• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Fanyeni Kazi kwa Bidii kwa Kutumia Taaluma zenu-DC Mbarali

Tarehe ya Kuanza: January 30th, 2021

Hayo yamesemwa na mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune alipokuwa akiongea na Wenyeviti wa Bodi za Shule za Sekondari, Waratibu Elimu Kata pamoja na Wakuu wa Shule za Sekondari kwenye kikao cha tathimini ya matokeo ya mitihani ya Taifa ya kidato cha Sita, kidato cha Nne pamoja na Kidato cha Pili siku ya tarehe 29/01/2021 katika ukumbi wa shule ya Sekondali Rujewa.

Katika kikao hicho Mhe. Mfune amewataka walimu wote kufanya kazi kwa bidii, weledi na kwa kutumia vizuri taaluma zao ili kuongeza ufaulu kwenye mitihani inayokuja.

 

“Tunajituma sana, ila kama tunajituma bila ubunifu ni sawa na sifuri, na hatutaweza kusonga mbele. Pamoja na mafanikio tuliyoyapata tusiamini kwamba hapa tulipo tumefika, tuendelee kufanya kazi kwa bidii na ubunifu mkubwa ili tuongeze kiwango cha ufaulu”

 

“Mimi pamoja na viongozi wenzangu wa Wilaya ambao tumekuwa tukihudhuria vikao mbalimbali tumechoka kuwapigia wenzetu makofi, kwa nini iwe hivyo siku zote? ifike muda na sisi tuwe tunapigiwa makofi kwa ufaulu mkubwa na kushika nafasi za juu.” Alisema Mfune.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma Msangi alisema kwamba kwa sasa Mbarali kuna shule nyingi za Serikali zimeongezeka za binafsi na za Serikali.

Ndg. Msangi aliongeza kuwa walimu wote watakaokuwa wanafaulisha wanafunzi kwenye masomo wanayofundisha ufaulu wa daraja A na B watakuwa wanapatiwa zawadi kama motisha na Ofisi yake.

 

“Mbarali tuliikuta ina shule 16 za sekondari za Serikali, mwaka 2019 tumeongeza shule 2, mwaka 2020 tumeongeza shule 6 na mwaka huu 2021 tunaongeza shule 4. Kati ya shule hizo nne shule moja itakuwa ni wa wasichana tupu itakayoitwa Uturo Girls ambayo itakuwa inachukua wasichana 80 bora. Baada ya kumaliza hiyo tutajenga na ya wavulana ambayo pia itakuwa inachukua wavulana 80 bora” Alisema Msangi.

Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Bi. Anna Shitindi alisema kuwa kwa mwaka 2021 ofisi yake imejipanga kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari kwa kuhakikisha wanaandaa mitihani ya awali kabla ya mitihani ya taifa, kuhakikisha shule zote zinatoa chakula cha mchana, kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa shule zote  pamoja na kutoa tuzo kwa wananfunzi na walimu watakaofanya vizuri

Bi. Shitindi aliongeza kuwa sasa kuna jumla ya shule 32 za Sekondari, kati ya hizo, shule 24 ni za Serikali na shule 7 ni shule zisizo za Serikali vilevile shule za kidato cha tano za sita zimeongezeka kutoka shule 3 kwa mwaka 2019 hadi shule 5 mwaka 2021.

Katika kikao hicho majadiliano ya kina yalifanyika na maazimio kuwekwa kwa ajili ya kuboresha Taaluma kwa shule za sekondari.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.