• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
Mbarali District Council
Mbarali District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhimira
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Fedha
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Ujenzi
      • Elimu Msingi
      • Uchumi Mipango na Takwimu
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo
      • Elimu ya Sekondari
      • Afya
      • Maji Vijijini na Taka Ngumu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mazingira na Taka Ngumu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Elimu Msingi
      • Elimu ya Sekondari
    • Huduma za Maji
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
      • Kata ya Mahongole
      • Kata ya Ruiwa
      • Kata ya Imalilosongwe
      • Kata ya Igurusi
      • Kata ya Itamboleo
      • Kata ya Mwatenga
      • Kata ya Kongolo Mswisi
      • Kata ya Mawindi
      • Kata ya Luhanga
      • kata ya Madibira
      • Kata ya Utengule Usangu
      • Kata ya Igava
      • Kata ya Rujewa
      • Kata ya Mapogoro
      • Kata ya Ipwani
      • Kata ya Miyombweni
      • Kata ya Ubaruku
      • Kata ya Lugelele
      • Kata ya Chimala
      • Kata ya Ihahi
    • Kamati za Kudumu
      • Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Kudhibiti UKIMWI
      • Kamati ya Maadili
    • Time Tabe
      • Ratiba ya vikao vya wah.Madiwani
      • Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi Itakayotekelezwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
      • Muongozo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Wateja
    • Mikakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu
      • Fomu za Maombi
    • Miongozo
    • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

WATENDAJI MBARALI WASAINISHWA MIKATABA YA LISHE KUOKOA AFYA YA MAMA, MTOTO

Tarehe ya Kuanza: July 24th, 2019

Watendaji wa Kata zote 20 zilizopo ndani ya Wilaya ya Mbarali, wametia saini mkataba wa kulinda Afya ya Mama mjamzito, mama anaenyonyesha pamoja na Mtoto mwenye umri wa chini ya miaka mitano  katika maeneo yao siku ya tarehe 23/07/2019 ikiwa ni muendelezo wa zoezi lililoanza katika ngazi ya Taifa, Mikoa, Wilaya na sasa ngazi ya Kata na Vijiji.

Akiongea katika zoezi hilo la kutiliana saini, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune alisema pamoja na jitihada zilizochukuliwa na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo, hali ya utapiamlo na udumavu  bado ni kubwa hususani katika makundi ya watu wenye mahitaji maalumu ya lishe.

Aliongeza kuwa ukishakosea mwanzoni katika siku za mwazo ambazo ni siku 1000 tangu kutungwa kwa mimba  hakuna tiba na unaweza ukamlaumu kila mtu kuhusu maendeleo ya mtoto na kupelekea kuwaonea wivu watoto wa wengine watakavyokuwa wanafanya vizuri darasani.

“Katika mikutano yote Waheshiwa Madiwani, tumieni mikutano hiyo kuelezea masuala ya lishe, lishe iwe agenda ya kwanza, muwatengee wataalamu wa  lishe katika maeneo yenu muda wa dakika 10 ili waeleze kwa kifupi masuala ya lishe  kwani  watoto wanazaliwa kila siku, hili ni jambo endelevu ambalo halitafika mwisho”


“Walengwa wakuu wa mkataba wa lishe ni watendaji wa kata, watendaji wa vijiji pamoja na maafisa maendeleo ya jamii kama waratibu wa masuala ya lishe kwa ngazi ya kata na vijiji ili kukamilisha hatua zote za uwajibikaji na usimamizi wa utekelezji wa masuala yote ya Lishe kwa ajili ya kuokoa Taifa.”


“Ninawaagiza kuhakikisha yale yote yalioandikwa kwenye mikataba yenu yanatelezwa na kusimamiwa kwani tathinimi itafanyika hadi kwenye ngazi ya kijiji. Ili tuwe na  watu wabunifu, wenye ujuzi wa kutosha kwa maendeleo ya Taifa suala la lishe ni jambo muhimu sana  ” alisema


Mkutano huo wa kutiliana saini kati ya Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi Mtendaji pamoja na Watendeji wa kata ulihudhuriwa na Waheshimiwa Madiwani, mwakilishi wa shirika lisilo la kiserikali la CRS, Afisa Lishe kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Maafisa maendeleo ya jamii pamoja na baadhi ya wataalamu kutoka ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halamashauri ya wilaya ya Mbarali.

Serikali inatekeleza mpango jumuishi wa Lishe wa Taifa wa miaka 5 ulioanza mwaka 2016/2017 -2020/2021 sambamba na kufanya tathimni ya utekelezaji wa makubaliano chini ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kwani Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI aliagiza mikataba ya Lishe isainiwe na Watendai wa ngazi ya Vijiji pamoja na Kata

Suala la Lishe ni la kila Mwanadamu, ila mkataba huu unawahusu akina mama wajawazito, akina mama wanaonyonyesha pamoja na watoto ambao hawajafikisha umri wa miaka 5.
MWISHO



Matangazo

  • UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA, NOVEMBA 27,2024 October 20, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI October 17, 2024
  • MPANGO MKAKATI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MBARALI 2018_2019- 2022_2023 June 08, 2022
  • MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELO KIASI CHA SHILINGI 1,010,267,500.00 March 13, 2021
  • Tazama

Taarifa Mpya

  • DC MBARALI UFUNGUA MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA KATA YA ITAMBOLEO

    May 22, 2025
  • ZIARA YA WAHESHIMIWA MADIWANI WA MBARALI KUJIFUNZA BIASHARA YA HEWA YA KABONI

    May 22, 2025
  • ZIARA KAMATI YA SIASA YA MKOA WA MBEYA WILAYANI MBARALI

    May 13, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI

    May 16, 2025
  • Tazama

Video

MBUNGE MBARALI ATOA MILINI 120 KWA AJILI YA SARE WANAFUNZI WOTE WALIOFAURU KIDATO CHA KWANZA
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Google
  • SAIRLA TANZANIA DASHBOARD

Tovuti Mashuhuri

  • RAS Mbeya Web Site
  • Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Salary Slip Portal

Ramani kwa wasafiri

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

writingMasterThesis

Ramani ya Sehemu

Wasiliana Nasi

    Rujewa Road 3 km from main Road: Then Drive Mkurugenzi road. 1

    Sanduku la Posta: 237 Rujewa Mbeya

    Simu ya Mezani: 252957440/252957447

    Mobile: +255784 906 216

    Barua Pepe: ded@mbaralidc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma Zetu

Copyright ©2021 GWF . All rights reserved.