• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Tuache kupeleka kadi zetu za BANK kwa watu wa mitaani-Msangi

Tarehe ya Kuanza: October 6th, 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Ndg. Kivuma H. Msangi, amewaasa baadhi ya walimu wanaopeleka kadi zao za  Bank (ATM) kwa watu wa mitaani kama dhamana ili waweze kukopeshwa fedha kuacha mara moja kwani shida haziishi na fedha hazijawahi kutosha vilevile wanaidhalilisha kada ya ualimu.

Ameyasema hayo siku tarehe 05/10/2019 kwenye maadhimisho ya siku ya walimu duniani ambapo kiwilaya yamefanyika katika kata ya Rujewa.

“Walimu wengi wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu, moja ya sifa ya Walimu ni ustahimilivu, vilevile Walimu ni watu wa kujitolea, kupitia hayo yote kada ya ulimu imekuwa na umuhimu na ina heshima, hata viongozi siku zote wamekuwa wakiwakumbuka walimu waliowafundisha. Walimu msikate tamaa, tunafahamu kuwa mazingira yenu ya kazi ni magumu”

Naye katibu wa Chama cha Walimu (CWT) Wilaya ya Mbarali Bi. Melea Nyang’uye alisema kuwa, siku ya Walimu Duniani ilianzishwa na Rais wa India mwaka 1967 na ikawa inaazimishwa katika siku ya kuzaliwa kwake yaani tarehe 5 Septemba lakin baadae ikabadilishwa na kuwa tarehe 5 Oktober na kwa upande wa Tanzania Chama cha Walimu kilianza rasmi mwaka 1996.

Bi. Melea amewataka Walimu kuishi katika maadili ya kazi zao kwani zamani mitihani ya darasa la saba ilkuwa inatumwa kwenye bahasha ya kaki na hakukuwa na ulinzi wala mtu wa kuilinda kwa sababu Walimu walikua na maadili mazuri lakin siku izi mitihani hyo inafungwa pamoja na ulinzi mkali na silaha za moto na hii ni kutokana na kuporomoka kwa maadili ya Walimu ikiwemo swala la kuvujisha mitihani.

Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Wilaya ya Mbarali Ndg. Issa Shemgei alisema kwamba msingi mkubwa wa siku ya Walimu ni sherehe na tafakuri ya jinsi gani ya kuenenda majukumu yao kwani kwa miaka kadhha ya nyuma alikuwa anapokea kesi zisizopungua 20 kwa mwaka za utovu wa nidhamu kwa walimu, lakini mwaka 2018 -2019 kesi zimepungua na ameweza kupokea kesi 6 tu ambapo kati hizo walimu 3 wamefukuzwa kazi na amewapongeza Walimu kwa kujitambua na kufanya kazi zao za msingi kwa weledi.

Maadhimisho yalianza kwa kwenda kutoa huduma katika Hospitali ya Wilaya ya Mbarali ambapo walitoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa, kufanya usafi eneo la Hospitali pamoja na kuchangia Damu. Sambamba na hilo kulikuwa na michezo mbalimbali kama, Kuvuta Kamba, kukimbia kwenye magunia, kukimbia na Gololi zikiwa kwenye Kijiko, kukimbiza Kuku, kucheza Draft pamoja na kucheza Bao.

MWISHO

Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.