatenga ina jumla ya wakazi wapatao 9,387 kati yao Wanaume 4,855 na Wanawake 4,982. Makabila yanayopatikana katika Kata ya Mwatenga ni wasangu, wabena, wasafwa, wawanji, wanyakyusa, wakinga, wasukuma, wamalila, wanyiha, wataturu na wandali

Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata shughuli za kiuchumi kwa wananchi wake kama ifuatavyo; kilimo, ufugaji na Biashara

Vyanzo vya Mapato katika kata hii inatofautiana kutokana na Kijiji kimoja hadi kingine, miongoni mwa vyanzo hivyo ni kama; faini/adhabu mbalimbali, pawatila za Vijiji, michango ya wananchi, Ruzuku kutoka Serikali kuu (Halmashauri ya Wilaya) pamoja na misaada kutoka kwa Wadau mbalimbali.

Hali ya Ulinzi na Usalama ndani ya kata ni nzuri kabisa kwani hakuna matukio ya kuhatarisha usalama. Aidha kila Kijiji kina Kamati ya Ulinzi na Usalama ambavyo vinafanya kazi usiku na mchana ambapo sambamba na majukumu mengine huhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.

2. HUDUMA ZA KIJAMII ZINAZOTOLEWA PAMOJA NA FURSA ZILIZOPO

 A. ELIMU

Kata ya Mwatenga ina Jumla walimu 25, shule za Msingi tatu (3).

 i. ELIMU MSINGI

  • Shule ya Msingi Uhusiano
  • Shule ya Msingi Mwatenga
  • Shule ya Msingi Kilambo

 ii. ELIMU SEKONDARI

hakuna shule ya sekondari

B. AFYA

Kata ya Mwatenga ina watumishi wa idara ya afya ni wawili (2), zahanati 1 kijiji cha Kilambo kati ya vijiji vilivyopo, magonjwa yanayosumbua mara kwa mara ni ; Maralia, Taifod, UTI na HIV

C. KILIMO, UMWAGILIAJI NA USHIRIKA

Kata ya Mwatenga ina jumla ya watumishi 2 idara ya Kilimo, Umwagiliaji na ushirika, na ina jumla ya wakulima 6,569, wanawake 3,963 wanaume 2,606. Eneo linalofaa kwa kilimo ni hekta 10,330, lakini eneo linalolimwa ni hekta 8,330. Mazao yanayopatikana katika kata ya ni, mpunga, mahindi, karanga, Alizeti, Mihogo, maharage, Nyanya. Tikiti maji na Pilipili Hoho.

Kuna skimu moja tu ya umwagiliaji.

Huduma zinazotolewa na Wataalam wa Kilimo ni ;

  • Huduma za ugani
  • Mashamba darasa juu ya Kilimo cha Kisasa
  • Hifadhi bora ya Mazao ya Chakula
  • Elimu juu ya ushirika
  • Ukaguzi wa vyama vya ushirika pamoja na ushauri wa namna ya kuviendesha na kuvisimamia
  • Kutatua Migogoro ya Wakulima na Wafugaji
  • Elimu ya masoko na stakabadhi ghalani
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya maji
  • Ushauri juu ya matumizi sahihi ya zana za Kilimo na pembejeo
  • Ushauri juu ya Kilimo bora cha Mazao
  • Kukusanya takweimu za Mvua
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji ya kila robo mwaka na kuwasilisha wilayani.
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya Utekelezaji wa Maendeleo ya Kilimo katika Kamati ya Maendeleo ya kata.

D. MIFUGO NA UVUVI

Kata ya Mwatenga ina jumla ya watumishi 2 wa idara ya mifugo na Uvuvi na ina jumla ya mifugo 23,038.

Huduma zinazotolewa na Idara ni pamoja na;

  • Tiba kwa magonjwa dhidi ya Mifugo
  • Huduma mbalimbali za Mifugo kama kuhasi, kukata pembe, kwato na midomo, kupiga chapa Mifugo, kukata meno, kuzalisha, kuogesha na Ukaguzi wa nyama
  • Ushauri juu ya ujenzi bora wa mabanda ya Mifugo
  • Kutoa elimu ya ufugaji bora wa namna ya ufugaji wa Mifugo yenye tija
  • Ukaguzi wa Nyama na usafi katika Machinjio
  • Kusimamia zoezi Endelevu la upigaji chapa wa mifugo

Sekta ya Uvuvi ni mojawapo ya sekta zinazofanya kazi katika kata hii. Idara inaendelea kushauri wananchi juu ya uchimbaji bora wa mabwaya ya samaki kwa ajili ya ufugaji wenye tija.

E. MALIASILI

Kata ya Mwatenga ina mtumishi 1 wa maliasili mpaka sasa ambaye anasimamia Kata ya Mwatenga na Mahongole

 ii. Hifadhi ya Misitu

Kata ya Mwatenga inaendelea kuhamasisha wananchi juu ya ulinzi na utunzai wa hifadhi za Misitu  kwa kupanda miti, kuzuia uharibifu wa mazingira kwa kuchoma mkaa na kukata miti hovyo bila ya kuipanda upya, pamoja na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya uoteshaji na upandaji miti.

 ii. Mikakati ya uhifadhi wa mazingira pamoja na faida inayopatikana kutokana na uhifadhi huo. 

Kata inaendelea kutoa hamasa kwa wananchi pamoja na taasisi kuhusiana na kuendelea kulinda mazingira hasa maeneo ya vyanzo vya maji kwa matumizi Endelevu, kuendelea kushauri kutengwa kwa Bajeti kwa ajili ya uoteshaji na upandaji wa miti katika Vijiji

F. MAENDELEO YA JAMII

Kata ya Mwatenga haina watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii mpaka sasa, huduma zinazotolewa na kata ni kama ifuatavyo;

  • Uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka 5
  • Elimu ya ulinzi na usalama wa mtoto
  • Elimu ya kupinga ukatili kwa akina mama na watoto
  • Kutetea haki za wazee, watoto na jamii kwa ujumla
  • Kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya
  • Kuhamasisha wazazi kupeleka watoto shuleni
  • Kufuatilia shughuli za kiuchumi zinazofanywa na wanufaika wa Tasaf
  • Kufuatilia Utekelezaji wa Kamati za ukimwi vijijni (VMAC)
  • Kuhamasisha Wanawake, Vijana na Walemavu juu ya shughuli mbalimbali za ujasiliamali
  • Kuhamasisha shughuli za Maendeleo kwenye mikutano na vikundi
  • Kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo vijijini.

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018 SHULE ZA WILAYA YA MBARALI MKOA WA MBEYA January 24, 2019
  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2018 HAYA HAPA January 24, 2019
  • JARIDA LA MIFUMO YETU - OFISI YA RAIS TAMISEMI January 22, 2019
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSIANA VYETI VYA KUZALIWA KWA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 5 NA ZAIDI YA MIEZI 6 September 10, 2018
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC amshukuru Mdau wa Maendeleo kwa Kuguswa na Uhaba wa Madawati

    February 18, 2019
  • MAWAZIRI 8 WATUA MBARALI KWA AJILI YA MPAKA WA HIFADHI YA TAIFA RUAHA

    February 15, 2019
  • Baraza la Madiwani Lapitisha Bajeti Bilion 39.3

    January 29, 2019
  • Baada ya Miezi 8 tutaanza kupata huduma kwenye Hospitali yetu Mpya ya Wilaya- Mfune

    January 24, 2019
  • Tazama

Video

KUHITIMISHA MAFUNZO YA MGAMBO KATA YA MAWINDI TAREHE 16/11/2018
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255713317374

    Barua Pepe: ded.mbarali@mbeya.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Hatimiliki ©2018 GWF. Haki zote Zimehifadhiwa.